Nimezaa nae lakini namuogopa! niko njiapanda

chamng'asi

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
211
385
Nilianza nae vzr miezi kadhaa akapata ujauzito akiwa chuoni. Akazaa kuendelea na chuo na sasa ameshahitimu na mtoto ana miaka minne.

Nilitarajia akimaliza chuo nifanye taratibu za kuishi nae tulee mtoto wetu na ikibidi tuongeze.
Shida nikaanza kuiona nilipokuwa karibu nae baada ya kurudi masomoni.

1. Ana wivu wa kukera anacontrol simu zangu yani sina privacy tena
2. Ni mkorofi, mkali, mbishi hakubali kushindwa
3. Hana huruma na mimi hataki kusikia neno sina pesa... Mtagombana
4. Hapendi maisha magumu anapenda raha muda wote
5. Ni mvivu anapenda kulala na kuchezea simu
6. Ni mchafu kuanzia yeye mpaka nyumba hii inanikera sana
7. Hana upendo kwa ndugu na rafiki zangu
8. Anavaa na kukaa ovyo mbele ya mtoto na ukizingatia ni mtoto wa kiume

Sijalipa chochote kwao japo wananijua na Ukweli sina Amani na yeye hata kdg.... NAMUOGOPA.
Natamani kumlea mtoto wangu kwa namna ninayoitaka lakini sijui la kufanya niko njiapanda.....
Semeni neno ili nijue mustakabali wa maisha yangu na mtoto wangu maana keshanivuruga akili, mwili na roho....!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana ndugu,

Hapo cha maana angalia namna gani unaweza kumhudumia mtoto wako kwani huyo mwanamke atakusumbua sana ukiishi naye.

Tena shukuru ameonyesha makucha yake mapema kabla haujamuoa.Ungejuta!
 
...Mkuu, Kasoro zote hizo hukuziona wakati mkipeana Mimba?
Anyway, japo chomoa tu Mkuu. Huna haya ya kutafuta Ushauri JF.
Hakufai. Hizo Tania amekua Nazi huko kwako unadhani ukimua utaweza kumfundisha chochote ili abadilike?
Huwezi. Hakufai...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Mkuu, Kasoro zote hizo hukuziona wakati mkipeana Mimba?
Anyway, japo chomoa tu Mkuu. Huna haya ya kutafuta Ushauri JF.
Hakufai. Hizo Tania amekua Nazi huko kwako unadhani ukimua utaweza kumfundisha chochote ili abadilike?
Huwezi. Hakufai...

Sent using Jamii Forums mobile app
Na mimi nimejiuliza swali kama la kwako mkuu, ina maana huyo mwanamke hana zuri hata moja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom