Nimjibu vipi anielewe?

Nimjibu vipi anielewe?

Naomba namba ya huyo msichana nimwambie badala yako
 
kaa kimya. ulimtongoza kakataaa sasa unataka uanze kujitetetea ili iweje. bado unampenda????
 
Mwambie mimi na wewe si mtu na kaka yake
 
Habari wanaMMU,


Ni hivi, wakati nikiwa chuoni nilitokea kumpenda binti mmoja mzuri, toto la Kipare.Katika maisha yetu ya pale chuoni tulikuwa tukishirikiana kwa kila hali, iwe kimaisha na hata kimasomo pia.Ilifika wakati ikabidi nivunje ukimya na kumtakia lililokuwa moyoni mwangu, alichukulia masihara nilipomwambia kwamba nampenda na yeye akadai kwamba hawezi kuwa mpenzi wangu ilhali yeye kanizoea mimi kama kaka yake.

Nilipoona msimamo wake umekuwa mkali basi nikaamua kutupa karata yangu kwa msichana mwingine wa palepale chuoni ambaye kiukweli alinielewa na tukaanzisha naye mahusiano. Nilitangulia kumaliza chuo nikamuacha bado akiwa masomoni.Sasa cha kushangaza siku ya Leo nimepokea message kupitia akaunti yake ya Whatsapp akiwa amenitumia picha ambayo ameidownload kutoka kwenye profile ya huyo mpenzi wangu ambaye walikuwa wakisoma wote akiniambia " Unajua hii picha nimeitoa wapi? Nashukuru Mungu niligundua hunipendi".

Wakuu sijamjibu chochote mpaka dakika hii na ikumbukwe nikiwa chuoni sijawahi mtongoza msichana yeyote kabla yake, nilikuja kuanzisha mahusiano na msichana huyu wa sasa baada ya yeye kunikatalia.Nashindwa kujua ana lengo gani ilhali alishanikatalia tangu mwanzo na mimi nikayaheshimu mawazo yake.Nahitaji ushauri wenu namna gani nitamjibu kwa busara anielewe pasipo kumkwaza au kumgombanisha na huyu mpenzi wangu.

Natanguliza shukrani, samahani kwa habari ndefu

Kati ya huyo binti wa mwanzo na huyo uliyenaye yupi unampenda zaidi???.
 
Ulitaka akijibu harak?alivyo kukatalia ulitakiwa kuvuta subra sasa wewe ulikurupuka hataingekua mm ningejua hukunipenda ungempenda kweli usinge tongoza mwingine ungeendelea kumsumbuwa.
 
Ulitaka akijibu harak?alivyo kukatalia ulitakiwa kuvuta subra sasa wewe ulikurupuka hataingekua mm ningejua hukunipenda ungempenda kweli usinge tongoza mwingine ungeendelea kumsumbuwa.
Time factor ni muhimu kuzingatiwa. Wa kwanza alikuwa mzito kutoa maamuzi kwa hasara yake. Ushauri ni kuwa kijana asirudi nyuma, atajiletea mikosi

Amen
 
Time factor ni muhimu kuzingatiwa. Wa kwanza alikuwa mzito kutoa maamuzi kwa hasara yake. Ushauri ni kuwa kijana asirudi nyuma, atajiletea mikosi

Amen

nashukuru kwa ushauri wako mkuu!
 
Ila jamani, sasa kama hapo unauliza nini, au unamtaka na huyo tena, unataka wadau wakupe tiketi. Mwambie picha umeitoa ktk profile ya mpenzi wangu, na wewe nilikupenda lakini hukunitaka, hivyo huna nafasi kwangu tena, utabaki kuwa kama dada yangu tu, sawasawa na vile ulivyonambia kipindi tunasoma, kuwa umenizoea mimi kama kaka yako.
 
Search your heart. The answer lies in you.

What do you want. From there you will know what to do.
 
khaaaaaaaaaaaa mjibu hivi "pruuuuuuuuuuu praaaaaaaa aga woyi woyi woyo woyo" halafu mwambie oyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Back
Top Bottom