Nimetapeliwa na mdada wa TPDF, ushauri wenu tafadhari

Nimetapeliwa na mdada wa TPDF, ushauri wenu tafadhari

Majeshi wa kike ni Mish-kaki ya wakubwa, don't west your time kijna....songa mbele ulikosea kumpa kilo 2 kwa pamoja next time kukiwa na dili ambayo inakuwia vigumu kwako kuisamehe...jaribu kulipa kwa mafungu(installments) Nusu mwanzoni na nyengine ukifanikiwa....Pia usiwe unaingia kichwa na dili zinazovutia sana...jaribu kushauri watu walokuzidi kiumri na elimu kabla hujaliwa kijana "Don't go to the offers that are so good to be true"
 
@umuhiri malato kama tamko la Nyerere lingekuwa sheria basi viboko 24 vingekuwa vinakusubiri; 12 siku unaingia na 12 siku unatoka ukamuoneshe mamsap.
 
Last edited by a moderator:
Kama unaamini uchawi hebu mloge kwanza! Wacha ubwege.. unapenda njia mkato umekutanana na mjanja sasa unatafuta haki gani wakati mwenyewe ulitaka kutoa rushwa!
 
ushatapeliwa si tukusaidiaje kinachofuata ni kwenda zako wema ushatenda
 
dada huyu anaitwa Tiba Abdallah ni askari JW, makao makuu JKT, nimaliza nae form four 2008 Nyanduga sec,mwaka jana alinipigia cmu kuwa kuna nafac za jw zimetoka nimtumie pesa na vyeti kwenye email,nikamtumia, hadi leo hii cmu hapokei sms hajibu nikipiga namba mpya akickia sauti yangu anakata facebook ameniblock, nifanye ndugu zangu nimloge,

Nifatilie makao makuu ya jeshi maana uthibitisho wa sms za m pesa upo,npo mkoani nifunge safari nikafatilie dar?,tafadhari watanzania nishaurini nimfanyeje mtu huyu, inaniuma kutapeliwa na mmtu ninaemfahamu na pesa yangu ni zaidi ya laki mbili wapendwa?

Toa upumbafu wako hapa..ulikuwa mvivu kusoma sasa unaanza kusumbua watu kutafuta kazi..nenda kalime huko
 
mtoa rushwa na mpokeaji rushwa wote mna makosa ,funga safari uone kilichomtoa kanga manyoya.we mpotezee jipange kivingine mkuu
 
Mimi nakushauri kwa upande wa kuku block facebook.Fungua akaunti nyingine ya facebook kisha mtafute na umfikishie ujumbe wako.

mkuu hujamuelewa mlalamikaji, anasema mdaiwa hata meseji hajibu,..
 
Kimsingi hatupaswi kutoa lawama kwa upande mmoja,
Sheria inasema mtuhumiwa ana haki ya kusikilizwa.tayari tumekusikiliza wewe, fanya utaratibu ututafutie Huyo Tiba Abdalah nae tumsikilize.
 
Potezea bwana hela hiyo ndogo sana usimloge mtu kisa hicho kijisenti plz potezea kabisa. Kwani kwa sasa unafanya kazi gani ?
 
Kama unaridhia kupoteza hiyo pesa ebu tuwasiliane nimfanyie mnyanga nimgeuze hata mbuzi uje umle hata siku ya idd mkuu umuhiri marato
 
Last edited by a moderator:
Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote mamzang'anya wote mna makosa.
 
Inaonekana tu upeo wako mdogo katika utafutaji na kama ulifanya siri mbona mnaumbuana sasa maana huenda hela yako ulomtumia kwa vile ulikuwa unamsumbua akuunganishe huenda kwa kukupa matarajio kakuambia tuma fedha fulani kwa akili yake akidhani itachukua muda mrefu ili apumzike na kero zako kumbe wewe ukawatangazia ndugu zako na wao kuamua kupitisha mchango na kukukabidhi ili upate hiyo kazi kwa muda mfupi ambao mwenzio hakuutegemea!. Huenda kwasasa mwenzio anashindwa akuelezeje nini maana wewe lengo lako ni kazi kwa namna yeyote hata kwa kuvunja sheria za nchi!
Ushauri
Futa kauli yako kwa kuondoa uzi huu na kisha tafuta ndugu wa rafiki yako ili ukapewe pesa zako kirahisi na si kuchafuana kupitia mitandao ila kama roho yako ni chafu/unafurahia rafiki yako kukosa kazi basi fuata ushauri wa kuandika barua uliotolewa na wadau hapo juu! Ukweli unaujua wewe ni nani alimshawishi mwenzake na kumbuka kuwa huenda hata sms ulizokuwa unamtumia huenda na mwenzio amezihifadhi huku akisaka ushauri kwa walio karibu naye juu ya jibu gani akujibu bila kuja mitandaoni na kukutaja kama ulivyofanya wewe! Angalia sana maisha yako unaonekana unaharaka/unataka njia ya mkato ya kufaulu kimaisha bila kusota ambapo ni hatari kwako na kwa wanaokutegemea kama mtu msomi katika ukoo!!
 
Pole ndugu yangu,hela imekwenda na ndugu yako anasota nyumbani!Usikute na cheti cha kufoji nayo ulinunua.
 
Back
Top Bottom