Msaada: Nahitaji taasisi ya mikopo Mwanza

Chawa Namba Moja

New Member
Jan 2, 2024
3
2
Wakuu salaam,

Niende direct kwenye jambo langu.

Binafsi ninajishughulisha na kazi zangu binafsi kwa mwezi huu mambo yamekuwa ni magumu sana. Nimejipiga piga wataoto wamekwenda shule kwa mshike mshike.

Lakini kuna sehemu waga napeleka mzigo,kulingana na mwezi huu nimejikuta nimetumia hadi mtaji wangu na muda huu nimekwama sijui pa kutokea.

Naomba kwa wadau wanaojua watu binafsi wanaokopesha maana yake ni kwamba sina sifa za kukopesheka benki yoyote kwasababu sio muajiliwa wa serikali au kampuni binafsi.

Nina barua ya manunuzi ya kiwanja kama dhamana yangu na pia kiasi ninachoitaji ni laki 3 tu kama kianzio. Kwa yeyote anaejua mtu anekopesha au ki taasisi kidogo cha ukopeshaji anisaidie wandugu.

Nina hali mbaya sijui nitaishi vipi.

Wadau wa mwanza anaejua anifahamishe.
 
Mzee kukopa kwenye vitaasisi uchwara iwe option ya mwisho. Ukikopa laki 3 usikute riba kwa mwezi ni 50% ambayo pengine itakula faida yako.

Jaribu kuwasiliana na unakopelekaga mzigo wakuazimishe, utawalipa ukishafanya biashara.
 
Kama shida yako inavumilika na unaweza kuitatua kwa njia nyingine itatue mkuu
Ili kwenda kwenye taasisi za mikopo sikushauri ndugu yangu hao jamaa wanariba kubwa Sana kiasi kwamba wanaonufaika ni wao na siwewe mkopaji
 
Back
Top Bottom