Nimetembelea Arusha mara ya kwanza nimekutana na kabila linaitwa Waarusha, sijawahi kulisikia

wa arusha ni wamasai,ila historia yao ni kwamba miaka hiyo ya nyuma hao wa arusha ambao ni wamasai walikuwa wanakaa milimani huko moshi, ila baada ya vita ya wamasai na wapare baadhi ya wamasai walikimbilia arusha ndio baada ya kuisha hapo miaka mingi wakaamua kujiita waarusha kwasababu hapo arusha mjini wao walikuwa wageni ndo maana waliamua kujipa identity hiyo ya waarusha.
ila tukiacha hayo pale shivaz ni hatari sana yani utasema kona bar ya mjini dar
shivers ilikua zamani
 
Umuofia kwenu wanajamvi.

Katika pilika zangu za maisha nimeingia jijini Arusha kwa Mara ya kwanza. Cha kushangaza mwenyeji wangu kanitembeza Sanawari, Mianzini, Kijenge, Sakina, Morombo na maeneo mengi tu na nikagundua kabila wanaoitwa Waarusha.

Nilikuwa sijui hii kitu kabisa kwa sababu Arusha ni mkoa wa Wamasai. Pia wachaga ndiyo wenye jiji hili tofauti nilivyokuwa najua ni la wamasai. Makabila mengine makubwa jijini ni Wairaq na Wapare. Ni wengi mno jijini. Wamasai ni wachache mno.

Hili nilikuwa sijui kabisa na utafiti wangu mdogo wa sosholojia ya Arusha mjini umenijuza mengi. Nitakuja na mambo mengine mapya bila kusahau ile mitaa ya vituko ya Shivaz na Mrina.
ACHA KUPOSHA WALAINI WENZAKO, R HAKUNA KABILA LA WAARUSHA ZAIDI YA WAKAZI WA ARUSHA, KUNA KABILA LA WAMAASAI WANAO WAITA WAARUSHA NI KUTOKANA NA MAKAAZI ....
SECONDLY WACHAGGA NI INTRUDERS WALIYOPO MAHALA PENGI NA SIYO KWELI ETI NDIYO WATAWALA KWANI PIA NI MAJIRANI NA WAMAASAI HIVYO HATA INTERMARRIAGES WAMEFANYA SANA KUTOKANA NA UJIRANI WA KARIBU.
VIVA CHUGGA SISI NDIYO WA R THE OG POWER AND POOLING NA SIYO WA VILAINI KAMA WALIVYO KULE...ILA TUNA WA BOOST NA KUWASAIDIA KWA SANA KAMA KAWA.
 
nikama tu vile watu waliozaliwa mitaa ya kariakoo na maeneo ya katikati ya jiji la dar es salaam wanavyopenda kujiita "wana dar es salaam" ilihali kimakabila sio wazaramo bali ni watu wa makabila mchanganyiko ya tanzania na wahamiaji toka sudani,wahabesh na waarabu wenye asili ya oman na yemen.

mfano wa hili ni mzee wangu Mohamed Said
 
Hao ni mongoo mkuu, Hawataki Umasai wao kisa tu kukaa town muda mrefu, Asilia ni Wamasai Kabisa
KAMA NI SABABU YA KUKAA MJINI WALE WAARUSHA WANAOUSHI OLDONYOSAMBO HUKO NAKO NI MJINI? PIA WANAZUNGUMZA TOFAUTI NA WAMASAI. WANASIKILIZANA SIO 100% . YAANI NI KAMA WACHAGGA WA MACHAME NA WAMERU.MBONA WAMERU SIO WACHAGA? NILIWAHI KUSOMA NAO UMASAINI NIKIWA MDOGO MWARUSHA NA MAASAI WAKO TOFAUTI HATA KIMAUMBILE? WAMASAI WENGK SLIM WAARUSHA SIO
 
Niliwahi kusoma mahali kwamba kabila la Waarusha limetokea mkoa wa Kilimanjaro eneo linaitwa Arushachini miaka ya 1800 na kuweka makazi kwenye himaya ya Wamasai eneo la Selian, Arusha (wanajitofautisha hivyo na wamasai pamoja na kwamba wanaongea kimasai ila kwenye shughuli za kiuchumi wao walijishughulisha na Kilimo zaidi)

Nilisoma tu mahali msinihoji sina majibu ila nilikaa Arusha miaka flani wengi wanasema hao ni wamasai tu wa mjini
Mimi sikijui kimasai ila hao Waarusha hata mimi niliwahi sikia asili yao ni wachaga ila sikumbuki ni upande upi wa uchagani. Wanao wajua vizur Waarusha wanasema hata baadhi ya maneno yana fanana na uchagani.
 
Mje na tanga mshangae makabila hamjawahi sikia kabisa.
mwawajua Wasegeju nyie?
Mwawajua Wanguu?
Mwawajua Wadaiso?
 
Makabila yenye nguvu kimapato kwa mji wa Arusha ni Wachaga, Wapare, Waarusha, Wameru mwisho Wamasai.
 
Siku ukijua historia ya maasai ndio utajua kua waarusha ni wamasai endelea na research yako ila jua kwamba kuna wamasai aina kumi na mbili na wote ni wamasai
Nimekaa Arusha more than 20 nawajua vzr sana waarusha hamtakag kuitwa masai tena utawasikia na wao wanawaponda wamasai
 
Back
Top Bottom