Nimezipenda solution za January Makamba kiukweli

Huyu Januari Makamba si mtu wa kuaminika. Uzalendo wake na credibility yake inatia mashaka kwani ni puppet wa Rostam Aziz na Edward Lowassa (DOWANS syndicate). Ni mtu hovyo huyu.
 
Well said. Inaonekana huyu jamaa kapelekwa pale kwa kazi moja tuu, kulinda maslahi ya RA kwenye umeme na madini. Toka achaguliwe yeye na DOWANS! DOWANS mpaka amejisahau anaongea kama vile ndio serikali.

Tumemshtukia.
 
Hmmmmmm! solution indeed?

Kuamuru kuwashwa mitambo ya dowans. Hivi hikamati ina maslahi yanani
Wamesahau swala la dowams lipo mahakamani? Na chaajabu Raisi aliwaamuru tanesco watafute mitambo
Ya kukodi . Sas tufutelipi lamakamba ama laraisi na je makamba hajui swala
Lakuingia mkataba na dowans nikinyume na sheria? Minafikiri kamati inge shauri na si
Kuamuru , kama wana amuru kuna maslai binafsi
 
Kama ni rais wa kutangaza sijui,kama ni makamba mi sijui.
(shairi lako nimelikubali)
 

Mkeshaji, swali lako murua sana sina uhakika kama limejibiwa kama bado angalia kanuni za kudumu za bunge 2007 zinavyosema:

9.-(1) Majukumu ya Kamati ya Kudumu ya sekta yatakuwa
yafuatayo:
-
(a) kushughulikia bajeti ya Wizara inazozisimamia;

(b) kushughulikia Miswada ya Sheria na Mikataba inayopendekezwa kuridhiwa na Bunge iliyo chini ya Wizara inazozisimamia;

(c) kushughulikia Taarifa za kila mwaka za utendaji za Wizara hizo;

(d) kufuatilia utekelezaji unaofanywa na Wizara hizo kwa mujibu wa Ibara ya 65(3) (b) (sic)ya Katiba.

Ibara ya 63 (3) (b) ya katiba inasema:

(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza–

(a) kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;

(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;

Kwa kweli Januari inaelekea hajui mipaka ya kamati yake kisheria na kikatiba, Bodi ya Tanesco ni legelege na usiyojua madaraka yake kama sheria ya kuanzisha tanesco inavyosema na menejimenti ni dhaifu mnio kwa kuburuzwa hovyohovyo tu. Si ajabu wanaogopa kuwa wakikataa watafukuzwa kazi.

Mimi naona huu ndio wakati muafaka wa kufukuza bodi na menejimenti ya Tanesco kwa kushindwa kufanya kazi na badala yake kazi zao kufanywa na mamluki Januari.
 
Matatizo yote yanaikumba TANESCO yanasababsishwa na shirika hilo kuingiliwa kiutendaji. Sasa Management inaona ni vyema kiuzia migodi umeme kwa sababu inapata pesa kamili za 125 MW tofauti na huku viwandani ambako mita zote zimechezewa ili kuonyesha umeme unaotumika ni kidogo kuliko unoingia, hivyo shirika kupata mapato kiduchu.

Mtakumbuka ile issue ya TANESCO na kiwanda cha Cement Tanga ambapo Dr Rashid alitaka kujiuzulu kama kiwanda hicho kitarejeshewa umeme kwa maagizo kutoka ngazi za juu baada ya kukamatwa wakiiba umeme.

Hivyo kitendo cha Kamati ya Januari Makamba kuifundisha management na apte umeme na nani aispate hakikubaliki hata kidogo na kitadhooifisha mapato ya shirika hilo. Naomba management ya TANESCO iachiwe iuze umeme wake kule wanapopaata mapato.
 
Migodi ndo wanaingizia TANESCO mapato makubwa kuliko makampuni mengine na sitashangaa kusikia kwamba wana mikataba inayowalinda wasikatiwe umeme.

Fumbo mfumbi mjinga mwelevu ataling'amua
 
Mimi huwa najiuliza sana kuhusu Tanesco. Kwa uelewa wangu, tanesco inapaswa kujiendesha (self sustainable) kama mradi kwa sababu huo umeme wanaozalisha tunaulipia. Pamoja na madeni wanayodai kwa wateja lakini bado wana nafasi ya kujiendesha kabisa. Iwapo wanhitaji kujipanua nadhani wanatakiwa kutafuta vyanzo vya finances kama miradi mingine inavyofanya. Kwa hali ninavyoiona ni kwamba huu mradi haulipi na ndiyo maana hauishi migogoro na matatizo tunayoyaona. Hivi inawezekana vipi tangu enzi hizo wameshindwa kutosheleza mahitaji ya umeme kwa walau 50%? Yaani haiingii akilini kabisa. Pamoja na kwamba hii ni "public good" lakini haikupaswa kuwa kama ilivyo sasa.
Mie wanachonishangaza hawa watu wa tanesco ni kuendelea kutumia "traditional and conversional" sources ya nishati ya umeme (maji na mafuta). Matumizi ya gesi bado hayaonyeshi tija japo kuna njia zingine kama zile za kutumia upepo. Nashindwa kabisa kuelewa hivi huyo CEO na mainjinia kibao huwa wanafanya nini huko tanesco?
Kwa kweli inachosha na kukera sana
 
sadly jamaa ana brag mtaani kwamba mitambo ya dowans inawashwa j3 na hamna kitu cha kufanya, anasema umeme utawaka siku nzima. hii inanishangaza kwa ajili dowans ni 100mw na wakati upungufu ni more than 500mw
 

Another bogus politicians at work, hawa wanatuletea upupu tu hapa, tumechoshwa na hawa vilaza wa kufikiri.
 

Nimeikubali analysis yako. I like thinkers like you!
 
kuna watu kibao wana iba umeme na wafanya kazi wanajua lakini kwa kuwa hii nchi imekaa kifisadi fisadi tu ndiyo maana wasoma mita hupewa 2000 kwa mwezi wana kaa kimya, nijukumu lao Management ya Tanesco kujipanga na kuzibiti hali hiyo na wakiamua hawashindwi....kwenye nyekundu sikubaliani na wewe kabisa hawawezi kuashiwa wafanye watakalo wakati wananchi wanaumia, kamaleo TANESCO ukiwaruhusu wafanye huu ujinga kesho kuna shirika lingine litafanyi hivyo hivyi kama tunavyoona kwenye bidhaa kila mfanya biashara akijisikia kupandisha beianafanya hivyo matokeo yake tuna yao...gas, mafuta nk
 
namkubali january makamba, I wish yeye ndiyo angekuwa waziri na ngeleja angebaki mbunge.

Makamba Januari hana lolote analojua KUHUSU UMEME. He is just a politician. Huyu amekuwa planted na JK,RA na EL.
Anachoongea hapa ni siasa tu,hakutakuwa na solution yoyote hapo. Hivi you people mnafikiri Tanesco Engineers wanaweza kuwa hawajui kuwa kwenye hiyo migodi unaenda umeme Megawati ngapi na wazigawanye vipi???Mpaka Januari Makamba ndo aje kuwafundisha kazi TANESCO wakati hajui hata Calculation moja ya namna ya kupata hiyo MW 1?????

Inachekesha kweli kweli. Mimi nilishasema several times kwenye JF kuwa TATIZO KUBWA TULILO NALO WATANZANIA HIZI NYAZIFA ZA UWAZIRI HAWAPEWI PROFESSIONALS! Ilitakiwa Waziri wa NIshati na Madini awe Engineer aliyebobea kwenye UMEME, a doctor or Professor in that field. Ngeleja alikuwa MWANASHERIA wa Vodacom kabla hajaingia kwenye siasa!!!What do you expect from him???

Januri Makamba ni mhitumi wa shahada ya KUSULUHISHA MIGOGORO YA WAKIMBIZI. Halafu watu wanategemea atoe ufumbuzi wa tatizo la umeme. Never,he won't. He is as bogus as anybody in CCM.
 
Well said. Inaonekana huyu jamaa kapelekwa pale kwa kazi moja tuu, kulinda maslahi ya RA kwenye umeme na madini. Toka achaguliwe yeye na DOWANS! DOWANS mpaka amejisahau anaongea kama vile ndio serikali.

Tumemshtukia.

Mbona hajaongelea uwiano wa ukusanyaji kodi migodini kwenye Corporate tax na PAYE tax.January hana uwezo wa kuongelea vitu technical ambavyo ni beneficial kwa nchi.Ni bingwa wa kuongelea vitu vya kitapeli/ kisanii zaidi kama DOWANS.


Makamba hajui kwamba kuna watanganyika wamehamishwa maeneo ya machimbo na hadi leo hawajalipwa?

Je hajui kwamba kuna ajenda imelala ya wawekezaji huko Mara kutiririsha maji yenye sumu mto mara NA WATANGANYIKA HAWAJAFIDIWA????

hUYU mAKAMBA KWANZA NCHI HAIJUI hajui matatizo yanayowakabili watanganyika leo nakuja na hoja nyepesi ya DOWANS, hoja mabayo majibu yake yako kwenye riport ya Mwakyembe.Huyu anatusanii anakula posho bure tu

Amekuja na mradi wa posho za vikao vya kamati yake.Watanganyika kama hamjui huyu kabuni mradi, ina maana kila wakati wankutana na wanlipana posho.Nina uhakika hadi mwisho wa mwaka kamati ya NISHATI NA MADINI itakuwa imetumia peasa nyingi za walipa kodi kutokana na vikao kwa kisingizio cha DHARURA PROJECT
Mdogo wangu MNYIKA zinduka bomu hilo litawalipukia la posho


 

Sidhani kama TANESCO wana uhuru wa kuamua chochote kuhusu mustakabali wa shirika kimkakati wala kibiashara. Maamuzi yote yako kwa vigogo walioko CCM-CC. Hakuna shirika la umeme la taifa hapo; wao wameamua ni sehemu ya ulaji na ufujaji tu - hata serikali nayo haioni taabu kutolipa deni la TANESCO labda kama kuna maslahi binafsi (Net Group Solution). Kuna wanaopendekeza TANESCO ivunjwe na kuundwa upya. Jawabu ni kuivunja CCM kwanza (na kuiunda upya kwa wanaotaka idumu) ndipo tuweze kushughulikia sekta ya umeme inavyostahili. Wao wanasema "kujivua gamba" lakini sina imani kama wanaweza kuendesha "mapinduzi ya kweli" kuondoa tabaka la mafia linalokinyonga chama na uchumi wa taifa taratiib na kwa uhakika zaidi.
 
Mara nyingi huwa najiuliza hivi kweli sisi Watanzania tuna akili ama tunatumia zaidi hisia kama wanyama. Ikiwa leo tumeshindwa kuendesha shirika la reli mbovu toka mjarumani yenye gharama ndogo kabisa ktk kufanyia ukarabati tutaweza kweli kuendesha reli ya kasi inayotumia umeme?..Na kama tunashindwa kuzalisha umeme wetu wenye uwezo wa mega 3,000 tukizalisha asilimia 15 tu kwa sababu tumeshindwa kukarabati hizo dams (cheapest of them all) Je, tutaweza kukarabati haya malengo mengine ambayo tunayapanga!

Kwa fikra hizi za kina Makamba ndio maana JK kasema Nyerere kaiacha nchi maskini kwa maana kwamba utajiri wa nchi ni fedha zilizoko benki sio rasilimali na maliaasili zake... Ama kweli naogopa kusomea uchumi chuo kikuuu UDSM.

Haya ebu turudi nyuma kuifikiria hiyo Dowans, ni kiwango gani cha umeme wa dharura tunaouhitaji leo, sii chgini ya mega 200 hao Dowans wanaweza kuzalisha mega 35 hadi 100 kama wataongezea mitambo mingine... sasa kuna ulazima gani wa kuwasha hii mitambo yenye utata mkubwa ya ufisadi halitukijua fika kwamba shida ya umeme haitakwisha na mgao lazima uendelee..

Jamani, jamani tukumbuke kwamba Dowans ni kampuni hewa ambayo wameiunda haoa hao viongozi baada ya kula fedha za wafadhili wakijua wamepiga bao..Hawana pa kuipeleka na ndio maana bado imefungwa wakitafuta njia.. Sasa mimi nasema hivi kama wao ni waungwana na maadam mitambo imeshaletwa nchini na hawawezi kuitupa baharini waiwashe pasipo kumlipa mtu kwani hakuna wa kumlipa. generator hiyo tumepewa buree msaada baada ya baadhi viongozi wetu kwenda Houston na kulia na manispaa ya jiji hilo..

Nawaomba sana wakazi wa Marekani na hasa Houston, fuatilieni kwa ukaribu hizi generator zimenunuliwa wapi na kwa kiasi gani hata mtaupata ukweli wanaojaribu kuuficha...Bomba la gas kwenda Mwanza nilisema nani atapewa?...Haya nambieni leo hii ni nani CEO wa shirika linalopewa jukumu la mradi huo..

Niliwahi kusema Bush baba kanunua Kigamboni na anataka kuwekeza watu wakabisha sana, wakaja na gear za udini na chuki kwa sababu ambazo mimi sizielewi, sasa nadhani mnayakubali maneno yangu. Hivyo tafuteni kwa undani hilo shirika linalotaka kuwekeza Kigamboni mji mpya na tafuteni wenye hisa kubwa kisha turudi hapa tuzungumze zaidi...Na bado, Kiwila pia kuna mpya ambayo kauziwa mhndi ambaye katafuta mwekezaji kuficha uchafu uliotokea.. Haya yote hamyaoni na kuyachoka jamani?
 
Naungana na wewe Niweze. naamini kuna mapendekezo mengi ambao wataalamu binafsi(enegy consultants wa nje na wa ndani) walishafanya utafiti na kupendekeza short, medium amd long plan solution kwa tatizo letu hili la umeme. Tatizo liliopo ni utekelezaji na uvivu wa kuamua wa serikali yetu iliyopo madarakani.
Mara zote vipaumbele vyetu ni vya zima moto na kwa maslahi ya Ki CCM zaidi na hasa matumbo yya wakubwa wenye ulafi usiokuwa ma maana.
Mikataba mingi iliingiwa ili kujustfy tatizo na kutoa mianya ya kupata ulaji. hapo ndipo kwenye Tatizo? Taifa Makini haliwezi kuniambia kuwa Kamati ya siku 12 ya January[ sipendi kumwita makamba kwani napata kichefuchefu kwa jina hilo) tena isiyokuwa na wataalamu kwamba imekuja na mapendekezo ya solution ya umeme Tanzania.
Kweli kwenye vipofu hata mwenye makengeza anakuwa mtawala!!!!

Sasa tupo kwenye lindi lililotakana na kudharau Taaluma kwa muda mrefu na Tuna mgao ! zaidi tunaongozwa na serikali ile ile isioona. Nafikiri dawa sio kususia mtindo walioutumia kupata ulaji ili nasi tupone kidogo! Bora Nusu Shari kuliko Shari kamili! . Twende nao kama wanavyotaka ili Umeme kidogo urudi kwenye mtandao.hii itasaidia uchumi usiporomoke zaidi na kunusuru asilimia karibu 4 ya watanzania ambao kipato chao kwa namna moja ama nyingine kinategemea kuwepo kwa umeme.

Tusipokubali hilo basi tusisubiri watu hawa wakae mpaka miaka mitano iishe maana hali itakuwa mbaya zaidi. Tuwangoe sasa na tuweke watu makini watakaoeshimu utaalamu.
Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…