Nimesikitishwa na aina hii ya usajili unaofanywa na Mwenyekiti wangu Freeman Mbowe

Tunachofanya sasa ni kama wanaume wanaovizia wanawake wanaoachwa na waume zao then sisi tunaingia kwa mbwembwe kwa lengo la kutaka kufunganao ndoa. Tunajua wameachwa kwa sababu gani? Tena muogope mwanamke anayeachika kwa mumewe then haraka haraka anakusanya virago vyake na kuhamia kwako. Je wakipatana na mumewe utakuwa katika hali gani? Siri zako zote zitakuwa hadharani.

Nikiri kwa dhati ya moyo kwamba, sijafurahishwa na aina ya usajili unaofanywa na Mwenyekiti wangu Freeman Aikael Mbowe. Dhamira ni njema ila aina ya watu tunaochukua kwa kweli tuna kila sababu ya kujiona hatujitendei haki.

CHADEMA si chama cha kuokoteza wanachama. CHADEMA si chama cha kutegemea mtu anayechukia CCM kwa sababu tu maslahi yake yamepokonywa. CHADEMA si chama zoa zoa. Kilijengwa kwa misingi imara ambayo iliasisiwa na wazee wetu Edwin Mtei na Bob Makani. Ninasikitika kusema kuwa tunawakwaza sana wazee hawa ambao walitumia nguvu kubwa kuweka misingi imara ya chama chetu.

Tulivyomchukua Edward Lowasa tulipewa propaganda kuwa anakuja na wabunge 50 pamoja na wenyeviti wa Mikoa 18 na Wenyeviti wa wilaya wa CCM zaidi ya 100. Hata hivyo, tulichoshuhudia ni kinyume chake. Leo hii tukifanya tathmini ya wanachama tuliowachukua utakuta zaidi ya nusu wamesharejea CCM kiakili na wengine wametangaza hadharani kukihama chama chetu.

Huku mitaani tunachekwa sana kwa sasa. Mwanzo walikuwa wanatuita kichaka cha mafisadi na sasa tumeongezewa ugonjwa mwingine wa kuwa kichaka cha wauza unga na mateja.

Niwasihi sana viongozi wetu. Tanzania hii ina watu wengi ambao wanaweza kuwa potential katika chama chetu. Hapa ndipo CCM wanapotushika. Sisi tunahangaika na Wema Sepetu mmoja ama Edward Lowasa ama Frederick Sumaye ama Laurence Masha ama Milton Makongoro Mahanga ama Kingunge Ngombale Mwiru, wenzetu CCM wanafanya usajili wa maana kwa kutekeleza ilani ya chama chao na kujali maslahi ya wananchi. Wapo busy kutekeleza miradi ya vijijini ambako kuna wapiga kura wengi. Sisi tunang'ang'ana na watu wanaotafuta unafuu wa maisha! Twafwaaaaaaa!
Ametoswa Lowassa na bado CCM ipo!!! Who is Wema!?
 
Kuna watu wana wafuasi makanisa na wamewaambia waumini wao wamchague flani na bado wamemtosa huyo flani. Hizi akili za CDM nashindwa kuzielewa kabisa. Muachane na siasa mgeuze liwe kanisa la watu kufanya toba na kuokolewa
 
Kwa hiyo unataka kutuambia mtu akitaka kujiunga chadema kutoka chama cha Sisiem asipokelewe????? Mi Naona Wema Kaja mwenyewe baada ya kumshinda mambo huko alikotoka, we Ulitaka iweje kuhusu wanachama wapya
 
Kaondoka Lowassa CCM ikanshinda kwa nguvuuu sumaye kingunge sembuse Wema Jamani anae Fanya Ngono na Vitoto vidogo vya kwenye Matangazo ya Voda? Kaachana Wema na Wanaume wangapiii??? Lakini wanaume wote wanawake wao sembuse kuondoka CCM?

Kwanza TRA fanyeni haraka mchunguzeni Kodi analipa? Lipstick zake Ni original au fake TBS fanyeni hivyo......

Jamani wemaaaa? Wakukaa kumuogelea kwenye chama
 
Tunachofanya sasa ni kama wanaume wanaovizia wanawake wanaoachwa na waume zao then sisi tunaingia kwa mbwembwe kwa lengo la kutaka kufunganao ndoa. Tunajua wameachwa kwa sababu gani? Tena muogope mwanamke anayeachika kwa mumewe then haraka haraka anakusanya virago vyake na kuhamia kwako. Je wakipatana na mumewe utakuwa katika hali gani? Siri zako zote zitakuwa hadharani.

Nikiri kwa dhati ya moyo kwamba, sijafurahishwa na aina ya usajili unaofanywa na Mwenyekiti wangu Freeman Aikael Mbowe. Dhamira ni njema ila aina ya watu tunaochukua kwa kweli tuna kila sababu ya kujiona hatujitendei haki.

CHADEMA si chama cha kuokoteza wanachama. CHADEMA si chama cha kutegemea mtu anayechukia CCM kwa sababu tu maslahi yake yamepokonywa. CHADEMA si chama zoa zoa. Kilijengwa kwa misingi imara ambayo iliasisiwa na wazee wetu Edwin Mtei na Bob Makani. Ninasikitika kusema kuwa tunawakwaza sana wazee hawa ambao walitumia nguvu kubwa kuweka misingi imara ya chama chetu.

Tulivyomchukua Edward Lowasa tulipewa propaganda kuwa anakuja na wabunge 50 pamoja na wenyeviti wa Mikoa 18 na Wenyeviti wa wilaya wa CCM zaidi ya 100. Hata hivyo, tulichoshuhudia ni kinyume chake. Leo hii tukifanya tathmini ya wanachama tuliowachukua utakuta zaidi ya nusu wamesharejea CCM kiakili na wengine wametangaza hadharani kukihama chama chetu.

Huku mitaani tunachekwa sana kwa sasa. Mwanzo walikuwa wanatuita kichaka cha mafisadi na sasa tumeongezewa ugonjwa mwingine wa kuwa kichaka cha wauza unga na mateja.

Niwasihi sana viongozi wetu. Tanzania hii ina watu wengi ambao wanaweza kuwa potential katika chama chetu. Hapa ndipo CCM wanapotushika. Sisi tunahangaika na Wema Sepetu mmoja ama Edward Lowasa ama Frederick Sumaye ama Laurence Masha ama Milton Makongoro Mahanga ama Kingunge Ngombale Mwiru, wenzetu CCM wanafanya usajili wa maana kwa kutekeleza ilani ya chama chao na kujali maslahi ya wananchi. Wapo busy kutekeleza miradi ya vijijini ambako kuna wapiga kura wengi. Sisi tunang'ang'ana na watu wanaotafuta unafuu wa maisha! Twafwaaaaaaa!
Ndo mwisho wa chama unakaribia
 
Siku zote nipo CHADEMA
kinakuzuia nini kuhama ukaenda nawe kutekeleza ilani vijijini mi nafikiri mtu mpuuz hung'ang'ana kukaa sehemu anayoona iko mrama ila kwastayle unayoenda nayo umejifunza kwetu jaribu siku nyingine kuposti negative ili hata wajinga wasistuke kama afanyavyo mzee tupa tupa wa hapo lumumba
 
Wameshamlipa pesa

Watu nimegundua sio makin kwenye kutafakar maongez ya watu, hapa mkakati sio kupiga hela kutoka chadema , ulikua ni mkakati wa kuwawasha ccm watoe hela watakapoambiwa wema anahamia chadema. Sasa hapo chadema wametoa hela gani???
 
Nitasikitika tu kama wamemlipa pesa ila kuja chadema haina tatizo chadema ni chama cha wote na wanachama ndiyo mtaji. Nani ajuaye kuwa kwenye kura milioni 6 walizopata ukawa hazikuwepo za wauza unga, mateja na wavuta bangi, wezi na majambazi? Chama hakikatai mwanachama hakuna chama hicho vyama vyote vinamchanganyiko wa watu. Assume wewe ni katibu kata wa chama akaja mtu kufuata kadi utamnyima kwa sababu ya tabia huo utakuwa ni ubaguzi na chama cha kibaguzi hakitakiwi
 
You guys you should understand one thing, but this is my principle, "As a proffesional, I never deal with cheap people in serious issues"

That is my rule # 1.
Cheap people will never stop suprising you. This Steve's things (call conversations) are bullshit...

Rule # 2, Nimeshajifunza mda sana, na hii nilipata kutoka kwa rafik zangu waonfanya kazi za upelelezi, "Never have a serious n damaging conversation through phones", If u have serious conversion, meets that person, and if it is more serious no phones are allowed into the conversion room.

But in rule # 1 is the most important one, never deal with cheap people in very serious issues.
 
Back
Top Bottom