Nimetoa mahari ya Tsh. laki nane (8) nyumbani kwao na mzazi mwenzangu na wamenikabidhi binti yangu (mwanangu) ili nimsomeshe

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Wakuu nilipata kuzaa na mdada mmoja miaka kama mitatu hivi imepita. Kiukweli nimekuwa na mahusiano mema tu na mwanamke huyu kwa muda wote japo mie nimekuwa mtu wa harakati za hapa na pale na kutulia kwangu nyumbani ilikuwa shida.

Kutokana na hali hiyo ilibidi mzazi mwenzangu aendelee kuishi kwao huku mie nikiendelea na harakati huko duniani. Sasa hapa karibuni nilipoteza mawasiliano na mzazi mwenzangu na kupelekea ukaribu wetu kupungua hivyo kunifanya nipoteze imani naye.

Ni mwezi March ndiyo rasmi nimetulia na kumfata mpaka kwao na bahati mbaya alikuwa amesafiri na hakuwahi kunipa taarifa. Binafsi sikufurahishwa na usiri wake na niliamua kubreak mahusiano yetu.

Hivyo kwa mila na tamaduni zetu ilinilazimu kuwaandaa wazee kwa ajili ya kutoa mahari ya mtoto pekee ili awe mtu wa familia na ukoo wetu ambayo familia zilikubaliana kiasi cha laki 8 na jana mchezo umeisha.
 
Mkuu, Sijakuelewa. Ulibreak mahusiano halafu ukaenda kumlipia mahari huyo mzazi mwezio. Sasa tatizo lipo wapi?.

Tukio la wewe kupewa mtoto wako mbona ni haki yako au Ulinyimwa kupewa Mwanao hadi ulipe fedha za matunzo ya Mtoto?.
 
Mkuu, Sijakuelewa. Ulibreak mahusiano halafu ukaenda kumlipia mahari huyo mzazi mwezio. Sasa tatizo lipo wapi?.

Tukio la wewe kupewa mtoto wako mbona ni haki yako au Ulinyimwa kupewa Mwanao hadi ulipe mahari?.

Halafu jina la mtu huumba tabia. Jina lako 'The Lost' litakuja kusababisha ukapoteza kitu chako cha thamani ujue.
Ukimzalisha binti wa watu halafu bado hamjaoana, ikitokea mmeachana ili upate haki ya mtoto ni lazima umlipie mahali huyo mtoto ndio unakuwa na mamlaka nae.
 
Shukrani Mkuu ila mimi kuita hiyo pesa inayolipwa ili ME ampate mwanae kuiita mahari naona si sawa labda waite faini/tozo la kumkomboa mtoto etc.. Mahari analipiwa mke mtarajiwa tu.
Hizi taratibu wanazo wahaya.Yani ukizaa na binti wa kihaya bila kuoana itabidi ulipe hela(mahari) kwaajili ya mtoto wako hata kama ulikuwa unampa huduma zote.

Mambo ya kijinga sana haya.!
 
Ukimzalisha binti wa watu halafu bado hamjaoana, ikitokea mmeachana ili upate haki ya mtoto ni lazima umlipie mahali huyo mtoto ndio unakuwa na mamlaka nae.
Sasa wasiite hiyo Mahari. Waseme fedha za faini.

Tafsiri ya Mahari inatolewa kwa yule Binti unaemchumbia.
 
Ukimzalisha binti wa watu halafu bado hamjaoana, ikitokea mmeachana ili upate haki ya mtoto ni lazima umlipie mahali huyo mtoto ndio unakuwa na mamlaka nae.
Kwa utaratibu wa kabila gani? Maana unavyoongea ni kama vile nchi nzima inafanyika hivyo.
 
Kuna wapare wametaka kuniletea hii story.. nimeachana nao mtoto atakuja mwenyewe. Mwanamke mwenyewe Ana mabwana kibao mahari nilipe mie.. isitoshe Nina Mke niliyemlipia.. silipi mahari Mara mbili ni laana.
 
Huwa naona kabisa huko mbeleni nitanyimwa Mke. Hizi habari za mahari ya milioni, pesa ndani ya barua ya posa, faini ya kumtia binti yao mimba, mkaja wa nani sijui, blanketi la nani, koti la nani, kuwafungua vinywa wazee.
 
Back
Top Bottom