kwani hiyo taasisi bosi wake ni naniTanzania ina serikali ya kipekee.
NIMR,Taasisi ya serikali ya utafiti imefanya kazi yake na kuijuza nchi,kuwa virus vya ZIKA vipo.
Ghafla Naibu waziri,Dr.Kigwangala anatoka hadharani na kupinga ripoti ya NIMR!!!!Just one day bila hata ya site visit,!!!!
A failed system !!
Kama ni kweli, wabongo tumeisha. Sasa hivi hospitali hamna dawa ndio ZIKA inaingia ! Kweli tuta-zika wengi. Na hali ilivyo ngumu hata hela za vidonge vya kutuliza maumivu hakuna. Na kama ZIKA ipo, watalii ndio bye bye! Uchumi utazidi kudorora. Tena ukame ndio huo, na pale ambapo hakuna ukame kuna mvua za ghafla zinazobomoa majengo. Tutaishije?
Likitokea janga nani atatutaarifu?Na bosi aliyetangaza katumbuliwa. Hakuna mswalie mtume!
Wakati mwingine tutapinga hili kwa nguvu kubwa ili tu tusiathiri watalii ingawa itafiti uko sahihi.
Tafiti,
Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela,virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.
Dkt Mwele Malecela alizungumza na BBC na anafafanua kugundulika kwa virusi hivyo.
Chanzo: BBC