Nimetimiza mwaka mmoja JF

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Siku kama ya leo mwaka jana ndipo nilijiunga na JF kwa mara ya kwanza. Ninapenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru wanaJF wote kwa upendo na uvumilivu mkubwa mliouonyesha kwangu katika kuchangia maada zangu. Ni vigumu sana kuwashukuru wana JF wote kwa kuwa ni wengi sana, zaidi ya 20000 na wote walikuwa na mchango mkubwa katika kuniwezesha kuendelea kuwa member wa JF na kuweka post zaidi ya 1000. Lakini kwa uchache tu nitapenda kuwashukuru: ACID, Mch. MASANILO, KIRANGA, Fidel80, KATAVI, PDIDY, PRETA, WOFSUBSTANCE, M/KIJIJI, NYANI NGABU, AFRODENZI, FIRST LADY, MUKANDARA, QUININE, MALARIA SUGU, JEYKEYWAKWELI, ABDURULAHM, THE BOSS, PAULS na wengine wengi sana kwa changamoto ambazo mmekuwa mkinipa katika posts ninazoweka.

Mwingine ninayependa kumshukuru katika namna ya pekee sana ni Invisible. Siamini kama siku zote nimekuwa nikiweka posts nzuri. Lakini invisible na moderator wengine wamekuwa wavumilivu sana. Kwa muda wa mwaka mzima sikupata ban wala onyo. Thanks wakuu. Nitajitahidi kuendelea kufuata sheria na taratibu za JF kwa umakini

Lakini wapo ambao kwa sababu moja au nyingine tulishindwa kukubaliana: wapo ambao tulipishana kwa wazi na wapo ambao inawezekana waligugumia kimoyomoyo bila kusema. Kwa namna yoyote ile tuliyotofautiana nawaombeni radhi kwa dhati kabisa, na ninaahidi kupunguza kasi ya kuwaudhi katika mwaka huu mwingine ninaoanza.
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Keep it up!! but you forget to mention Fidel80

Very true DaMie, kwa kweli Fidl80 nadhani amesahaulika kwa bahati mbaya tu. Ni mtu mhimu sana katika mafanikio yangu. Thanks DaMie kwa kunikumbusha
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Usijali nipo hapo kwa wengineo hao

Mkuu Fidel80, kwa kweli ulipaswa utajwe, nafikiri ni bahati mbaya tu nilikusahau. Hatimaye nimeongeza jina lako. Mchango wako ulikuwa ni mhimu sana.
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Mkuu mimi nimekusamehe kabisaa kwa kutonilusha hapo!

Ha ha ha!! Henge, usijali mkuu. Upo katika kumbukumbu zangu lakini mpo wengi sana. Ningeweza kujaza ukurasa mzima wa watu mhimu kama ninyi:teeth:
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,212
2,000
: ACID, Mch. MASANILO, KIRANGA, Fidel80, KATAVI, PDIDY, PRETA, WOFSUBSTANCE, M/KIJIJI, NYANI NGABU, AFRODENZI, FIRST LADY, MUKANDARA, QUININE, MALARIA SUGU, JEYKEYWAKWELI, ABDURULAHM, THE BOSS, PAULS na wengine wengi sana kwa changamoto ambazo mmekuwa mkinipa katika posts ninazoweka.


Lakini wapo ambao kwa sababu moja au nyingine tulishindwa kukubaliana: wapo ambao tulipishana kwa wazi na wapo ambao inawezekana waligugumia kimoyomoyo bila kusema. Kwa namna yoyote ile tuliyotofautiana nawaombeni radhi kwa dhati kabisa, .
Mkuu, nambie, mimi niko kundi hilo la Bluu, au RED?......ni lazima tujichunguze bana!
Lakini Mkuu wangu hongera sana kwa mafanikio hayo...Kuna mengi sana tumejifunza toka kwako, na napenda nikwambie kuwa hakuna binadamu asiye na umuhimu katika Jamii yoyote!...Hata mwizi anakufunza kuwa makini!..right?
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,934
2,000
Mkuu, nambie, mimi niko kundi hilo la Bluu, au RED?......ni lazima tujichunguze bana!
Lakini Mkuu wangu hongera sana kwa mafanikio hayo...Kuna mengi sana tumejifunza toka kwako, na napenda nikwambie kuwa hakuna binadamu asiye na umuhimu katika Jamii yoyote!...Hata mwizi anakufunza kuwa makini!..right?
WEWE PAKA HATA MIMI NAKUWEKA KWENYE RED (jock)
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Mkuu, nambie, mimi niko kundi hilo la Bluu, au RED?......ni lazima tujichunguze bana!
Lakini Mkuu wangu hongera sana kwa mafanikio hayo...Kuna mengi sana tumejifunza toka kwako, na napenda nikwambie kuwa hakuna binadamu asiye na umuhimu katika Jamii yoyote!...Hata mwizi anakufunza kuwa makini!..right?
Mkuu Pakajimmy, bila hiyana kabisa upo kundi la bluu. Wale ambao hatukuwahi kukwazana. Shukurani sana kwa changamoto uliyonipa. Nafikiri umeona kwenye list ya niliowashukuru, hata Malaria Sugu na Jeykeywakweli wamo, japo sikuwahi kukubaliana nao hata siku moja kimtizamo. Lakini nimewashukuru kwa kuwa ubishi wao ulinifanya niongeze idadi ya posts.
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,212
2,000
WEWE PAKA HATA MIMI NAKUWEKA KWENYE RED (jock)
Afu Henge wewe hupendi kunitafuta tu wewe...Mi nduguyo kabisa ati!...Shauri yako bana...
Mambo vp lakini?...Wikiendi ndo inasogea hivi..unakula wapi?
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,934
2,000
afu henge wewe hupendi kunitafuta tu wewe...mi nduguyo kabisa ati!...shauri yako bana...
Mambo vp lakini?...wikiendi ndo inasogea hivi..unakula wapi?
mkuu itabidi nikutafute! Tuongee zaidi mkuu!
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,958
2,000
. Lakini kwa uchache tu nitapenda kuwashukuru: ACID, Mch. MASANILO, KIRANGA, Fidel80, KATAVI, PDIDY, PRETA, WOFSUBSTANCE, M/KIJIJI, NYANI NGABU, AFRODENZI, FIRST LADY, MUKANDARA, QUININE, MALARIA SUGU, JEYKEYWAKWELI, ABDURULAHM, THE BOSS, PAULS na wengine wengi sana kwa changamoto ambazo mmekuwa mkinipa katika posts ninazoweka.
[/B].

Hebu nifafanulie huyo hapo kwenye red unamshukuru kwa lipi haswa??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom