Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Siku kama ya leo mwaka jana ndipo nilijiunga na JF kwa mara ya kwanza. Ninapenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru wanaJF wote kwa upendo na uvumilivu mkubwa mliouonyesha kwangu katika kuchangia maada zangu. Ni vigumu sana kuwashukuru wana JF wote kwa kuwa ni wengi sana, zaidi ya 20000 na wote walikuwa na mchango mkubwa katika kuniwezesha kuendelea kuwa member wa JF na kuweka post zaidi ya 1000. Lakini kwa uchache tu nitapenda kuwashukuru: ACID, Mch. MASANILO, KIRANGA, Fidel80, KATAVI, PDIDY, PRETA, WOFSUBSTANCE, M/KIJIJI, NYANI NGABU, AFRODENZI, FIRST LADY, MUKANDARA, QUININE, MALARIA SUGU, JEYKEYWAKWELI, ABDURULAHM, THE BOSS, PAULS na wengine wengi sana kwa changamoto ambazo mmekuwa mkinipa katika posts ninazoweka.
Mwingine ninayependa kumshukuru katika namna ya pekee sana ni Invisible. Siamini kama siku zote nimekuwa nikiweka posts nzuri. Lakini invisible na moderator wengine wamekuwa wavumilivu sana. Kwa muda wa mwaka mzima sikupata ban wala onyo. Thanks wakuu. Nitajitahidi kuendelea kufuata sheria na taratibu za JF kwa umakini
Lakini wapo ambao kwa sababu moja au nyingine tulishindwa kukubaliana: wapo ambao tulipishana kwa wazi na wapo ambao inawezekana waligugumia kimoyomoyo bila kusema. Kwa namna yoyote ile tuliyotofautiana nawaombeni radhi kwa dhati kabisa, na ninaahidi kupunguza kasi ya kuwaudhi katika mwaka huu mwingine ninaoanza.