Nimfanyeje mwanamke huyu?

Nimfanyeje mwanamke huyu?

GAMAH

Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
38
Reaction score
2
Mimi ni mtanzania mwenye jinsia ya kiume nina umri wa miaka 33, nina tatizo lina nipa shida katika maisha naomba ushauri wenu wana JF. nlipata msichana ambae alikua amezalishwa na mwanmme asiyekua na msimamo wa maisha na yeye msichana akiwa kaishia kidato cha nne na matokeo mabovu....tulipendana na na huyo mwanamke nikawa na matarajio ya kufunga nae ndoa japo alikua na mtoto, ili awe mke mwenye manufaa nikajitolea kumpeleka shule akachagua chuo cha wanyama pori ambacho ni bei mbaya na kinalipiwa kwa dola, kipato changu ni kidogo ila nikajitahidi kujibana kumuandikisha hapo chuo na kutokana na kutokidhi kiwango cha kujiunga na chuo akatakiwa kuanza na Foundation course ambayo nililipa zaid ya mil. 2 akajitahidi akafaulu na kujiunga na cheti mwaka 2008, kwa bahat nzuri baba yake mdogo akasaidia kuchangia ada hadi akamaliza cheti, mungu akasaidia akapatikana mfadhali wa kumsomesha toka marekani ambapo alimlipia ada ya Diploma aliyomaliza mwaka jana,na atamsomesha DIGRII.
katika kipindi hiko chote alinifanyia vitimbi vingi ambavyo nilivivumilia kiasi kikubwa, kwan alidiriki hadi kunisaliti lakini nilisamehe na kuvumilia kwani nilijua na kuwekeza kwake kua atakua mke wangu. mwaka huu amepata ajira serikalini ana mwezi wa 6 sasa cha ajabu amekua akinifanyia vitimbi vingi japo yupo mbali na mimi ila anavionyesha mfano mdogo ni kwenye sikukuu iliyopita amtoka kwenye kituo chake cha kazi na kwenda mjini kulewa akidai amelala chumba kimoja na rafiki yake wa kike na mumewe, kifadha hana msaada na huku anajua mim kwa sasa ni mwanafunzi chuoni.
WADAU NIFANYEJE?? NIMKWAMA MKE NATAKA ILA NDIO HUYO NMECHOKA JAMANI
 
FADHILA MFADHILI MBUZI UTAMNYWAAAAAAAA MCHUZIIIII BINADAMU WANA MAUZIIII!!!!!!!!!!!!

Pole mwaya tenda wema nenda zako. Na shukrani ya punda ni mateke. Umepoteza mda wa kutosha hapo, its about time you move on! Hana upendo na wewe huyo ila yuko na wewe coz imembidi tu!

Wewe usihesabu ulichopoteza hesabu utakacho okoa. Mtu hakuheshimu hajamuoa ukimuo si ndo atakupanda kichwani????

Well i dont know if i sound convisin but if you want it black n white ni kuwa Wewe ulikuwa daraja lake la kutoka kimaisha! Sasa keshatoka hakuhitaji! Na huyo mfazili wa marekani huyo sijui! Ada ya MWEKA si mchezo pale, Dolari lazima zisomeke.
 
Ukisikia kunguru ni kama huyo wako.Kazi kwako,ila hapo huna mke!
 
Ningepata mvumilivu kama ww, loh. piga chini huyo hakuna mjadala.
 
kha huyo dada noma...yaani kaendagegeddwa kwenye threesome...balaaa!!!

dah pole sana wangu ila huu ntindo wa wanaume kusomesha haungii akilini kusema kweli. imekula kwako hiyo mwana.
 
Chukua time zako baba fumba macho kwa uliyoinvest huko nyuma na uokoe mda uliobaki na shekeli zilizobaki vilevile

Huyo hana hata sifa za mke kwahiyo wala usimwite hilo jina la mke
 
Wapo Watanzania wenzangu wana Moyo,mi zamani sana shabwagasha na nmemsahau.


Mkuu Tafadhali chukua maneno yangu "Muache huyo hakufai tena,si sehemu ya furaha yako"

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mie nakupa pole ila nikupe akiba ya maneno!! unapojitoa kwa msichana iwe kumsomesha au kumnunulia gari usiiweke akilini kama ndio kigezo cha wewe kuja kumuoa!! kigezo kiwe mapenzi ya kweli na uaminifu!! hawa wenzetu japokua tunajitoa kuwapenda na kutumia jasho letu kuweka maisha yao sawa wao hawanaga love in return!!
 
Pole sana mkuu,Songa mbele ndo mpango mzima uliobaki,mwombe Mungu akutie nguvu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
what goes around comes around..
Achana naye,fanya maisha yako ila kuna siku atarudi,halafu .....'cry me a river bitçh'
 
Kila mara huwa nawashauri watu humu ndani kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya GF na mke.
Unapoamua kumjali GF siku zote usitegemee return, maana mtu huyo anaweza kuwa kitu chochote wakati wowote.
Mwanamke ni wako akiwa ndani kama mke(nayo siku hizi naona inapotea), akiwa GF huyo bado ni wa wengi.
 
Kuna rafiki yangu alisomeshwa chuo na mumewe (then akiwa bf). Lakini alimuambia i want to officially meet your dad. Dada akasema ngoja tuanze na kaka na dada mkubwa. Akawaambia nakuja na mgeni. Kaka wa watu baadabya kunch akawaropokea tu mimi nampenda sana huyu na nataka kumsomesha. Lakini nataka kummeet baba pia. Kaka akasema baba akijua unamsomesha atajisononekea kwa kushindwa kulea mwanae. Nyie endeleeni.
Ndoa ina miaka 10+. On a serious note shosti hakuwa anampenda mkaka. Lakini alijikuta anampenda na sasa anasema nikikuta mtubanamendea mume wangu nitaua.

Huwezi kujicommit hivyo gizani!
Kila mara huwa nawashauri watu humu ndani kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya GF na mke.
Unapoamua kumjali GF siku zote usitegemee return, maana mtu huyo anaweza kuwa kitu chochote wakati wowote.
Mwanamke ni wako akiwa ndani kama mke(nayo siku hizi naona inapotea), akiwa GF huyo bado ni wa wengi.
 
Wewe Mjinga, ila umepata fundisho.
Mwanamke anakujibu utumbo na bado unamlipia ada?

Siku nyingine usirudie, umesikia?

Halafu kasalitiwa halafu kasamehe_kisa atakuwa mke wake wa ndoa...duuuuh...kweli dunian watu tuko tofauti sana
 
Mimi ni mtanzania mwenye jinsia ya kiume nina umri wa miaka 33, nina tatizo lina nipa shida katika maisha naomba ushauri wenu wana JF.
Karibu sana. Ushauri utapewa.
nlipata msichana ambae alikua amezalishwa na mwanmme asiyekua na msimamo wa maisha na yeye msichana akiwa kaishia kidato cha nne na matokeo mabovu....tulipendana na na huyo mwanamke nikawa na matarajio ya kufunga nae ndoa japo alikua na mtoto,
ulifanya makosa kwa kuruhusu kumpenda binti wa aina kama hiyo.
ili awe mke mwenye manufaa nikajitolea kumpeleka shule akachagua chuo cha wanyama pori ambacho ni bei mbaya na kinalipiwa kwa dola, kipato changu ni kidogo ila nikajitahidi kujibana kumuandikisha hapo chuo na kutokana na kutokidhi kiwango cha kujiunga na chuo akatakiwa kuanza na Foundation course ambayo nililipa zaid ya mil. 2 akajitahidi akafaulu na kujiunga na cheti mwaka 2008, kwa bahat nzuri baba yake mdogo akasaidia kuchangia ada hadi akamaliza cheti, mungu akasaidia akapatikana mfadhali wa kumsomesha toka marekani ambapo alimlipia ada ya Diploma aliyomaliza mwaka jana,na atamsomesha DIGRII.
Wewe ni mjinga. Huwezi kumsomesha mwanamke kwa ada kubwa wakati mwenyewe una kipato kidogo.
katika kipindi hiko chote alinifanyia vitimbi vingi ambavyo nilivivumilia kiasi kikubwa, kwan alidiriki hadi kunisaliti lakini nilisamehe na kuvumilia kwani nilijua na kuwekeza kwake kua atakua mke wangu.
Haa! Waligegeda pochi manyoya na wewe ukavumilia? You are a strong man.
mwaka huu amepata ajira serikalini ana mwezi wa 6 sasa cha ajabu amekua akinifanyia vitimbi vingi japo yupo mbali na mimi ila anavionyesha mfano mdogo ni kwenye sikukuu iliyopita amtoka kwenye kituo chake cha kazi na kwenda mjini kulewa akidai amelala chumba kimoja na rafiki yake wa kike na mumewe, kifadha hana msaada na huku anajua mim kwa sasa ni mwanafunzi chuoni.
WADAU NIFANYEJE?? NIMKWAMA MKE NATAKA ILA NDIO HUYO NMECHOKA JAMANI

tafuta wa kuoa bwana acha wenzio wamgegede papuchi
 
Tenda wema nenda zako, baadhi ya watu husema, huyo dada nahisi hakukupenda ila sababu ulikuwa unampa msaada ndo maana alijisogeza kwako.
 
Kimsingi huyo si wako tena...achana nae...inawezekna unatumia nguvu nyingi ili aendelee kuwa wako...lakni ni dhahiri kuwa amekufanya wewe kama back up...anza kufiki upya sasa.
 
Back
Top Bottom