Nusratt
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 1,707
- 4,192
Muda huu nimejikuta ghafla namkumbuka marehemu mama yangu, Mama mapacha Nusratt na Nasra.
Tulizaliwa mapacha na mimi nikiwa Dotto.
Kwa bahati mbaya nasikia mama alipata ajali akiwa na Kulwa (Nasra) wakati wakitoka hospitali ambako Kulwa alikuwa anaugua mafua na homa.
Mama na pacha wangu walisukumwa na gari dogo, Nasra alifia palepale eneo la ajali na mama alifia hospitali masaa machache baada ya kufikishwa hospitali.
Naambiwa nilikuwa na miezi 5 tu.
Baada ya maziko, baba yangu alinipeleka kwa bibi mzaa mama na hakuwahi kurudi tena mpaka leo hii.
Nimekua mkubwa sasa bila kuijua sura halisi ya mama yangu, pacha wangu Nasra wala sura ya baba yangu, zaidi ya kuwaona kwenye picha.
Huenda Nasra asingeugua siku ile, basi tungekuwa tuko familia kamili yaani sisi watoto, baba na mama yetu.
Niliendelea kukua nikijua bibi yangu ndie mama yangu mzazi mpaka pale siku moja aliponiambia ukweli kuhusu mimi, pacha wangu na wazazi wangu.
Nililia sana japo haikubadilisha uhalisia.
Bibi alinilea na kunisomesha kwa juhudi zote.
Aliuza mazao ili niende shule na hatimaye chuo.
Nilifanikiwa kiasi kupata elimu na kujiajiri.
Ila kabla bibi yangu hajafaidi matunda yangu vizuri, Mungu nae akamchukua bibi yangu.
Nimejikuta nakumbuka nilikotoka, nilipokuwa na hapa nilipo.
Mungu aendelee kumrehemu mama yangu, bibi yangu na pacha wangu. Hao ndio ndugu zangu kwani sikuwahi kumjua ndugu yangu yeyote yule.
Baba yangu alinitelekeza hivyo wala sitaki kujua kuhusu yeye.
Nimejikuta nawakumbuka sana.
View: https://youtu.be/cVb7QxyiuR4?si=eoSwWTiW4vt4z_K3