Nimjibu nini binti wa aina hii.

Mh ukweli inawezekana pia, ila lizzy kumbuka hata kusoma hakijui, halafu haijui dar kwani hata outing nimpaka tukitoka wote pamoja ndo tunamchukua, ila unalosema ni kweli, yaweza kua ashapata walimu.

dah! sas kama hajui kusoma hiyo simu anapiga na kupokea tuu?
kazi ipo!
 
Mie huwa ndio sijisumbui na hawa watu, tena wewe huna mtoto mdogo unaona tabu gani? Rudisha kwao utafute mwingine. Hawatabiriki hawa watu na hawana huruma wala adabu
 
Dah!!! Tunachokosea sisi wanadamu tuliopewa Neema ya kuwa na watu wakutusaidia kazi za nyumbani wakati sisi tukiwa na majukumu mengine, ni vile tunavyowachukulia kama watu wasiohitaji kufikiriwa na kusamehewa pale wanapokosea. Ni vile tunawafanya wao ni wakubwa wanajua kufikiria na wakidanganywa kwa nini wamedanganywa wakati hata wewe mtu mzima unaweza ukadanganywa na mwanaume na ukaingia mkenge vile vile.

Kesi yako dada, unasema huyu binti ulimchukua mdogo, ndo anakuwa hivo.....huna muda wa kutosha kukaa naye, yawezekana hujawahi hata kumpa ushauri na kumfundisha jinsi dunia inavyokwenda....ulikuwa ukimuona anakosea unampotezea....sasa angejua je kama anachofanya anakosea??? Ukisema ajue kile kilichomleta unamuonea kama hujamkumbusha na kumpa elimu ya kufikiria maisha na jinsi ya kupangilia mambo. Kuangalia TV sio dhambi lkn afanye kila kitu kwa wakati,, umemfundisha??? Na kama amedanganywa na vijana wa kiume, sio kosa lake pia ni kama wewe na mm tulivyo/tunavyoweza kudanganywa pia...umewahi kumpa Elimu juu ya hilo??? Ulimuona anabadilika ukampotezea si ndio....kwa nini unamlaumu. Kwa nn unataka mtoto wa miaka 18 hata 20 anayekaa ndani kwako na vyombo na TV na viti awe na akili ya kujua dunia inavyokwenda.

Unataka nani amwambie? Viti na meza na makochi na vyombo anavyoshinda navyo na moto na nguo anazofua ndo zimfundishe???? Tuwe na huruma na upendo kwa hawa watu. Sisi ndio tunaowaharibu. Umeongea naye usiku mmoja tu, unataka awe amebadilika??

Sisi tumewahi kukaa na house maid miaka kumi, mpaka akaolewa akiwa kwetu. Sio kwamba alikuwa hakosei ila mama alikuwa anamlea na kumfundisha kama alivyokuwa anatufanyia sisi. Tena yeye alikuwa hachapwi lakini sisi tulikuwa tunachapwa kama nini. Hakuna kusema huyu ni house girl na ukisikika unasema huyu ni mfanyakazi wetu unachapwa....tulikuwa tunamwita dada... Na ametoka ana maisha yake mazuri tu,ana akili za maendeleo ni mmwera lkn ukimsikiliza utadhani mchagga alivyokuwa na mawazo ya kutafuta pesa....amekuwa ni zaidi ya ndugu yetu. Fanya sehemu yako, ukishindwa kitaeleweka na utakuwa umenawa mikono.

Na hata huyu tuliye naye naye sasa hivi, anafanya vizuri kuliko hata mdogo angu tuliyezaliwa naye na ana umri sawa na yeye. Yani utampenda, anafundishika, na nina muda wa kuongea naye, kila jpili mfano tukitoka kanisani, namwambia umuhimu wa kumtegemea Mungu...na muonya pale anapokosea na anaomba msamaha. Hawezi kuwa sawa asilimia mia moja, lkn anopokosea najua kabisa hata mm nakosea kwa hiyo namfundisha na kumrejesha kwa upendo. Yani namshukuru Mungu manake hata majirani wanaona wivu wanatamani wamshawishi lkn kwa jinsi nilivyomweka karibu, anakuja kunambia fulani kanambia hivi na hivi. Halafu nampa shule mapema kuhusu hilo.

SIO UNAPOTEZEA.
JPIL NJEMA!!
 
Pole sana mrudishe kwao dear kabla mambo hayajawa makubwa , tayar ana watu wa pembeni . Hujui wanamfunza nini. Atakufanyia kitu kibaya bure. Mabinti bana wanataka uwanyanyase kama wahindi .
 
Mamushka,
Hii kitu nimeipitia tena wangu nilimsomesha redcross akapanda mpaka sasa nasikia anachukua degree ya nursing muhimbili lkn alichonitenda sina hamu aliniibia kila vitu vyangu vya gold vyote, na matusi juu, lkn hakumaliza mwezi alirudi na mgoti sikumkubali na bahati mbaya alikuwa na mimba ya kijana wa jirani ndo ilimuokoa wakamtunza na kaolewa na anasoma. Ila usimrudishe
 
Sikushauri kabisa kumrudisha hapo kwako. Cha kufanya ni arrangement ya kumrudisha kwao period.

Fahamu kuwa kwa huyo binti kuwa na m/wanaume hakupashwi kufanya ashindwe kutimiza wajibu wake au na kuwa na kiburi kwa mwajiri wake. Ukweli umedhirika kuwa pamoja na kumshauri bado aliondoka kwako na suppose angekuta huko alikoenda kuko sawa basi asingerudi na hivyo angekuweka ktk wakati mgumu. Huyo binti si mstaarabu kama ni kuondoka angekuaga tu

Kwa huyo ni wazi amejiingiza ktk makundi ambayo huyajui. Anaweza kuwaletea wezi au magonjwa. Kama nilivyoshauri mrudishe kwao.
 
the best ni kumsamehe.......
watu wakikosea na kujua makosa yao...
wanaweza badilika....

msamehe kwanza mpe...probation period...
 
mrudishe-cye tulishawah kulazwa milango waz na housmaid,alitoroka late 9t kwenda kwa mabwana,ebu fikiria,ametoka mwananyamala hadi mwenge,then frm mwenge 2 mbez beach,kufika huko kamkuta jamaa ana mwanamke mwingne,akawalaza wote on the same bed,though aliomba msamaha,hatukumuelewa,
 
Mamushka,
Hii kitu nimeipitia tena wangu nilimsomesha redcross akapanda mpaka sasa nasikia anachukua degree ya nursing muhimbili lkn alichonitenda sina hamu aliniibia kila vitu vyangu vya gold vyote, na matusi juu, lkn hakumaliza mwezi alirudi na mgoti sikumkubali na bahati mbaya alikuwa na mimba ya kijana wa jirani ndo ilimuokoa wakamtunza na kaolewa na anasoma. Ila usimrudishe

Mimi pia kujuta ndo naogopa, huruma inaniijia but kama amelala nje jana then ni mrudishe bila kujua elimu alopewa huko aliko mh, yaweza ni cost wangu. Ngoja akirudi ntamsikiliza anachosema.
 
mimi pia kujuta ndo naogopa, huruma inaniijia but kama amelala nje jana then ni mrudishe bila kujua elimu alopewa huko aliko mh, yaweza ni cost wangu. Ngoja akirudi ntamsikiliza anachosema.

kama anajuta kweli msamehe
wasichana wa kazi ndo zao hizo...
Mpaka ajute ndo anajifunza....

Ukiona msichana wa kazi katulia ujue
alishakosea akajuta,
wengine hudanganywa na kupewa mimba.
Hurudi vijijini na kujifungua,
wakija tena mjini,hawadanganyiki tena,
wanatulia....
 
jamani mimi namuonea huruma huyo msichana wa kazi.mpe one more chance,akivuruga basi.binaadamu wote huwa tunakosea na tunajifunza kutokana na makosa yetu,sisi tuna dada wa kazi ambae anakaa na mama yetu,yupo zaidi ya miaka 10.ila kuna kipindi alishawishiwa,akaondoka akapata mimba na akajifungua.dunia ilimfunza,kila anapoenda kutafuta kazi,kwa kuwa ana mtoto wanamkatalia.aliempa mimba akamkimbia.akarudi kwa mama kuomba msamaha,kwa kuwa alikuwa anajua kuitunza nyumba vizuri sana,na kazi huna haja ya kumwambia anazifanya mwenyewe,nikamwambia mama amchukue pamoja na mtoto wake,anakaa yeye na mtoto wake.kwa kuwa dunia imemfunza,yupo nyumbani,na tunampenda kama mdogo wetu.huyo dada mfahamishe,ila akirudia tena ndio basi.ila nina wasiwasi nae kama hatorudia kwani ni bora ungempeleka kwao kwa muda,aijue hali halisi ya maisha,halafu umchukue ukae nae
 
kama ni yatima mbna unafanya jambo zuri,makosa yanasameheka.ukimfukuza huwez jua utampata yup.ww mvumilie mbna ndo maisha,unasuluhsha then yanaisha,kama ni kufukuza utafukuza wangap?
 
the best ni kumsamehe.......
watu wakikosea na kujua makosa yao...
wanaweza badilika....

msamehe kwanza mpe...probation period...

Ukweli jibu sina, kaja mchana getini kampigia cm mdogo wangu, anamwambia niombee dada anisamehe nimetoka kanisani kuombewa nimeanguka, yani sasahivi natabia nzuri sana. Kanikuta ndani nimemuuliza vipi mbona uko hapa akadai hamna kitu, kaondoka kamwambia dogo ntarudi dada hasira zake zikiisha. Ukweli sielewi.
 
kama ni yatima mbna unafanya jambo zuri,makosa yanasameheka.ukimfukuza huwez jua utampata yup.ww mvumilie mbna ndo maisha,unasuluhsha then yanaisha,kama ni kufukuza utafukuza wangap?

Nikweli lakini.
 
kama ni yatima mbna unafanya jambo zuri,makosa yanasameheka.ukimfukuza huwez jua utampata yup.ww mvumilie mbna ndo maisha,unasuluhsha then yanaisha,kama ni kufukuza utafukuza wangap?

Nikweli lakini, kwani anadai mi nampenda sana dada na pia napenda kuishi nae sijui kwanini nimefanya hivi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom