Nimjibu nini binti wa aina hii. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimjibu nini binti wa aina hii.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mamushka, Mar 5, 2011.

 1. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Habari za weekend people, nimekosa la kufanya nikaona niulize kwenu wadau Mimi naishi na wadogo zangu wawili wakike na wakiume wakiume anafanya kazi, wakike yuko chuo ila anafungua mwezi huu ataondoka. Sasa tuna house maid wetu ambaye mimi ndo nilimleta kutoka mwanza vijijini, tumekaa nae muda mrefu sana tu, na kwa vile kati etu hakuna anaeshinda home yani mimi na my brother kazini tunarudi jioni, na mdogo wetu pia alikua ana fanya field sehemu kwahiyo kurudi kwake pia ni jioni. Msichana ghafla kawa na tabia za ajabu sana, anakiburi, heshima ya kinafki, tukirudi ndo anakua busy na kazi muda wote wa mchana na usiku ni busy na African Magic , lakini kwakua kila mtu yuko busy na mambo yake na uchovu wa kazi pia tunampotezeaga tu. tunaishi nae kama ndugu imemfanya ajisahau sana. Jana mi nilijaribu kuongea nae vizuri tu nikamwambia jinsi alivyosahau kilichomleta hapa ni nini, nikamuonya pia kua mwangalifu na vijanavijana kwani hata usiku huwa anachelewa kulala akiwa busy na simu na snema za ki nigeria, kunapesa nilimpatia apeleke sehem flani akalipe maziwa hakufanya hivyo tokea tarehe1 nimemuuliza akadai ntapeleka kesho yani leo nikaingia zangu kulala. Leo alfajiri mdogo wangu wakiume aliskia milango inafungulia then kuangalia akaona binti anatoka na mabegi, akanigongea room kwangu nikamuona ndo anaishia getini, nikatoka nikawasha gari nikamfuata kwa hofu kwamba akipotea ntajibu nini kwao na niyatima huyo binti. Kwakua nilikua na gari na yeye kwa miguu sikufanikiwa kumpata ikanibidi nirudi home, nikaanza kazi za usafi ghafla naingia jikoni namuona anatoka chumbani kwa mdogo wangu wa kiume nakuja jikoni kuendelea na kazi, nilichofanya nilimuomba anipatie zile pesa, aliponipa nikamwambia naomba ukaniletee mizigo yako ulobeba asubuhi nikukague, then uondoke kwa uhuru kwani ndo maisha ulochagua. Nikamuuliza my brother alifuata nini room kwako? Akanijibu mi nilikua nimelala sikujua kama niyeye nimeskia mtu akiingia na kutoka. Kwenye sasaba mdogo wangu wa kike kampigia akapokea kujua ni mdogo wangu akakata cm, sanane mchana kaanza kumpigia mdogo wangu akiwa analia ana muomba aongee na mimi ili ni msamehe arudi anadai nimegundua nimefanya ujinga na nimemkosea sana dada sina pa kwenda, na mjomba wangu kanigombeza sana kwanini unaondoka kwa huyo dada anaekulea kama mdogo wake. Mimi nimeshindwa kuelewa ni wavlana wake wamemshauri then wamemkimbia? Au kunamtu alimdanganya atampa kazi then kamtosa? Mpaka dakika hii ana m beep my ccta amuombee kwangu ni msamehe arudi, dogo kamwambia njoo uongee nae mwenyewe. Anadai anaogopa nikimkamata ntamrudisha kwao na yeye hataki kurudi. Naombeni mnishauri ni fanyeje juu ya hili, ni mrudishe aendelee na kazi? Au akija nimpeleke kwao? Au ni fanyeje, Asanteni.
   
 2. joellincoln

  joellincoln Senior Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mh kama amekuwa ivyo huwezi jua ameamua kurudi kufanya nini labda wamemwambia asiondoke mpaka apunguze baadhi ya asset zako za nyumbani, usikute wamemwambia we mjinga sana utaondokaje bila kumtia hasara huyo bosi wako? so watch out and be very careful kulia anaweza kuwa anapretend tu, kwanza angekuwa serious angekupigia wewe mwenyewe simu, mtu umemfata akadengua sasa unamtaka wa nini. Nashauri usimrudishe kazini tafuta mwingine. Cha msingi wataarifu wazazi wake, kuwa ameacha kazi mwenyewe na wewe umekubali matokeo, then mpe nauli arudi kwao mwanza basiii. Tena asilale kwako mchukulie hoteli one night akiamka apande ally's bus aende akalime viazi kudadadeki. Anatikisa kiberiti yeye amekuwa waziri wa sheria? mwambie amekitikisa wewe umekiwasha kudraaadeki. Mimi yalishanipata, aliondoka maid after one week akarudi nikamsamehe nilijuta, ndugu yangu kumbe alirudia vitu alinisafisha mbaya, sina hamu kabisa.A liiba vitu vingi sana na alianza mpaka kuleta mibazazi inapigia mzigo palepale nyumbani kwangu nikiwa kazini. So uwe careful tu!
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Pole sana Mamushka....ndo zao kujisahau na hasa wakishapata wanaume wanaowaweka sawa....si tatizo lako mwenyewe...bora na huyo anafanya kazi kuna wengine hata uji wa mtoto anaacha kumpa kisa africa magic mara sijui maria churi ili mradi tu.
  Nakushauri mpe likizo kidogo apumzike....ataona thamani ya kuwa kwako na hayo unayomtendea.....si katingisha kiberiti bwana muonyeshe tu kimejaa....nia yangu ajifunze na ajipe nafasi ya kuelewa umuhimu wako na jinsi unavyomlea kama mdogo wake......somo tosha.

  kama baada ya mwezi....muulize ungependa kurudi au?nakuhakikishia atarudi na heshima juu.....ukimrudisha sasa atarudia huo mchezo.....

  Ila kama unamhitaji sana na huwezi ishi bila yeye,mvumilie au mrudishe akae huku unatafuta mwingine....ukishampata mwingine,mlipe kilicho chake na nauli ya kurudi kwao na muachane kwa amani....ila usimuambie unamtafuta mwingine ukishampata mrudishe kwao kwa uzuri tu......na umsamehe pia.
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Ushauri huu mzuri Mamushka....huwezi jua anarudi kwa lipi? pengine walishamjaza hila huko atokako? hawana shukrani hawa viumbe.....
   
 5. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  rudisha hiyo mutu kwao
   
 6. Bangusilo

  Bangusilo Senior Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu muache arudi, then jipange mridishe nyumbani mapema, atakuletea matatizo zaidi.
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mrudishe kwao bana
  Kaomba msamaha sawa, msamehe ila mwambie umepata mtu mwingine wa kazi
  Machozi yasikuzubaishe, hata wewe ukitaka unaweza ukayaita hata hapo ulipo bila sababu na yakaanza kutoka
  Huyo sio mdogo wako wala ndugu yako kwamba utaweza kumtafuta akileta madhara
  Akikataa tumia ujanja.
  Mtumie huyo huyo mdogo ako mwambie aseme umemsamehe arudi nyumbani
  Akirudi mwambie umepata simu kutoka kwa ndugu zake wanaomba arudi kwao kusalimia then baada ya wiki moja atarudi tena Dar
  Ukifanikiwa kumpeleka kwao unamuacha huko huko
  Kwisha kazi
   
 8. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  kazi unayo...pole sana.....au ana kichaa?.....unaweza kuta ana mizimu ya kwao so kipindi kikifika vinalipuka....hasa wakati wa mawingu yakitanda
   
 9. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mie nimeingiwa na huruma...msamehe,mwache aendelee na kazi atakuwa amejifunza...nakusihi usimrudishe anaweza ht kujiua...

  hahahaa ila hapo uliposema ulimuona anatoka chumbani kwa kaka yako ulinichanganya kidogo,almanusura nianze kumlaumu yeye ndio anampa kiburi hapo kwenu kwa kuduu naye..LOL :A S 13::A S 13::wink2::wink2:
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mrudishe tu kwao.
  Halafu hawa watu sijui kwanini huwa wanajisahau!
  Ukiishi nae vizuri atataka yeye ndio atawale nyumba. Kazi kweli kweli.
   
 11. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thank you my dear, bora nifanye hivo, mpaka sasa hayuko kwangu anambeep mdogo wangu, kibaya zaidi hajui kusoma wala kuandika.
   
 12. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Samahani mamushka, lakini huyo mtot ulimuweka hapo ulitegemea yeye hahitaji ile huduma???? Mwanzoni ulimchukua akiwa mdogo hata yale mambo yetu alikuwa hajui sasa amekua bado unataka a-behave kama mtoto mdogo??? Hebu kuweni na utu kidogo, naona wote mnachangia kumpiga chini huyo binti ila jueni kuwa hata yeye ashakuwa mtu mzima hivyo anahitaji raha kama nyie. Msikilize kwanza uone may be tatizo lake lilikuwa ni ukosefu wa huduma wa muda mrefu sasa akaenda kupata kwa raha zake... Msamehe arudi nyumbani ila mwambie mdogo wako aache kumchakachua......
   
 13. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sawa bosi wangu.
   
 14. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh ok ngoja nijaribu njia hiyo pia, wasiwasi wangu akipata shida tu.
   
 15. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hahaaa mwezi mchanga sio, hana kichaa wala mizimu ulimbukeni tu unamsumbua.
   
 16. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  inaelekea huyo alitarajia kwenda kuhamia
  kwa kidume lakini jamaa amemchomolea
  (usishangae akiwa tayari ana kabebi kwa tumbo).

  wewe msamehe na mpokee kisha hakikisha anapima ujauzito
  akiwa hana ujauzito endelea nae kwani atakuwa amejifunza kwamba
  vidume haviko tayari kumchukua jumla jumla hivyo atakuwa ameweka akili.

  swali: kweli unaamini mdogo wako wa kiume hakujua kwamba binti aliingia
  chumbani kwake? wewe ndio unamfahamu vyema mdogo wako. si vibaya
  ukaangalia uhusiano wao kwani anaweza akawa nae anajipumzisha kwa huyu
  binti na ndio kiini cha dharau kwani wewe ni wifi. yote yanawezekana.
   
 17. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sante sana kwa ushauri wako my dear, ntaufanyia kazi. God bless you.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah wafanyakazi wa nyumbani hua wanachosha wakati mwingine!!!
  Ukishaona hivyo jua kuna mtu anamjaza kichwa mahala and there is no telling ni mtu wa aina gani!!
  Bora umrudishe kwao mapema kabla hujapishana na pick up ikitokea nyumbani kwako!!!!
   
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mrudishe kwao huyo ameshalijua jiji so atakusumbua saaana tuu, vivulana vinamdanganya huyo msichana wa kazi akishakuwa na simu tu baasi kazi ndani hazitafanyika, wauza magenge, mchicha, wauza maji, akina mangi ndo wanawabadilisha hawa mabinti siku hizi hakuna wasichana wa kazi wazuri kabsaaaa
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mamushika,

  Ukicheka na nyani utavuna mabua.

  Rudisha bintii kwao..ikibidi vaa bukta ufanya usafi wa nyumba yako mwenyewe. Saidiana na hao wadogo zako kazi wakati unatafuta msaidizi mwingine. Ukigeuka nyuma ujue unaweza kugeuka jiwe...utalia na kusaga meno.

  Hivi lakini watu mnakuwa na huruma kiasi gani kuwapa hawa wahudumu wa kazi uhuru kwa kuchezea DSTV 100% kama vile wako likizo? Nyumbani kwangu, mwanafunzi na mhudumu wa kazi hana muda wa kuchezea TV labda vipindi maalum tu...Hata watoto wangu hawana hiyo nafasi ya kuchezea TV 100%. Inakuwaje beki tatu anakuwa kwenye TV wakati wote?
   
Loading...