NIMR: Asilimia 45 ya watoto wachanga wakutwa na Virusi vya homa ya ZIKA Tanzania, asema Mwale Malecela

Sasa homa ya zika ikapoteaje bila ya jitihada zozote za kuwatoa mbu wanaosababisha hiyo homa ya zika au walikuja kama watalii tu na kuondoka?

Hawa jamaa wanapenda mambo rahisi kweli matatizo yote yanayoikabili sector ya afya kipindi hiki wanakuja hadharani na habari za homa ya zika.
 
Tanzania ina serikali ya kipekee.
NIMR,Taasisi ya serikali ya utafiti imefanya kazi yake na kuijuza nchi,kuwa virus vya ZIKA vipo.
Ghafla Naibu waziri,Dr.Kigwangala anatoka hadharani na kupinga ripoti ya NIMR!!!!Just one day bila hata ya site visit,!!!!
A failed system !!
Hivi Ummy ni darasa la ngapi?
 
Tanzania ina serikali ya kipekee.
NIMR,Taasisi ya serikali ya utafiti imefanya kazi yake na kuijuza nchi,kuwa virus vya ZIKA vipo.
Ghafla Naibu waziri,Dr.Kigwangala anatoka hadharani na kupinga ripoti ya NIMR!!!!Just one day bila hata ya site visit,!!!!
A failed system !!
Duh! Nilijua tu kuwa ni chezo hili, sasa tumwamini?
 
Mkurugenzi wa NIMRI dk Mwele Malicela anasema wamefanya uchunguzi na kugundua ugonjwa huo upo Tanzania,Ummy Mwalimu na Hamis Kigwangala wanasema haupo.Ni nani yuko sahihi?
Ok, JPM katengua uteuzi wa Mwele usiku huu. Natumaini sasa unaelewa nani yuko sahihi!
 
1.jpg


Pichani ni watoto wadogo ambao vichwa vyao ni vidogo kupindukia kwa
mujibu wa mdau Mpoki Bukuku aliyenishushia habari hii hivi punde.

Wadau kwa niaba ya mdau Mpoki Bukuku aliyeniletea habari hiii hivi punde ni kwamba
kuna watoto wa ajabu wamezaliwa kama muonavyo pichani ambao ni wa Bi Sophia Lipeleta mkazi wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi ambaye alifika ofisi za gazeti la mwananchi hivi punde kwa nia ya kuomba msaada kwa wasamaria wema kwani watoto wake hawa hawawezi kuongea japokua wana umri mkubwa na kuomba kama kuna mtu atapenda kufanya utafiti anaweza kuwafanyia na kujua tatizo, lakini wako Dar na hawana chakula wala pa kulala kwani hivi sasa wanalala stendi za mabasi. Mama yao anaomba msaada wa hali na mali,nami nimeona niungane na ndugu yangu Mpoki Bukuku kuomba msaada kwa wasamaria wema ili tuwasaidie watoto hawa.
Kwa wale wenye nia ya kuchangia watoto Hawa Mnaweza
kumpigia Simu Mpoki Bukuku kupitia Number hiii
+255222450878 au Fax +255222450886
E-mail:mpokibukuku@yahoo.co.uk
2.jpg
Mama Sophia Lipeleta mkazi wa Nachingwea Mtwara akiwa na watoto wake walemavu pichani na kueleza kuwa alikuwa na watoto saba wa aina hiyo sasa wamebaki hawa watatu baada ya wengine kufa.
3.jpg
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida.
 
Huu ugonjwa Tanzania upo muda mrefu tu, ila ulikuwa haufuatiliwi. Kuna dogo mmoja yupo kama hao wa kwenye picha ni mkubwa tu. Ila kuibuka kwa kasi huko Amerika ndio kumetushtua.
 
,
Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela,virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.

Dkt Mwele Malecela alizungumza na BBC na anafafanua kugundulika kwa virusi hivyo.


Chanzo: BBC
Fedha za wafadhili zinatafutwa
 
Wataalam wa Afya hapa Tanzania wanajua sana kutumia fursa. Mara Dengue imeingia, mara Mafua ya Ndege yameingia, Mara tezi Dume imeshamiri, Mara Homa ya Ini karbia sote tunayo nk nk. Vyooote hivyo ni Kutafuta International Attention ili kupata fedha za Miradi. Wapi MEWATA na Kansa ya Ziwa.....hhahahaaaa nafikiri hawa wakifanyiwa Audit na CAG watakimbia Nchi. Kwa suala la Zika acheni wadau wapige zumari wafadhili waje. Safi sana wataalam wa afya.
Pesa ya bill gate inatafutwa!
 
Huu ugonjwa mara ya mwanzo uligunduliwa nchini Uganda miaka mingi iliyopita. Sishangai kuskia Tanzania upo na inawezekana upo zamani.
 
Hao watoto, naliwaona magogoni feri mle kwenye jumba la kusubilia kivuko wasafiri, na nikahisi kwamba hii ndio zika, ila kwa Tanzania tulikuwa bado hatujagundua ndio maana ikawa hivyo. Sasa kwa mfano huo, huyu Waziri wa Afya ataongea nini? Au anachuki na huyo Dada, au!! Bado mimi sijaelewa, atoe taarifa ya kupinga na Mh Rais anatengua hapo hapo. Jamani hii Tanzania yetu wote, power no permanent.
 
Back
Top Bottom