Nimetengeneza App ya kumsaidia mtoto katika mathematics

southern boy

Member
Jan 12, 2016
59
121
Kuna wakati nilikua nikiwaza juu ya kutengeneza kitu sana sana katika swala la Elimu. Sasa nimefanikiwa kutengeneza app like game inaitwa Endless mathematics quiz, ni app ambayo nimeiweka playstore itamchangamsha mtoto wa primary au o level katika hesabu za msingi (basic math) kwa kumpa hesabu za kujumlisha,kutoa na kuzidisha kwa sekunde mbili za kufikiria ili aweze kutoa jibu.

Mtu anaweza akapata maswali mengi awezavyo ila akikosa hapo ndipo game over na kuonyeshwa amepata ngapi.

Kwa mtoto huchangamsha akili na kwa mkubwa pia it`s so fun to play. Click link hapa chini ikupeleke playstore kudownload Endless Mathematics Quiz na pia naomba feedback nini cha kuboresha

Endless Mathematics Quiz - Android Apps on Google Play

ONGEZEKO/MABORESHO
Kutokana na mawazo ya watu kuusu hii app katika swala la muda, sasa muda umeongezwa hadi sekunde 3. Ila maswali 10 ya kwanza mtu atatakiwa kufikiria kwa sekunde 5 yanayofuata 10 (yaani 11 hadi 19) ni kufikiria kwa sekudne 4 na yanayoendelea kwa sekunde 3.

Pia imeongenzwa option ya kuweza kuangalia kumi bora (top 10) ya record ambazo umeweza kupata, yaani mfano kama umecheza mara 100 basi mara 10 ambazo umeweza kupata maksi nyingi zitarekodiwa
 
safi sana mkuu sema hao wa primary smartphone wanazipata wapi?maybe unge focus kwa hawa wa a level
hapo ndo kuna utata, hata hao o level wanabanwa wasitumie simu maana watahama kutoka lengo zuri kwenda lengo baya
 
hv nipe somo kidogo... ninavyoweka apps playstore mimi huwa nafaidikaje... au napataje faida kwa knowlegde niliyotumia..!!!

kuna mawili mkuu
mara nyingi ukiweka app playstore faida inakuja pale unapoifanyia monetization (kuweka matangazo ya google) ambayo hutokea kila mtu akiitumia app kipindi data ipo on

lingine ni kuwa yawezekana ukaweka app ambayo mtu atatakiwa kulipia ili kuitumia
 
safi sana mkuu sema hao wa primary smartphone wanazipata wapi?maybe unge focus kwa hawa wa a level[
/QUOTE]

Nilichowaza mimi ni kuwa ukiwa kma mkubwa na una mdogo wako au mtoto wako ni vizuri ukawa una mpa app hii siku 1 moja achezee ili kuongeza uwezo wake wa math

Alafu kwenye maelezo pia nimesema hta mkubwa anaweza akachezea sababu hufurahisha pia, just try it. Mi mwenyew nimeicheza sana its so fun kwa mkubwa
 
Watu wengi wamelalamika kuusu mda sasa mda umeongezwa hadi sekunde 3, ila maswali 10 ya kwanza utatakiwa kufikiria kwa sekunde 5 yanayofuta 10 yaani 11 mpka 20 kwa sekunde 4 kisha yanayoendelea ni sekunde 3
 
Hesabu ni mazoezi tuu

Sitaacha kumtolea mfano binti mmoja alikua hapendi hesabu kama nini form 2 necta alikula F tulipo ingia form 4 mwanzoni alikuja mwalimu akawa anatoa sana mazoezi mpaka kufika necta yule binti alipata B

Hapo ndipo nolipoamin binadamu wote ni sawa
 
.hongera sana..hii app nitasuggest kwa ninaowafaham wanapokuwa nafas badala ya kuwapa watoto wacheze game wanaweza kutumia hii app..its useful..
 
Kuna wakati nilikua nikiwaza juu ya kutengeneza kitu sana sana katika swala la Elimu. Sasa nimefanikiwa kutengeneza app like game inaitwa Endless mathematics quiz, ni app ambayo nimeiweka playstore itamchangamsha mtoto wa primary au o level katika hesabu za msingi (basic math) kwa kumpa hesabu za kujumlisha,kutoa na kuzidisha kwa sekunde mbili za kufikiria ili aweze kutoa jibu.

Mtu anaweza akapata maswali mengi awezavyo ila akikosa hapo ndipo game over na kuonyeshwa amepata ngapi.

Kwa mtoto huchangamsha akili na kwa mkubwa pia it`s so fun to play. Click link hapa chini ikupeleke playstore kudownload Endless Mathematics Quiz na pia naomba feedback nini cha kuboresha

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.NmasweTech.Endl essMathQuiz

Umetumia programming language gani Mimi nilitengeneza ya kumsaidia mtoto kujua namba kwa kingereza kwa mfano akiweka input 120 inamunyesha one hundred and twenty
 
Umetumia programming language gani Mimi nilitengeneza ya kumsaidia mtoto kujua namba kwa kingereza kwa mfano akiweka input 120 inamunyesha one hundred and twenty
Nimetumia C sharp (c#) kutengeneza. Weka basi hata link mkuu ya hiyo app yako ili tuichecki
 
Nimetumia C sharp (c#) kutengeneza. Weka basi hata link mkuu ya hiyo app yako ili tuichecki

Bado sijaimplement version ya simu.hii inarun kwenye pc ndio nataka nitengeneze ya kuweka kwenye play store,kuna application nyingine ambayo umeishatengeneza? Nami ni programmer nadhani tunaweza kuexchange experience katika application development
 
Ouk basi kama ikwezekana nitumie hata kwenye email hizo setup za hiyo app (isayaexavery@yahoo.com) niicheki. Kuusu application nyingine nilizotengeneza ni hizi
1. Akili Test - Ipo playstore Bofya link hii ku-download- Akili Test - Android Apps on Google Play

2. Cards Memory Test - Ipo playstore bofya link hii - Cards Memory Test - Android Apps on Google Play
 
hapo ndo kuna utata, hata hao o level wanabanwa wasitumie simu maana watahama kutoka lengo zuri kwenda lengo baya
Wazazi wanawaazima cmu zao watumie kwa muda ambao mtoto anapaswa afanye hizo hesabu baada ya hapo anaichukua cmu yake.
.hongera sana..hii app nitasuggest kwa ninaowafaham wanapokuwa nafas badala ya kuwapa watoto wacheze game wanaweza kutumia hii app..its useful..
Yap uko sahihi.
 
Back
Top Bottom