Nimeyasikia haya... Je inawezekanaje?

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
Niko kwenye kijimgahawa napata supu, meza ya pembeni kuna mama wa makamo yupo na mbaba mwingine nao wamekaa wanakunywa soda. Yule mama machozi yanamtiririka ikabidi nitege sikio japo niambulie mawili matatu ya kunijuza chanzo cha kilio chake.

Kwa niliyoyaskia niliweza kugundua kuwa mama ana kijana wake ambaye according to yeye amebambikwa kesi ya kumbaka mwanafunzi mwenzie, mama anadai huyo msichana alikuwa ni girl friend wa kijana wake na baba wa msichana amem frame up kumkomesha tu. Baba wa msichana ameshafungua kesi na anadai apewe laki tatu ili afute kesi. Yule mbaba aliyekaa nae pale nagundua kuwa ni mganga wa kienyeji na kwa kujiamini kabisa anamuambia mama "Usiwe na wasiwasi dada, nitafutie tu elfu arobaini tupoteze faili"

Toka siku hiyo najiuliza hivi inawezekanaje kwa hawa jamaa kupoteza mafaili? Hebu nijuzeni inakuwaje watu mlio na experience na haya mambo.
 
kama imewezekana ku mfrem huyo mtoto wa kiume na kumsingizia kubaka, Basi kupoteza faili ni ize kabisa.
 
:nono:Men....ingekuwa ni rahisi kupoteza files za kesi mbona kusingekuwa na mtu anafungwa. Watu na hela zao wanaenda kunyea ndoo sembuse huyo. ingekuwa nafuu kama angemuambia ngoja nimbadilishe mawazo(Kumpumbaza) baba wa binti akafute kesi. ila hii ya kupoteza file...hapana. tena file ndo litawekwa juu kabisa na liwe linaangaliwa mara kwa mara. Mzizi Mkavu hii inaizungumziaje mtaalam wetu wa tiba mbadala
Niko kwenye kijimgahawa napata supu, meza ya pembeni kuna mama wa makamo yupo na mbaba mwingine nao wamekaa wanakunywa soda. Yule mama machozi yanamtiririka ikabidi nitege sikio japo niambulie mawili matatu ya kunijuza chanzo cha kilio chake.

Kwa niliyoyaskia niliweza kugundua kuwa mama ana kijana wake ambaye according to yeye amebambikwa kesi ya kumbaka mwanafunzi mwenzie, mama anadai huyo msichana alikuwa ni girl friend wa kijana wake na baba wa msichana amem frame up kumkomesha tu. Baba wa msichana ameshafungua kesi na anadai apewe laki tatu ili afute kesi. Yule mbaba aliyekaa nae pale nagundua kuwa ni mganga wa kienyeji na kwa kujiamini kabisa anamuambia mama "Usiwe na wasiwasi dada, nitafutie tu elfu arobaini tupoteze faili"

Toka siku hiyo najiuliza hivi inawezekanaje kwa hawa jamaa kupoteza mafaili? Hebu nijuzeni inakuwaje watu mlio na experience na haya mambo.
 
Last edited by a moderator:
Kwa nn usingemfuata huyo mbaba umuulize inawezekanaje? Na kuonekakana uko serious ungempa na ww ishu ya uongo na kweli uone inakuaje?
 
Mimi ninahisi huyo jamaa hakuwa mganga, mleta mada ulijiridhisha vipi kuwa yule ni mganga? I have a second thought huyo jamaa atakuwa ni mtunza kumbukumbu wa majalada ya mahakama....hayo mara nyingi huwa yanapotea sana...mbona kontena bandarini zinapotea ndio sembuse mafaili?
 
Niliuliza wenyeji ndo wakanambia yule jamaa ni mganga wa kienyeji maarufu sana. Ila nakumbuka pia kuna story niliiskia miaka ya tisini, m'bongo mmoja alikamatwa na unga, i think ilikua Australia, ikapigwa kazi ile coke ikageuka kuwa unga wa chakula!
 
Ndio maana twaambiwa ukiwa shule usijihusishe na mapenzi badala ya kula buku ili ulofa uuage watoto wadogo waendekeza ngono tena hata wazazi wanafahamu,na hao wazazi badala ya kukemea hiyo tabia wao wanachekelea,huyo mama waache alie aliyataka,hata soni hana,je hicho kidume cha mbengu kingekuwa ndio kina mnaniiibinti yake angekaa kimya?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom