Nimesoma Ualimu nimemaliza lakini sina kazi

Nyie watu mnaotoa majibu rahisi kwa hoja ngumu mnakela sana, ni bora ukawa msoma.comments tu kuliko kuandika maneno yenye kukera watu kama haya.

Hivi unajua Tanzania,private schools ziko ngapi? Na tangu serikali iache kuajiri walimu ni lini na je kila mwaka kuna wahitimu wangapi wanaletwa mtaani?...
Kaka Nina hakika na wewe unaandika tu hapa hata hujawahi kwenda kwenye shule hata moja, Mdogo wangu amemaliza form six akaona kukaa iddle hakufai, jirani Luna shule ya sekondari ya serikali akaomba kwenda kujitolea, wakapenda kazi yake na kuanza kumlipa allowance, Mi siongei uzushi naongea experience ya kweli.
 
Kaka Nina hakika na wewe unaandika tu hapa hata hujawahi kwenda kwenye shule hata moja, Mdogo wangu amemaliza form six akaona kukaa iddle hakufai, jirani Luna shule ya sekondari ya serikali akaomba kwenda kujitolea, wakapenda kazi yake na kuanza kumlipa allowance, Mi siongei uzushi naongea experience ya kweli.
Mkuu Mimi ni mwalimu kwa taaluma, ninajua shida iliyopo katika kupata nafasi kwa private schools,enzi zangu wasomi walikuwa wachache lakini nilipomaliza chuo nilitembeza barua za maombi hadi nilichoka,

Acha kabisa kurahisisha unapoongelea changamoto za kupambania maisha

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Nyie watu mnaotoa majibu rahisi kwa hoja ngumu mnakela sana, ni bora ukawa msoma.comments tu kuliko kuandika maneno yenye kukera watu kama haya.

Hivi unajua Tanzania,private schools ziko ngapi? Na tangu serikali iache kuajiri walimu ni lini na je kila mwaka kuna wahitimu wangapi wanaletwa mtaani?...
Kwa mara ya kwanza leo umeongea point ya msingi
 
Mkuu Mimi ni mwalimu kwa taaluma,ninajua shida iliyopo katika kupata nafasi kwa private schools,enzi zangu wasomi walikuwa wachache lakini nilipomaliza chuo nilitembeza barua za maombi hadi nilichoka,

Acha kabisa kurahisisha unapoongelea changamoto za kupambania maisha

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Kaka uliomba kujitolea ukakataliwa?
 
Kaka uliomba kujitolea ukakataliwa?
Mkuu. Mimi bado nakuambia wewe ni mtoto wa mama ,sasa hebu chukulia mtu chuoni alikuwa anajisomesha hana baba wala mama Leo hii umwambie ajitoleee atakula nini?

Mambo ya kujitolea ni watoto wa mawaziri na wabunge sio kwa mtoto wa mkulima.acha kabisa ,kuna watu sana maisha magumu Sana halafu umwambie ajitolee ,dheni kwa muda gani?



Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mkuu. Mimi bado nakuambia wewe ni mtoto wa mama ,sasa hebu chukulia mtu chuoni alikuwa anajisomesha hana baba wala mama Leo hii umwambie ajitoleee atakula nini?...
Hapa ndio kwenye changamoto kaka, kwenye kujitoa kuna baraka sana, haijalishi background yako. Sio kila mahali utaanza kwa kupata pesa.
 
Hapa ndio kwenye changamoto kaka, kwenye kujitoa kuna baraka sana, haijalishi background yako.
Sio kila mahali utaanza kwa kupata pesa.
Mwenzio kaandika NUMBERS wewe unaandika maeneno rudi juu kapige mahesabu ya zile takwimu walimu wote wakijitolea kila shule itakuwa na walimu sichini ya 200+ je hiki kinawezekana kuwapa hapana ndio maana kutokana Number haingopi walimu kibao washaomba kijitolea shule kibao jibi nk hakuna nafasi ukienda kuomba.

Leo kuna mwenzio katoka jana kuomba ila yote kwa yote katika maisha yangu siwezi kujitolea ni ujinga ingekuwa kujitolea inakupa mazingira ya kukupa ajira ya uhakika (serikali) hakuna graduate angeacha ila kuomba kujitole mbimde, kupata mbinde, ukipata kulipwa mbinde, ukiwa unalipwa pesa ya ice cream, ukipewa ajira kabisa bado si ya uhakika na ashahara mkangafu.
 
Mwenzio kaandika NUMBERS wewe unaandika maeneno rudi juu kapige mahesabu ya zile takwimu walimu wote wakijitolea kila shule itakuwa na walimu sichini ya 200+ je hiki kinawezekana kuwapp hapana ndio maana kutokana Number haingopi walimu kibao washaomba kijitolea shule kibao jibi nk hakuna nafasi ukienda kuomba Leo kuna mwenzio katoka jana kuomba ila yote kwa yote katika maisha yangu siwezi kujitolea ni ujinga ingekuwa kujitolea inakupa mazingira ya kukupa ajira ya uhakika (serikali) hakuna graduate angeacha ila kuomba kujitole mbimde, kupata mbinde, ukipata kulipwa mbinde, ukiwa unalipwa pesa ya ice cream, ukipewa ajira kabisa bado si ya uhakika na ashahara mkangafu.
Numbers inatokana na maneno, Ukijitolea unajitoa Chochote utakacholipwa ni sawa, Katika maisha yangu nimejifunza kitu kimoja nacho ni kuwa "in everything that i do it's not all about money", Na katika hili Mungu amekuwa akinilipa.
 
Numbers inatokana na maneno, Ukijitolea unajitoa Chochote utakacholipwa ni sawa, Katika maisha yangu nimejifunza kitu kimoja nacho ni kuwa "in everything that i do it's not all about money", Na katika hili Mungu amekuwa akinilipa.
Hiyo Quote IPO sahihi ila sio kwenye nyanja ya uwalimu jomba hemu angalia pale juu nimeandika neno “MBINDE” malangapi.
 
Mkuu Mimi ni mwalimu kwa taaluma,ninajua shida iliyopo katika kupata nafasi kwa private schools,enzi zangu wasomi walikuwa wachache lakini nilipomaliza chuo nilitembeza barua za maombi hadi nilichoka,

Acha kabisa kurahisisha unapoongelea changamoto za kupambania maisha

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Mkuu Hongera, inaonekana Badae uliajiriwa, Upo government Au private
 
Mkuu Hongera, inaonekana Badae uliajiriwa, Upo government Au private
Niko government mkuu,kiufupi ogopa sana mtu anayekupa majibu rahisi wakati hoja zako ni ngumu,eti nenda private schools ,kweli private schools zaweza ajiri walimu 140,000+ ,ooh Mara kajitolee,sasa utakula nini huu si uzembe mkubwa.

Mimi baada ya kuzungusha barua enzi hizo nilichoka baadae niligeukia shughuli za ufundi ujenzi kwani kuna ndugu zangu watatu ni mafundi hivyo nikawa kibarua ,nilipiga jobs sana pale Kahama,kibarua kwa siku alikuwa analipwa elfu nane ,ila shughuli zake unalala mdomo wazi,pesa tamu kazi chungu ,acha kabisa

Nawapa pole sana watu wote wanaohangaikia ajira ,maana ni shughuli pevu

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kumbe umewahi piga saidia fundi nawewe, mimi pia kabla sijapata ajira niliwahi jaribu aiseh sio kazi ile mkuu unaweza kufa location, mambo ya kuchimba shimo la choo, mara mchanga wake muujaze kwenye vyumba viwe level, mara upandishe cement mbichi juu kwa kutumia ngaz hahahahaha sio kabisa hapo uliposema unalala mdomo wazi ni kweli na usipoangalia unakuwa mlevi wa kutupwa.
Niko government mkuu,kiufupi ogopa sana mtu anayekupa majibu rahisi wakati hoja zako ni ngumu,eti nenda private schools ,kweli private schools zaweza ajiri walimu 140,000+ ,ooh Mara kajitolee,sasa utakula nini huu si uzembe mkubwa...
 
Mimi nafanya popote tafadhali niunganish japo nmejikita kweny kisw na history nipo Dar
Mkuu naomba nikuhangaikie jumatatu maana upo mbali nikifanikiwa hiyo nafasi nilipokutajia nitakupa namba uongee nao
 
Pia wakuu kwasisi walimu ni vizuri kuomba nafasi hata school za msingi english medium trust ke huwezi kosa na wanalipa laki 3 hadi 4 kuna 2 nazijua zinalipa lako 7 na 8 ni top sana.

Tujitahidi sana kuomba nafasi kwingi confidence ni muhimu na kumtegemea Mungu atufungulie milango maan wengine tulipata kazi kimiujiza moujiza tu
 
Nitapenda kufahamu ili niwe inspired kua student naweza pata na mimi coz nimeona nikaprocess kidg kuandaa ka Cv na kale ka video demo

Are you hard-working or hardly-working?
  1. Asilimia 51 ya walimu nchini, hawafundishi wanafunzi wakati wa saa za kazi.
  2. Walimu wapo wengi, lakini wanaofundisha ni wachache
  3. Walimu kutofundisha wanafunzi madarasani kwa muda uliopangwa na kupokea mishahara, ni sawa na kuwa mfanyakazi hewa anayeiibia fedha serikali.

WAKATI Serikali ikipambana ili wanafunzi wapate mazingira bora ya kujifunzia, kwa kuhakikisha kunakuwa na madawati, maabara, vitabu na sheria ngumu kwa watakaooa au kuwapa ujauzito wanafunzi, utafiti umebaini kuwa asilimia 51 ya walimu nchini ni watoro.

Utafiti huo uliofanywa na wadhibiti ubora wa elimu katika shule mbalimbali, umebaini kuwa asilimia 51 ya walimu nchini, hawafundishi wanafunzi wakati wa saa za kazi.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Juma Kaponda, alisema hayo juzi wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya uwezeshaji wa wawezeshaji wa kamati za shule 528, wanaotoka katika halmashauri 123 za mikoa 19 nchini nzima.

Kwa mujibu wa Kaponda, utafiti huo uliofanyika katika miezi ya hivi karibuni, ulibaini ni asilimia 49 tu ya walimu waliopo kazini wanafundisha na hao asilimia 51 hawafundishi na baadhi yao kama wakifundisha, ni kwa muda tu na kuondoka kwenda kufanya shughuli nyingine.

Kutokana na udhaifu huo, Kaponda amewaagiza maofisa elimu wa mikoa, ofisa taaluma wa mikoa na wenzao wa ngazi hizo katika wilaya, kuanza kufuatilia walimu shuleni kuona kama wanawajibika kufundisha madarasani.

Alisema kitendo cha walimu kutofundisha wanafunzi madarasani kwa muda uliopangwa na kupokea mishahara, ni sawa na kuwa mfanyakazi hewa anayeiibia fedha serikali.

“Walimu wapo wengi, lakini wanaofundisha ni wachache kwa sasa ni lazima sisi viongozi tufanye kazi ya kusimamia maadili ya walimu, ufundishaji na kuhakiki ubora wa kiwango cha taaluma na wale wazembe hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma,” alisema Kaponda.

Kaponda alisema mwalimu asiyefundisha kwa muda mrefu hata kama alikuwa ni mzuri kwa kiwango cha juu, uwezo wake hupungua na kurudisha nyuma kiwango cha taaluma katika shule husika. Katika hatua nyingine, serikali imetoa Sh bilioni 15 kwa ajili ya gharama za Julai za uendeshaji wa shule zote za msingi na sekondari nchini.

Kaponda amesema tayari fedha hizo zimepokewa Tamisemi na taratibu za kuingizwa katika akaunti za shule husika umeshakamilishwa kwa ajili ya matumizi ya uendeshaji wa shule kwa mujibu wa utaratibu uliopo.

Alihadharisha kuwa matumizi ya fedha hizo yafanyike kwa malengo yaliyowekwa na serikali chini ya mwongozo uliotolewa na kwa watakaokwenda kinyume chake, watawajibishwa kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.

Chanzo: HabariLeo

Utoro wa walimu madarasani ni Asilimia 51
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom