Nimesoma Ualimu nimemaliza lakini sina kazi

masanjuo

Senior Member
Oct 10, 2016
184
306
Nimesoma nimemaliza lakini sina kazi kazi ngumu

Naombeni mnisaidie jamani nipo radhi kufanya kazi yoyote nina umri wa miaka 26 nmemaliza shahada ya elimu toka 2017 nmejikita kweny kufundisha history na kiswahili jamani naombeni nisaidie Tafadhali naomben Mimi ninamajukumu nanijikidhi.
 
Anahitajika mwalimu kwa ajili ya kufundisha Ordinary level (form one to form four). Mwalimu anahitajika kuwa na Bachelor Degree of arts with Education (History).

Experience awe na angalau miaka miwili (2 year's) katika kufundisha somo husika (History).

Shule ipo mkoa wa Tanga. Kwa mawasiliano tuma CV yako kwa namba 0622513133 au 0758994103.
 
Asante kesho natuma

Pole mkuu upo wapi? Kutaja location ni muhimu ili kama kuna nafasi karibu upewe......binafsi kuna nafasi Iringa shule ya wasichana tu ni boarding school wanahitaji English language na History ni mwaka wa 3 huu......
Mkuu nipo hapa nimesoma English na history Nina uzoefu wa mwaka mmoja.
 
Nimesoma nimemaliza lakini sina kazi kazi ngumu

Naombeni mnisaidie jamani nipo radhi kufanya kazi yoyote nina umri wa miaka 26 nmemaliza shahada ya elimu toka 2017 nmejikita kweny kufundisha history na kiswahili jamani naombeni nisaidie Tafadhali naomben Mimi ninamajukumu nanijikidhi.
Mwalimu unakosaje kazi? Tafuta shule binafsi kajitolee. Ukipiga kazi watakuzoea na kuanza kukupa pocket money, ukiwa ASSET WATAKUSAJILI FASTA.
 
Mwalimu unakosaje kazi? Tafuta shule binafsi kajitolee. Ukipiga kazi watakuzoea na kuanza kukupa pocket money, ukiwa ASSET WATAKUSAJILI FASTA.
Nyie watu mnaotoa majibu rahisi kwa hoja ngumu mnakela sana, ni bora ukawa msoma.comments tu kuliko kuandika maneno yenye kukera watu kama haya.

Hivi unajua Tanzania,private schools ziko ngapi? Na tangu serikali iache kuajiri walimu ni lini na je kila mwaka kuna wahitimu wangapi wanaletwa mtaani?

Kwa taarifa yako tu private schools kwa tanzaniani ni almost 1000+ kwa primary na secondary,na Mara ya mwisho kwa serikali kufanya mass employment ni mwaka 2015,na kila mwaka wakati wanafanya mass employment kipindi hicho waliajiriwa takribani walimu 40,000+,sasa anza kuhesabu tangu mwaka 2015 hadi Leo ni miaka mingapi na kuna wahitimu wangapi,kwa hesabu ya haraka tu kuna wahitimu almost 140,000+ wa fani ya ualimu

Hivyo ukiwa na shibe ustoe majibu mepesi kwa mwenye njaa ,kukaa kimya napo ni busara.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom