Nimrejeshee nini mamsapu!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimrejeshee nini mamsapu!?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Jun 28, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimrejeshee nini mamsapu!

  Wakati ule tulipoanza mahusiano, yeye aliniambia amewahi kuwa na mahusiano na mtu mmoja tu ambae hata hivyo hakudumu nae muda mrefu. Nilipomtizama usoni, alionyesha wazi kabisa ni mwenye kauli ya uaminifu..kama kawaida ya wanaume nikamkazia macho na kumuuliza tena lakini akaisimama kwenye kauli yake moja tu " I swear, nakuambia na sina sababu za kudanngaya".!!..wakati huo mimi nilikwisha kuwa na mahusiano yaliyiosambaratika na zaidi ya wanawake sita (wote wakitegemea tutakuwa pamoja milele daima!! lakini wapi!). Sikumweleza undani mpaka miezi kadhaa ikakatika....wakati huo mmoja ya wanawake niliyokuwa nahusiana nae kabla tayrai alikuwa na ujauzito..dhamira ilinisuta, nikamweleza ma-msapu kuwa kabla hatujaendelea na uhusiano mimi nina mwanamke ana ujauzito lakini sidhani kama anatanifaa kuliko yeye..akalia sana baadae akasema" basi bwana mimi sitaweza, wewe endelea..." nilimsihi sana kuwa mimi sina tena uhusianao na yule mwanamke niliyempa mimba.

  Baada ya siku mbili akaniambia hana jinsi, tuendelee..wakati tukikaribia kufunga ndoa, yule mwanamke niliyempa ujauzito akajifungua baby boy, awali ilikuwa vurugu kwa upande wa kwao wakitaka niwe napeleka matunzo ya mtoto, simu na sms zilikuwa haziishi kama sijapeleka matunzo. Mamsapu akanishauri nimchukue mtoto tuishi nae, nilisita nikijua labda ahatamlea vizuri kwa kuwa si wake..mtoto akiwa na miaka miwili na nusu tu nikamchukua...wakati huo pia mamsapu akanishauri nimchukue na mdogo tuishi nae ..nalo nilisita lakini yeye akalazimisha, siku moja niliporejea safari nikamkuta dogo katinga nyumbani na nyumba imekuwa na furaha ya ajabu sana ...Hakika sasa ni mwaka wa nane anaishi na mtoto wa mwanamke mwenzie na wa kwake kama wote kawa zaa mwenyewe , huwezi kujua kama kuna tofauti ya mama ..anamlea vizuri sana kiasi cha kwamba nami naona myo wake ni wa ajabu sana!.

  Mama ya mtoto aliolewa lakini wakati alibahatisha kuja nyumbani akataka kuleta fujo akimtaka mwanae..mamsapu alighazabika sana kiasi cha kutaka kumrusha makonde kwa matamshi aliyomtolea...Hakika sijui nimrudishie nini mamsapu kwa ukarimu anaonitendea!!!.Najua ni wanawake wachache sana wanaweza kuwa na roho ya kutojali na kubeba jukumu linalotokana na dhambi za wengine huko nyuma ikiwemo kuishi na watoto wasio wao.

  Yeye si mtu wa kabila la kwetu, wakati ule naingia nae katika pingu za maisha baadhi ya ndugu akiwemo mwanamke mwenzie (mama yangu mzazi) waliniambia pengine niwe makini anaweza asikubali kuishi na mtoto asie wake, asiwe mkarimu kwao na mimi pia nk..lakini sasa najua kumbe mkeo ni zaidi ya mtu mwingine yeyote, yeye ndie anaweza kukuhudumia hata ukiwa unashindwa kitandani, ndie anayeweza kuvumilia mapungufu yako, akakubali kuzoa matapishi yako ukiwa na afya au mgonjwa, akaivumilia harufu mbaya ya pumzi zako za ulevi, sigara, jasho, soksi au ubovu wa meno
   
 2. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,712
  Likes Received: 8,263
  Trophy Points: 280
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Glory be to God,.......good woman
   
 4. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  nakushauri ukawapime DNA na hao uliozaa nae, wanawake hawaeleweki huenda amesha neutralize kwa kukubambikia na wewe mtoto bila kujua ndio maana hana kinyongo usichukulie poa kirahisi tu. Ni mtazamo tu washikaji msijenge chuki
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Wanawake wameumbwa na mioyo ya huruma sana!
  mshukuru Mungu kwa kukupatia mke mwema!
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mpe heshima yake na usije rubuniwa maana hamchelewi mkiona vicheche na mkipata vijicent.
   
 7. l

  ladywho Senior Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Uwe mwaminifu kwake daima!
   
 8. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu DNA ya nini bhana wakati watoto wamezaliwa chumbani mwako na pengine katika maisha unaweza kuishi na watu baki (wasio wa damu yako) na ukakaa nao kama wanao...kwa mfano wajomba nk? Ukijua mtoto ni wako inaongeza nini au ukijua si wako wakati tayari uliamimi ni wako huoni athari zake kwako na familia kwa ujumla hasa hao watoto wasio na hatia ambao pengine walikwisha kukupenda na kukuheshimu kama baba yao? .

  Mkuu hujui wakati fulani watoto wa mwenzio ambao umewalea vizuri wanaweza kuwa na heshima na msaada mkubwa kwako kuliko wanao uliowazaa? Zipo familia nyingi sana sasa ambazo watoto hawawaheshimu kabisa wala kuwajali wazazi wao kwa chochote kile na pengine kusema hawakuzaliwa na wazazi hao. Tunajifunza na kupata nini kwa wale tuliowazaa kama hatuwezi kuwapenda hata wale tusiowazaa? ...

  Waache tu baha waendelee kuniita baba na mie nawaita wana wangu hata kama chakachuzi (but not to this woman!!) ..mambo ya DNA haya ni kujalibu kufukua matatizo yasiyotarajiwa.
   
 9. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  i love this coment hata sikuwa na wazo kama hili
   
 10. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mpende na kumuheshimu na kumthamini sana,
   
 11. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huna cha kumrejeshea,sifa na utukufu zimuendee muumba aliyekujalia hayo!Upendo wa dhati na Nidhamu kwa ndoa yako viujaze moyo wako!
   
 12. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mpende sana, mheshimu pia mthamin kwa kuwa utambua thaman yake kwako, Big up uyo mkeo maana ni wanawake wachache sana tupo hivyo.
   
 13. A

  Aine JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Muonyeshe upendo wa dhati na usitoke nje ya ndoa
   
 14. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,712
  Likes Received: 8,263
  Trophy Points: 280
  Mhhhh!????????????!
   
 15. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Huyo hakika ni mke mwema.
  Kaa ukijua kuwa naye kama binadamu wenhgine ana mapungufu yake. Usisite kumsamehe kila anapokukosea, mwite na umuonye kwa upole.
  Umesikia mtoto mzuri?
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  ngoshwe, wanawake wengi ni wema,hasa ambao hawakuumizwa kabla. ni jukumu lako kumuonesha upendo wa hali ya juu na kumheshimu (hata pale hela zitakapokutuma vinginevyo), zaidi ya yote hakikisha huleti mtoto mwingine tena nyumbani maana nakuhakikishia utakuwa umejivurugia eden yako. mkeo anakupenda, ni muaminifu na anakujali. love begets love, naamini ni kwa sababu na ww umemuonesha upendo pia. kila la kheri, Mungu akusaidie usiharibu maana shetani mshtaki wako yuko macho uteleze ili akuumbue!
  nimekoshwa sana na mtizamo wako juu ya DNA. kuna sehemu kama biological father lakini kuna urafiki na upendo unaojengeka mara baada ya mtoto kuzaliwa. kwa positive attitude hiyo, u will reach height! kila la kheri
   
 17. The great R

  The great R Senior Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoshwe ni wako ndio mana wamwona watofauti.
  Ila kilichookoa hapo ni kwamba ulimwambia mapema,jambo zuri sana.
  Angegundua mwenyewe baadae ungeona mziki wake,nakupongeza kwakua mwanaume jasiri na kumweleza mkeo uhalisia wa mambo sasa changamka mpate wa pamoja furaha itanoga zaidi.Unajua ndoa ninini safi sana bro
   
 18. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  shwari mkuu namjari sana kwa jinsi anitendeavyo.
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Mmmmmmmmh!!! Hili la kwanza sidanganyiki hasa ukizingatia kuwa nimeishi na mama wa kambo machachari nikiwa na umri mdogo sana. Na kile kibano chake mpaka leo miaka takriban 30 baadaye bado nakumbuka utadhani kimetokea mwaka jana. Hilo la pili la kumshukuru mungu naunga mkono hoja.
   
 20. T

  Tata JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  DNA inafaa kama unatafuta hoja za kuachana na mwenzi wako. Vinginevyo sioni kama ina umuhimu. Kwa mila na desturi za kabila letu ukizaa na mke wa mtu ni sawa na mpumbavu tu anayepanda mbegu za mazao jangwani halafu anatarajia kuvuna. Kwa mujibu wa sheria zetu za kimila wewe mzaa hovyo huna haki yoyote na mtoto na anabaki kuwa ni wa kwenye familia alikozaliwa. Hivyo baba mwenye mke hana haja ya kuwa na wasiwasi kwani watoto wote kwenye mji wanabaki kuwa mali yake halali. Ndio maana mila ya kuoa wengi inaendelea kudumishwa bila matatizo.
   
Loading...