Nimetakiwa kuripoti Polisi Central kesho bila kujulishwa sababu yoyote

Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,045
2,821
Wakuu Leo kwa upole nawasalimu wote kwa unyenyekevu wa kipekee uliojawa hofu na huzuni kubwa.

Utakapo jadili au kuchangia naomba uzingatie hili bila kuongeza sababu yoyote ya zaidi kuhusu mwenendo wangu wa maisha. Mimi ni mfanyakazi serikali na sana nimebase kwenye biashara zaidi ya kazi na zaidi sijihusishi na mambo yoyote ya uvunjaji wa sheria kwa maana ni RAIA mwema na niko highly respected katika mtaa wangu kutokana ni jitihada zangu za kimaendeleo kiasi cha kuwa role model wa vijana wengi mtaani. Niko ofisi zangu tatu ambazo zimekuwa zikiletea maendeleo kiasi cha watu kushangaa.

Kilichonistua Leo saa 4 usiku nikiwa nataka kufunga biashara yangu nimefuatwa na watu wawili waliokuja ofisini kwangu wakiwa katika gari aina ya Harrrier old model na kunifahamisha wao ni maofisa wa polisi kitengo cha upelelezi kutoka central polisi na mmoja amenionyesha kitambulisho lakini nikiwa na bumbuwazi hata sijakumbuka hata kunote jina.

Wamenifahamisha kwamba Nina kesi ilioko huko central na natakiwa kuondoka na wao usiku huu. Bahati nzuri dukani kwangu kuna ukuta wa nondo mtu hawezi ingia ndani. Nilipotaka wanijulishe Nina kesi gani? Hawakutaka na walitaka kutumia ubabe ila ilibidi niite jamaa zangu wanisaidie kujua tatizo. Baada ya kufika rafiki zangu wa jirani, jamaa wakashuka kidogo na wameniuliza maswali yafuatayo:-

1. Unaitwa Fulani (wakitumia professional yangu je ni kweli nina taaluma hiyo? Jibu ndio
2. Nina kitambulisho cha kazi au cha Uraia? Jibu ndio.
3. Kwa nini tulipoacha namba ofisini kwako takribani miezi miwili nyuma hukutaka kutupigia? Jibu, sikupewa taarifa na hamjaacha taarifa kwamba nyie ni polisi nilijua za watu tu kawaida na huwa simtafuti mtu bila shida.

Mwisho wameniachia ila wamenitaka kesho saa 4 nilipoti polisi central kwa mahojiano. Na wamenisihi kama nitakuwa na kitambulisho cha kazi nisiende na mdhamini ila kama sina lazima niende na mtu wa kunidhamini. Sikuwahi tegemea hata siku moja nitatakiwa kuripoti wanakoripoti watu wenye makosa makubwa hata Mara moja. Na mpaka muda huu usingizi sina siku hizi hawachelewi kukupa kesi ya uhujumu uchumi. Binafsi sijioni kuwa ni mtu wa hatari kwa kiwango hicho.

Naombeni msaada wa mtu mwenye uelewa wa matukio kama haya. Nina work ID je niende pekee yangu au nichukue backup? Msaada wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pole Mkuu, Nenda na Mdhamini hii itaweka shikizo katika Reaction baada ya lolote kutokea huko polisi. Mambo ya Job ID yataleta delay tuu Naona

Lakini umerisk ID yako ya JF Mkuu what if hao maafisa wako humu JF si ushajianik hapo uwe mzee wa Siasa Sasa

I'm on that good kush and alcohol
 
Nitafanya, kuhusu Id ya Jf siyo shida, mimi si mtu wa masiasa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole na mkasa ndio dunia ilivyo. Cha msingi nenda na mwanasheria wako usiende bila mwanasheria wako. Onyo
 
Mkuu pole kwa kipindi hiki tegemea lolote hivyo nakushauri kufanya yafuatayo.
Mosi wape taarifa ndugu zako ikiwa ni pamoja na familia yako.
Pili hakikisha unamshirikisha mshauri wako wa kisheria juu ya hilo na umsihi awepo kipindi cha mahojiano hayo
Tatu mpe taarifa mjumbe wa mtaa au mwenyekiti wa mtaaa.
Kamwe usiende pekee yako shukuru kwa kuwa zoezi lao la kukuchukua pekee yako limekwama.
Ni hilo tu zaidi Mshirikishe Mungu katika maombi
 
Ahsante, najitahidi kufikia ushauri wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom