Nimetapeliwa Sinza

Nimetapeliwa Sinza

Hekaya za Abunuasi

Senior Member
Joined
Jan 6, 2014
Posts
166
Reaction score
38
Ndugu zangu nisaidieni kama naweza kuwapata walionitapel na warejeshe malipo niliyoyatoa.

Siku moja nilienda Sinza kwa Remy nikitafuta nyumba!Nilionyeshwa dalali na nikazunguka naye,nyumba alizonionyesha sikuridhika nazo!Baada ya cku 2 nikapigiwa simu na akasema umepata nyumba?Nilimjibu bado then kanambia njoo kwa Remi kuna nyumba!Ndugu zangu nilitoka Posta Haraka,nilipofika Kwa remi nilimpigia simu akanambia kuwa yeye ameenda kumuonyesha MTU shamba lkn ana kijana wake anaitwa Fred,after 6mins alikuja kijana akatupeleka kuangalia nyumba.Niliona nyumba nikamuuliza mwenye nyumba yupo wapi?Akasema Makongo!Kesho yake huyu Fred(0656389300) akatupeleka makongo kwa Mwenye nyumba tukalipa.

Siku ilifika ya kuhamia kabla ya kuhama tuliwasiliana na yule mwenye nyumba hapatikan kwa simu.Kumbe tumelipa kwa MTU fake.Nilifungua RB na nilienda na police wawili pale nilipolipia geti halikufunguliwa!Siku nyingine niliwachukua ten a police wa upelelezi tukavizia mvua inanyesha tukApiga hon getin get likafunguliwa.Kijana akatukaribisha sebulen,wale polise wakiwa na nguo za kiraia walimuuliza yule kijana mzee yupo akasema yupo wakamwambia sisi nin wagen wake.Ile nyumba INA kigorofa na yule kijana alipanda juu dk5 akashuka akasema kwan hamkuwasiliana na Mzee kwa simu?

Mzee hayupo yupo Zanzibar na anakuja Leo jion.Police walimwabia yule kijana Tupe namba zake yule kijana akatoa namba na polise alipiga ile no. Jamaa akapokea akasema hayupo Zanzibar na anafanya kazi bank na hataki usumbufu kama police WAPO kwenye nyumba yake basi waichukue au waichome moto,Ila huyu jamaa naamin alikuwa ndan nikawambia polisi wakasema hawana search warrant.Tukarudi.

NDUGU ZANGU NAWAOMBENI MAWAZO YENU AU USHAURi ili tuwakamate hawa matapeli waweze kurudisha hizi hela kwan nilikopa ndugu zangu.AHSANTEN
 
Bei gani ulitoa mkuu? Pole sana hao jamaa wanajiamini na nini kiasi hicho? Duh aisee
 
Duh! pole sana. Laiti Polisi wetu wangekua wanafanya kazi kwa dhati na ARI ya kupambana na utapeli, hiyo ingekua kazi rahisi sana kwa sababu tayari unapo pa kuanzia.

Achana na hao akina Fredy na number zao za simu, pahala pa kuanzia ni hapo kwenye nyumba. lakini agh! sijui,, usikute ukaendelea kutupa tu gharama nyengine zaidi.
 
Pole sana ndugu yangu.
Kwa kweli inasikitisha sana watu wakiwekea maisha ya kuishi kwa utapeli tu. Its shame Tanzania tuko katika hali kama hii.
Mimi nafikiri kazama na Polisi lazima mwenye nyumba atajulikana tu. Kwanza huyu kijana anayeishi hapo atakuwa anajua mpango mzima hao matapeli. Huyu ndo wa kuanza naye.
Kwa kweli inauma. Pole sana
 
Inakera sana aisee, yani 6m mtu umezisaka kwa jasho then mwingine anaichukua tuu!! Ndio mana wanarogwa hakyamama
 
Ahsanten ndugu!Million tatu nililipa cash!the rest kwa tigo pesa kwan alinambia amefiwa anazika Mpwapwa kwa hiyo nimtumie ili awatumie mafundi wamalizie ukarabati
 
Aisee una slip au mkataba wowote nao....? Usikate tamaa kirahisi muombe Mungu atakuonyesha njia.....banana na wapelelezi anza kumuweka,ndani yule dalali wa kwanza, Fredy na huyo mwenye nyumba hewa....jipe moyo, jiamini, naamini utapata haki yako bila kutoa hata kumi polisi....
 
Polisi nao wa siku hizi unaweza kujikuta unapoteza tena pesa zaidi za kuonga.., jaribu kama kuna wenyeji wa mitaa hiyo au wababe mtaani waulize wakutafutie huyo kijana Fred ili uanzie hapo, kama wanafanya mambo kiujanja ujanja ni ku-solve kiujanja ujanja pia. Utapeli sio mzuri kabisa unachukua pesa ya mtu wala hujui kaipata kwa shida gani wala huu sio ujanja ni ujinga ambao mtu unaweza kupoteza maisha yako kwa kuganga njaa. Wabongo tubadilike
 
Dah. Pole mkuu, ila kuna umuhimu wa makubaliano yetu yoote siku hizi kuwa na mwanasheria. Mimi kwakweli injustice za nchi yetu zinanifanyaga hata kutumia illegal means mida ingine. Chukua zako wazee wa kazi wa 4 mnamtaimu jamaa, kibano cha nguvu then unampa wiki arudishe hela. Kuepuka usumbufu wa ushahidi hata usiwepo letewa picha tu.
Au kama vipi samehe! Mimi mpaka sasa nimetapeliwa zaidi ya mil 15 mpaka nimeamua biashara za kitaa sasa basi!
Ila kuna jamaa mmoja mkiona nyamgluu sipatikaniki JF kuanzia wiki ijayo mjue nimekimbia nchi, maana yule lazima nim Ulimboka kwa kweli!
 
Mkuu pole!! Huenda police wanajua hilo swala lako' nawashakula kitu.

Hiyo pesa ni nyingi' na pigana paka upate hatma yake.

Kama police wameshindwa kukupa ushirikiano fanya hivi' tafuta vijana wakazi uwaonyeshe hiyo nyumba kimya kimya then walipe vizuri' kazi yao ni kati ya hizi mbili itakayofaa tumia.

1) wamteke mtoto wa mwenyenyumba au mke wake hata yeye mwenyewe ikiwezekana (then peleka sehem itakayokuwa ya Siri yako nahao uliowatuma' mlishe na mpe kila kitu ila awapigie ndugu zake kwamba kapewa masaa kadhaa wasipo tuma pesa anamalizwa)

2) vuta pumzi na punguza jazba' jifanye umepotezea tu then kaa mda utakaodhani watakuwa wamejisahau' then tuma vijana wakafanye kazi nzuri yakuiwasha moto hiyo nyumba ya makongo..

Ni mtazamo tu'

Akili zakuambiwa changanya na zako utapata mwafaka mzuri tu.
 
Pole sana mkuu...(ashakum si matusi )i nakushauri ubadili na jina...(no offense)..
 
Haki ya nani poleni sana.Mie nina dada yangu ana bonge la jumba Tegeta anahangaika kutafuta mtu wa kuishi humo kwa miaka mitatu maana yeye anaenda kusoma.heeee wengine mnatapeliwa jamani kweli watu tunatofautiana.
 
Polisi nao wa siku hizi unaweza kujikuta unapoteza tena pesa zaidi za kuonga.., jaribu kama kuna wenyeji wa mitaa hiyo au wababe mtaani waulize wakutafutie huyo kijana Fred ili uanzie hapo, kama wanafanya mambo kiujanja ujanja ni ku-solve kiujanja ujanja pia. Utapeli sio mzuri kabisa unachukua pesa ya mtu wala hujui kaipata kwa shida gani wala huu sio ujanja ni ujinga ambao mtu unaweza kupoteza maisha yako kwa kuganga njaa. Wabongo tubadilike

Nakushauri ukipata tena pesa kana hizo sogea kando ya mji upate kiwanja. Milioni sita unamaliza chumba na kuhamia. Ni pesa ndefu. Achana na kupanga kama kampuni za simu ambazo zinajua tanzania zinapita tu.vyou arwle here to stay for the rest of your life.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom