Nimetimuliwa na baba mkwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimetimuliwa na baba mkwe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bujibuji, Dec 21, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Nina mchumba ambaye nimemchumbia na tuko kwenye mikakati ya kufunga ndoa hapo mwezi wa sita mwakani.
  Jana jioni nilitoka na mchumba wangu kwa ajili ya matembezi ya jioni.
  Nlipofika nyumbani kwao nikamkuta babake yupo kibarazani na mama yake.
  Nikawasalimia lakini baba hakuitikia, akaanza kunigombeza kuwa mimi ni kapuku na sina vigezo vya kumuoa mwanae, akaniambia hapo hapo ulipo, toka nje.
  Nikafungua geti na kuondoka.
  Binti akawa nanipigia simu haongei chochote analia tuu.
  Je niendelee na uhusiano huu au nijiondokee na umasikini wangu/
   
 2. T

  The Lady Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani pole sana, mambo ya uhusiano sometimes ni magumu na yana complications nyingi. Cha msingi usikilize moyo wako wewe uamue. Iwapo utaamua kuendelea naye ipo tu siku mzee ataelewa kwani mapenzi ukihusisha na utajiri haviendi. Iwapo utaamua kutoendelea naye, mueleze ukweli kabisa bado mapema ili aumie roho lkn atazoea.

  Ila napata utata kidogo hapa, hadi mmefikia hatua ya kupanga kuoana mwezi wa sita mwakani, baba alikuwa hajashirikishwa? au mmejipangia nyie wawili kwanza? Maana kama alishirikishwa na kuridhia kuwa uwe mkamwana wake, asingekugeuka.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Kwani binti anasemaje?
  Ni yeye ambaye hakutaki au hutakiwi na baba mkwe ?
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Yeye baba mkwe ndiye aliyepokea mahari, nashangaa sijui siku zote hakuuona ufukara wangu ?
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Baba analamba mwanae
  Kakuonea wivu tu teh yteh tehe
   
 6. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Labda huyo dingi amegundua kuwa kwenu mna element za uchawi au magonjwa ya kurithishana ndio maana ameamua kukupiga chini.
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  demu anakupenda san
  baba hausiki cz labda anataka wa mahela meng na wewe huna BT CHA MSING DEMU AMEKUKUBALI KWA HALI ULIYONAYO SO POA WE ENDELEA
  USIWE NA MAWAZO YA KUMUACHA DEMU CZ HANA MAKOSA HATA KIDOGO utampa adhabu isiyostahili..
  ayo mawimbi tu...endelea kushikamana na demu ba mkwe atainua mikono juu km mkionyesha msimamo....MKWE MCHAGA AU MUHAYA?
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Mzee wa Kichagga
   
 9. u

  urassa Member

  #9
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaelekea umelipa mahari kidogo tofauti na mlivyokubaliana, kwa hiyo unaonyesha unataka mtoto wa watu bure Kama wewe ni fukara omba upewe bure.:target:
   
 10. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Baba mkwe keshachukua mahari and then unataka ujiondokee??!!
  Duh! umetoa mahari mapema sana,pia isijekuwa ndo kamchezo kao kuchukua mahari za watu na kuanza vi2ko!!!
  Bulaza komaa, kama hawataki chukua chako mapema usepe!!
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Hivi nini maana haswa ya neno mahari?
  Mi nadhani wazazi ndio wanapanga mahari kisha muoaji analipa kile kilichopangwa na wazazi, how come dogo awe amelipa tofauti na alichopangiwa?
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  nimelipa mahari yote hadi watu wakawa wanasema sio vizuri kulipa mahari kwani wakwe watasema najionyesha uwezo wangu, sasa najuata kwelikweli
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Baba anamwonea wivu mwanae - He is one of them - f!@k!
   
 14. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kaka huna kabati ya mbeo na redio ya picha.... Ohoo pole sna tupilia mbali tafuta mwingine kama ni mahali hela ni makaratasi hasara roho!
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ongea na huyo binti muelewane msimamo wenu ni upi.
  Nyie wawili ndio wa kuyasimamia maisha yenu.
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  niliwahi kukumbwa na mkasa kama huu ........ila kwangu alikuwa ni mama mkwe...........
  ilikuwa balaa sana sitasahau......kikubwa binti awe upande wako...kuna wazaz wanajudge the ice by its peak!!!!

  akikuona tu anajua uko kapuku kumbe...............!
   
 17. j

  jmisana Member

  #17
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtie mimba huyo binti baba atakukubali tu mazee,mahari kala alafu analeta za kuleta ?.
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Hii mbinu yako ya kimafia sana, lakini inalipa ile mbaya
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  wiki mbili zilizopita kuna rafik yangu alikuwa anafunga ndoa.....siku ya harusi ilipofika si kuna ile maharusi wanaenda saluni asubuhi then saa nane ndo ndoa inafungwa...basi bwanakumbe baba wa binti alikuwa mahali za watu wawili...huyu jamaa yangu ndo akafanikiwa kuoa...sasa siku hiyo binti anatoka saluni na mpambe wake wanaelekea kanisani....mim na bwana harusi tayari tuko kanisan... yule jamaa aliyechukuliwa mahali then akakataliwana n wazaz wa binti akiwa na nduguze... waliliteka gari la bibi harusi + mpambe.....wamekaa nao kusiko julikana kwa wiki nzina na juzi ndo wametelekezwa mahali usiku.....

  mpaka mda huu ninaoongea bwana harusi yuko hosp kalazwa.......

  presha iko juu sana...........
   
 20. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #20
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Du very sad story
   
Loading...