Nimefurahi sana leo kumuona huyu jamaa akiwa katika hali hii

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
4,134
5,243
Asalam alaykum

Leo ni siku ya Ijumaa nawatakia siku njema wana JF wote humu ndani.

Jambo kubwa lililo nifurahisha sana katika nafsi yangu ni kumuona huyu mwamba saigon saleh a.k.a Saigon akiwa katika hali ya utulivu kabisa na unyenyekevu wa hali ya juu sana,ndani ya msikiti ninao swalia swala za kila siku na za siku kama ya leo aljumaa.

Saigon alikuwa katika muonekano wa kistaarabu kabisa wa mavazi ya kanzu nyeupe na kilemba cha rangi zenye mchanganyiko wa nyeupe na nyekundu...hakika nilipata furaha sana ndani ya nafsi yangu..kumuona kijana huyu aliyekuwa kinara wa hiphop wa kundi la Diplomatz waliokuwa miongoni mwa waanzilishi wa hiphop na bongo fleva hapa nchini pia mtangzaji wa zamani wa eatv wa kipindi cha hiphop base.

Mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wafatiliaji wa kubwa wa hiphop hapa bongo na nje ya nchi,hivyo saigoni alikuwa ni miongoni mwa watu niliokuwa na wafatilia sana kabla ya kuachana na hayo mambo....kwa sasa si mshabiki sana kama zamani.

Kilichonifanya niandike hapa ni uwezo wa Mungu mtukufu kunikutanisha na mtu niliyekuwa namkubali sana ndani ya nyumba ya ibada tena baada ya swala ya ijumaa, tena huku nyumbani kwetu ujiji kigoma mwisho wa reli aisee nimefurahi sana,Saigon alikuwa mnyenyekevu sana katika maongezi yake kiasi kwamba unaona imani imejaa katika moyo wake kwa sasa..japo kuwa kuna watu walisema amepoteza network mara dishi limeyumba....naweza kusema jamaa yuko timamu kabisa sema kwa sasa ameamua kumtumikia mola wake mtukufu hivyo tuache kumchafua.

Nadhani katika watu waliokuwepo pale msikitini hakuna aliyeweza kumfahamu kama alikuwa mtu maarufu kwenye fani ya hiphop....walijua ni sheikh wa kawaida,nilipata wasaa wa kumsalimia akaitikia kwa adabu sana....alikaa chini na kuwapa nasaha wanafunzi wanaosoma katika msikiti huu wa markazi hapa ujiji...kisha akaletewa mizigo yake mabegi na vitu vingine akapanda pikipiki akawa ameondoka bwana saigon ndani ya mji mtukufu wa ujiji....saigon ni mzima wa akili na anajitambua kabisa sikuweza kupiga nae picha simu yangu ilikuwa chaji.
Allah amuongoze saigon na watu wote duniani.
 
InshaAllah tumuombee kheri kijana mwenzetu na tumuombe mwenyezi Mungu amfanyie wepesi kwenye maisha yake ya kila siku na sisi InshaAllah tumuombe mwenyezi Mungu atujalie kheri na kutuweka kwenye njia sahihi....

Nasikia pia Hashim Dogo kutoka kikosi naye kwasasa ni ustaadhi ule usela wake wa block 41 kauacha na iwe kheri pia kama naye yuko kwenye njia hiyo...bila shaka na Kala Pina naye atajifunza kutoka kwa masela wake...
 
InshaAllah tumuombee kheri kijana mwenzetu na tumuombe mwenyezi Mungu amfanyie wepesi kwenye maisha yake ya kila siku na sisi InshaAllah tumuombe mwenyezi Mungu atujalie kheri na kutuweka kwenye njia sahihi....

Nasikia pia Hashim Dogo kutoka kikosi naye kwasasa ni ustaadhi ule usela wake wa block 41 kauacha na iwe kheri pia kama naye yuko kwenye njia hiyo...bila shaka na Kala Pina naye atajifunza kutoka kwa masela wake...
Amiin amiin shekh wangu...hakika leo nimefurahi sana...jamaa katulia anamuonekano wa kistaarabu sana hakika ukifuata maamrisho ya Muumba huwezikupotea kabisa....jamaa walikuja katika makundi ya tabligh leo ndio waliokiwa wanaondoka huku kigoma.

Allah awaongoze na sisi pia tuwe mfano wa kuigwa katika jamii yetu.
 
hapa mtaani kwetu Mabibo jirani na Madrassat chidi boy kuna mama anaitwa mama saigon huwa anatuizia aana vitafunwa vya chai


Huyu bwana Saigon ana ngoma moja inakwenda kwa jina la Poverty ni nzuri sana
Jamaa alikuwa mkali sana...kwenye flow za hiphpop rap....huwezi amini kama ndio yeye kwa sasa kabadilika kawa mpole mnyenyekevu.
Mama mmempa jina kwa ajili ya saigon au kwa ajili ya hiyo huo wimbo wa poverty?
 
Saigon Allah kashamuonyesha nuru ila hv karibuni alikuw morogoro akiwa mtangazaji wa tv iman naona atakuwa anajishghlisha na mambo mengine,ila amekuw mwema sana sshv Allah atuongoze sote ...aamin
Kweli kabisa, jamaa ametulia kabisa unaiona nuru ya wema usoni mwake...kama unaimani kidogo unaweza dondosha chozi.
 
Back
Top Bottom