flintsky
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 654
- 747
Habari za Jumapili,
Usiombe haya yakukute hata ungekuwa mbabe kama Scopion lazima uwe mdogo kama sisimizi.
Nina rafiki mmoja tumeshibana sana yaani ni zaidi ya rafiki au naweza kusema ameshakuwa ndugu yangu.
Ana mpenzi wake ameshamvalisha pete kitambo tu kinachosubiriwa ni ndoa tu, kiukweli yule mwanamke hajatulia kabisa ni zaidi ya mara moja nishamkuta katika mazingira sio mazuri tena wanaume tofauti na mapozi ya kimapenzi! Kuna rafiki yangu mwingine aliendaga nae hadi Mbeya akakaa nae wiki mzima huko yeye alienda kikazi.
Niliamua kukaa kimya maana kuingilia mapenzi ya watu mwisho utaonekana mchonganishi nikanyamaza ili jamaa mwenyewe siku aje ajionee lakini ikawa inaniuma sana naona rafiki yangu pale anapotezewa muda tu.
Nikaamua kujifunga mabomu nikamueleza nje ndani zote za mchumba wake! Jana nimefika ofisini asubuhi naambiwa natafutwa na mwanamke [emoji15] huku jamaa wananiangalia dizaini flani! Haijapita muda hamadi shemeji huyu hapa hajanawa hata uso wala kupiga mswaki kanisimamia mbele.
"Haya nieleze lini nilikuuzia maana unasema mimi nauza" jasho lilitoka nikaanza kusweti balaa ikabidi niwe mdogo nikajitetea tu kwamba nililewa ili niue soo, maana watu wa ofisini wakaanza kujipitisha wajue kuna nini? Daah! Yaani hapa najuta kumwambia msela nimeona namsaidia kumbe sikio la kufa haliskii dawa, sina hamu.