Nimezama kwa Bar Maid

Nimezama kwa Bar Maid

Pale mwishoni mkuu nimeeleza kuwa mazingira niliyokutana nae pamoja na mazingira ya kazi ndio vyanipa wasiwasi mkuu. Ushauri wako nimeuelewa sana mkuu. Thanks

Usife moyo Mangi. Huyo huyo ungeweza kutana naye katika sehemu za ibada pia, angalau kwa style mliyokutana unajua fika unajihusisha na mtu wa aina gani. All the best.
 
Wewe oa, ni wachache sana wanaokuwa wawazi hivyo, anaweza akawa msomi wa masters lakini ndio ikawa mateso kwako Na kukupunguzia siku za kuishi, cha muhimu ni amani ya moyo, ondoa neno Bar maid, ita mke
 
Shida za dunia hii wakati mwingine hupelekea watu kufanya kazi ambazo hata hupunguza heshima ya utu wao! Usimuhukumu huyo au mwingine yeyote kwa kigezo cha mazingira ! Utu na tabia yake vishike hatamu katika tafakuri yako na baadae maamuzi!
Upo sahihi kabisa
 
Bar maid ni mtu na ni mwanamke kama wanawake wengine.Huwezi jua nini kilimpelekea kufanya kazi bar.Kama umemuona anastahili muoe tu na utaenjoy kama wanaume wengine.Hivi ndoa zinazovujika kwa sababu tofauti wanawake walikuwa wauza bar? Huyo anahitaji kuolewa kama wengine.Na ni mwaminifu kama ulivyoeleza.Ukimpoteza utaumia baadae.Halafu marufuku kuwaambia nduguzo kuwa alikuwa anauza baa.Mtafutie kazi au biashara ndo muanze mchakato wa ndoa.Binafsi nimebariki.Unipe kadi nitachanga
 
Una hatari sana aisee naonea huruma familia yako.

Thamani yako na vitu unavyo fanya ni tofauti.
 
Bar maid ni mtu na ni mwanamke kama wanawake wengine.Huwezi jua nini kilimpelekea kufanya kazi bar.Kama umemuona anastahili muoe tu na utaenjoy kama wanaume wengine.Hivi ndoa zinazovujika kwa sababu tofauti wanawake walikuwa wauza bar? Huyo anahitaji kuolewa kama wengine.Na ni mwaminifu kama ulivyoeleza.Ukimpoteza utaumia baadae.Halafu marufuku kuwaambia nduguzo kuwa alikuwa anauza baa.Mtafutie kazi au biashara ndo muanze mchakato wa ndoa.Binafsi nimebariki.Unipe kadi nitachanga
Hahahahah nmeipenda hiiinmkuuu.

Atupe kadi ,,,tuhududhurie ,tule ,tucheze ,,tunywe.
 
Muwe wapenzi for atleast 4 years.

Mpe mtaji afanye biashra nyingine, aachane na hiyo kazi ya sasa.

Naamini wapenzi wanakutana popote pale.

Mke wangu tulikutana kwenye bus la Kilimanjaro, alikuwa anagawa maji, i will never regret.
 
Jitwishe huo mzigo unakufaa, ukichelewa nitamfuatilia ili na mimi nipate burudani yake ikiwezekani naweka mzigo kichwani.
 
Kama yuko hivyo usemavyo alikubalije kwenda kulala na wewe na akakudai hela siku ya kwanza kukutana nae? Au ndo kabadilika baada ya kuwa na wewe?
 
Back
Top Bottom