gwamaka aswile
Senior Member
- Mar 26, 2015
- 186
- 106
Tuachane na itikadi za kivyama, tuachane na ushabiki wa kisiasa nikimuangalia john pombe magufuli anavyoongea kila mahali anapopitwa kutambulishwa naamini kabisa tanzania imempata mtu sahihi wa kuivusha katika kipindi hiki kigumu cha kiuchumi na kisiasa. Ukweli mimi huwa naamini zaidi katika personality kuliko uvyama katika wanasiasa wa upinzani kwa wote kwa ujumla nikiwaangalia namuona dkt. Slaa ni mtu mwenye dhamira ya kweli kabisa kabisa so is magufuli ujue hawa jamaa ni watu ambao wako sirius sana. Nimempenda zaidi magufuli pale anaposema nikiwa rais nitakuwa rais wa watanzania wote si upinzani si ccm na nitawatumikia kwa moyo wangu wote. Sijayapenda zaidi maneno, la hasha bali nimependa namna anavyoyaongea ukweli ni kuwa hata ukimuangalia unaona kabisa kuwa huyu mtu ni mstaarabu. Japo kuna watu wanamkosoa kwa vitu vidogo vidogo lakini naamini kabisa magufuli atashauriwa kwenye vitu vidogo na atakuwa bonge la rais. Bila kusahau amweke muhongo kwenye nishati na filikunjombe apewe tamisemi awakomeshe wakurugenzi wezi ili maendeleo yaonekane fasta