Nimetokea kumpenda mke wa rafiki yangu

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,778
Just kumpenda tu upendo wa kawaida, msije kunihukumu eti labda hivi wala vile. Nampenda tu kama ninavyowapenda watu wengine

Nimempendea upole, ana matamshi safi yasiyo na upuuzi, mrembo, anajua kujisafisha na kujipamba, mavazi anayovalia yanampendeza, si mwongeaji kiviile japo ana sura ya ucheshi, hana makuu na mtu, muda wa utani kwake ni wa utani, na muda wa kazi kwake ni wa kazi.

Popote ulipo shemu wangu itoshe tu kusema kuwa NAKUPENDA, nimevutiwa na wewe na ninaamini kuwa ipo siku nitakutana na mwanamke mwenye sifa kama zako. Unavutia asikwambie mtu, rafiki yangu kaokota dodo chini ya mnazi. Mtoto umefundwa ukafundika

Mtoto wa mama umekamilika kila idara, una huo mshepu walai, sauti kama ya celine dion, sipati picha hiyo miguno pindi uwapo na rafiki yangu kwa chemba. Tabasamu ulilonionesha jioni hii ya leo limenidatisha sana. Najikuta nakuona wewe pindi ninapozifunga mboni za macho yangu. Ni wewe tu umetaradadi ndani ya moyo wangu

Wakuu, mniombee nipate mwanamke wa kufanana naye. Japokuwa nimekwisha mtumia sms kumueleza duku duku lililo ndani ya moyo wangu kwa maneno niliyoyaandika hapo juu. Ni nusu saa sasa sijajibiwa chochote kitu

Hakika rafiki yangu kapata chombo
images.jpg
 
Muda si mrefu mtashare abdalakichwapofu ya mumewe.
Endekekeza agape kwa mke wa rafikiyo
 
Back
Top Bottom