Nimfanye nini huyu dada jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimfanye nini huyu dada jamani?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Da Pretty, Jan 11, 2012.

 1. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hongereni kwa kuingia mwaka mpya.
  Nina jambo limetokea leo ambalo ni mfululizo wa mambo mengi yaliyokua yakitendeka siku zilizopita.
  Ni story ndefu ntajitahidi kuifupisha.
  Ninaishi kwenye nyumba ndogo na mdogoangu mwanafunzi na mtoto wa 4yrs ambaye ni mtoto mdogoangu mwingine na msichana wa kusaidia kazi ukizingatia nina huyu mtoto mdogo nami ni mfanyakazi.
  Leo nikiwa kazini nimepigiwa simu na tax driver wa pale jirani na kwetu kua msichana wangu ameonekana na begi anaondoka,na ameenda kuchukua tax pale ndio wakawa wanamuhoji maana kuna wanaomfahamu(mara nyingi nikiwa kazini kama kuna kinachotakiwa nyumbani nawaomba hao madereva wanifikishie hivyo humkuta yeye).
  Nikawaambia wamzuie,nikamtuma mdogoangu aende akaongee na huyo binti amuulize kwanini alitoroka badala ya kuaga?
  Binti akahojiwa,hakutoa jibu lolote,akasachiwa eti kabeba laptop,camera na perfume(nimeshangaa,nilitegemea atabeba nguo na labda simu!) akasemwa pale,akanyang'anywa alivyochukua nikawaambia wamruhusu aende maana nisingeweza kukaa nae tena,akaruhusiwa akaenda.
  Sasa jioni hii narudi nyumbani nikapita kwa wale madereva waliyoniambia yamenichosha!!
  Wanasema walipomuuliza anaenda wapi akasema kuna dada anafanya kazi salon kwangu,anaishi kinyerezi ndio waliongea kua aondoke atamsubiri tabata asubuhi ile (hajataja tbt ipi) ni kweli nina salon hapa jirani na ninapoishi na kuna mfanyakazi anaishi kinyerezi(naamini hawa madereva hawamfahamu) nae anatafuta housegirl.
  Nimeshindwa kuelewa namfanyaje huyu dada wa salon.
  Na siku za nyuma nilikua na binti ambae alikuja kwangu akiwa mjamzito nikampokea vizuri,
  haohao wafanyakazi wa salon kwangu (wa kinyerezi)wakaanza kumzonga na maneno akawa ananiambia hadi tumbo limekua ndio wakawa wanashangaa eti ana mimba nimuondoe atanitia mzigo(wakati nilijua mapema) binti kaenda kwao kujifungua,huyu kaja tar 30 Dec washamchukua.
  Hivi niwafanyeje hawa wafanyakazi wa salon kwangu??
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mfukuze kazi. . .
  Anaonekana kabisa hakupendi au labda anakuonea wivu, pengine hata hapo saluni anadokodokoa. Ili kuhakikisha kitu kama hicho hakitokei tena mwondoe hapo na uhakikishe anakaa mbali na msicchana wako atakaefuata.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Achana nao, wapuuzie. Ukianza kujiingiza kwenye ligi zao watakushughulisha na kukutia wazimu buree! Ukipata hgeli mwingine muonye juu ya hao wadada na umuambie umuhimu wa utu. People will come and go in ur life for a reason!
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Sana sana unachoweza kufanya ni 'kuwatania'. Waambie naskia nyie ndo mabingwa wa kuiba mahausigeli wa watu, then cut the story short na uwabadilishie topic. Watajionea aibu wenyewe.
   
 5. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Kafukuze
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mmhhhh lol.........
   
 7. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Yani huyu kilichonikera alitaka kuniliza pia!
  Nimepata hasira hadi najiuliza sijui niwapigie niwaseme,naamua kunyamaza maana nahisi ntakereka zaidi.. Au kesho nirudi mapema niwaseme au niwatimue nifunge salon nitafute wengine ila nawaza gharama nitakayoingia.
  Imenikera sana.
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  "ni lazima ifike mahali watanzania tukubali kufanya maamuzi magumu" - Edward Ngoyai Lowasa (Mb)... Tafakari, chukua hatua!
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  duh, siwezi kaa na adui karibu angu.
  Nikikuamini, watch my back, and will watch yours.
  Stab me!!? Out of my sight.

  Hapo kaanzia hausi gelo, kesho ataleta majambazi.
  Wivu hauna adabu wala mipaka.
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  maneno mazuri, tatizo reference

   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Hehehe! Some confrontations are not worth it! Maid ni liability, ukianza kucheza ligi daraja la 9 lazma upoteze mwelekeo!
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Dahhhh
  kitu nilichogundua dunia hii biashara na kuonea huruma mtu haviendani..
  hiyo biashara ni yako, ( hopeful unamlipa mshahara wake kama makubaliano yenu, na unamuheshimu)
  Vinginevyo ni akiba. wewe ndio mwene usemi wa mwisho ikija kwenye biashara yako. wafanyakazi wako
  wanatakiwa wakusikilize wewe, uwe mmbaya uwe mzuri maamuzi ya mwisho ni yako. Na kama umegundua
  mfanya kazi wako mmoja hana adabu au anafanya visivyo ongea nae mpe onyo akirudia tena mlipe mshahara
  wake wa mwisho achape lapa.. ( kazi zenyewe hizi za shida umemuajiri mtu hana heshima , ajiri mwingine ) ..
   
 13. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Uko sahihi,maamuzi magumu ni kama kumfuata mwizi wako na kumwambia ukweli,lakini zaidi shughlika na wafanyakazi wako wa ndani, waandae kisaikolojia kukutana na mishetani na mijizi itakayowashawishi vibaya hapo mjini na wape matunzo wasichana wako wa kazi hapo home na upendo hadi hata akishawishiwaje iwe ngumu kuondoka. House gal ni kama mlezi,invest in her,wapo wenye shukrani na uelewa! Pole dear!
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ukiwafukuza utapata wengine (wapo wadada wengi tu wanaohangaika kupata kazi), ukiwaacha next time wanaweza wakafanya kitu kikubwa zaidi.

  Unaweza ukaamua kukaa kimya wiki iishe bila kuwauliza chochote ila ukawa unatafuta wafanyakazi wengine, ukishapata unawatimua. Hamna haja ya kuwasema maana wenyewe wanajua walichokifanya.
   
 15. G

  G.JUMA Senior Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  naam Lizzy umebofonga ukweli coz kinachotakiwa ni kujipanga.
  Kwa sasa da perry hauna wafanya kazi wa kukusaidia, yupo kwa ajili ya kukuharibia hivyo usilaze damu mtimue coz huyo amekuchoka mpaka mwisho ukimuacha akipata nafasi ya kukuliza utasaga meno mwana JF Mwenzangu.
  Hiv da perry unamlipa kwa huduma anayokufanyia ya kukutoroshea ma house gel wako?
   
 16. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  kha! Tia chaka huyo demu. Nalog off
   
 17. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwann uumie na kukaa na kinyongo moyon,unatakiwa ulifanye hili gafla kabla hawajajipanga,kafunge salun hata mchana wa jua kali badilisha makufuli na vitasa walipe chao waambie unafunga kwa mda mpaka utakapowatafuta tena!bora utumie garama ili uishi kwa aman,rahic ni ghali kuliko ghali!
   
 18. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kumfata kumsema huyo dada sio jambo kubwa tena kwangu kwa sababu story ipo wazi kua alihusika.
  Na yule housgal ni mgeni mno isitoshe nilijitahidi kwenda nae vizuri kwa sababu namuachia nyumba na mtoto,sijui nini kilichomshawishi.
  Mbaya zaidi hadi kuiba vitu navyohisi kama vile alitumwa!!
   
 19. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kweli biashara na huruma ni tofauti.
  Nami sina huruma tena nao hasa walipokosa huruma kwa mtoto wangu.
  Mtoto alikua shule,kama ingekua sina taarifa,huyu mtoto angerudi toka shule angefanyaje? Na mlango hakufunga,yeyote angeingia.
   
 20. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  beki tatu ni pasua kichwa hasa kama ni wa kutoka ile mikoa wazoefu...kaa nae kwa tahadhari zote na tegemea retirement notice any tym
   
Loading...