Nimetimuliwa na baba mkwe

Nina mchumba ambaye nimemchumbia na tuko kwenye mikakati ya kufunga ndoa hapo mwezi wa sita mwakani.
Jana jioni nilitoka na mchumba wangu kwa ajili ya matembezi ya jioni.
Nlipofika nyumbani kwao nikamkuta babake yupo kibarazani na mama yake.
Nikawasalimia lakini baba hakuitikia, akaanza kunigombeza kuwa mimi ni kapuku na sina vigezo vya kumuoa mwanae, akaniambia hapo hapo ulipo, toka nje.
Nikafungua geti na kuondoka.
Binti akawa nanipigia simu haongei chochote analia tuu.
Je niendelee na uhusiano huu au nijiondokee na umasikini wangu/

Hii habari yako haijitoshelezi inatakiwa taarifa zaidi. Hii mikakati ya harusi baada ya miezi sita ilikuwa inafanywa na nani? Je baba mzazi wa binti hakushirikishwa? Inakuwaje unamchukua binti toka kwao kwa matembezi ya jioni bila baba kuwa na taarifa kuwa una mpango wa kuoa kwake? Je mlishaonana na kuongea na baba wa binti kabla ya hili tukio au ndio ilikuwa mara ya kwanza unakutana naye?
 
Jamaa naona alisha elezea kuwa baba mkwe ndiye aliyepokea mahari na alikuwa akishiriki kwenye mpango mzima.
yeye baba mkwe ndiye aliyepokea mahari, nashangaa sijui siku zote hakuuona ufukara wangu ?
hii habari yako haijitoshelezi inatakiwa taarifa zaidi. Hii mikakati ya harusi baada ya miezi sita ilikuwa inafanywa na nani? Je baba mzazi wa binti hakushirikishwa? Inakuwaje unamchukua binti toka kwao kwa matembezi ya jioni bila baba kuwa na taarifa kuwa una mpango wa kuoa kwake? Je mlishaonana na kuongea na baba wa binti kabla ya hili tukio au ndio ilikuwa mara ya kwanza unakutana naye?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom