Nimesikitishwa na aina hii ya usajili unaofanywa na Mwenyekiti wangu Freeman Mbowe

Kada wa CHADEMA

JF-Expert Member
Feb 27, 2016
289
615
Tunachofanya sasa ni kama wanaume wanaovizia wanawake wanaoachwa na waume zao then sisi tunaingia kwa mbwembwe kwa lengo la kutaka kufunganao ndoa. Tunajua wameachwa kwa sababu gani? Tena muogope mwanamke anayeachika kwa mumewe then haraka haraka anakusanya virago vyake na kuhamia kwako. Je wakipatana na mumewe utakuwa katika hali gani? Siri zako zote zitakuwa hadharani.

Nikiri kwa dhati ya moyo kwamba, sijafurahishwa na aina ya usajili unaofanywa na Mwenyekiti wangu Freeman Aikael Mbowe. Dhamira ni njema ila aina ya watu tunaochukua kwa kweli tuna kila sababu ya kujiona hatujitendei haki.

CHADEMA si chama cha kuokoteza wanachama. CHADEMA si chama cha kutegemea mtu anayechukia CCM kwa sababu tu maslahi yake yamepokonywa. CHADEMA si chama zoa zoa. Kilijengwa kwa misingi imara ambayo iliasisiwa na wazee wetu Edwin Mtei na Bob Makani. Ninasikitika kusema kuwa tunawakwaza sana wazee hawa ambao walitumia nguvu kubwa kuweka misingi imara ya chama chetu.

Tulivyomchukua Edward Lowasa tulipewa propaganda kuwa anakuja na wabunge 50 pamoja na wenyeviti wa Mikoa 18 na Wenyeviti wa wilaya wa CCM zaidi ya 100. Hata hivyo, tulichoshuhudia ni kinyume chake. Leo hii tukifanya tathmini ya wanachama tuliowachukua utakuta zaidi ya nusu wamesharejea CCM kiakili na wengine wametangaza hadharani kukihama chama chetu.

Huku mitaani tunachekwa sana kwa sasa. Mwanzo walikuwa wanatuita kichaka cha mafisadi na sasa tumeongezewa ugonjwa mwingine wa kuwa kichaka cha wauza unga na mateja.

Niwasihi sana viongozi wetu. Tanzania hii ina watu wengi ambao wanaweza kuwa potential katika chama chetu. Hapa ndipo CCM wanapotushika. Sisi tunahangaika na Wema Sepetu mmoja ama Edward Lowasa ama Frederick Sumaye ama Laurence Masha ama Milton Makongoro Mahanga ama Kingunge Ngombale Mwiru, wenzetu CCM wanafanya usajili wa maana kwa kutekeleza ilani ya chama chao na kujali maslahi ya wananchi. Wapo busy kutekeleza miradi ya vijijini ambako kuna wapiga kura wengi. Sisi tunang'ang'ana na watu wanaotafuta unafuu wa maisha! Twafwaaaaaaa!
 
We sio kada wa chadema.

Nimepitia post zako zoteeee kwenye profile yako. Wewe ni kuponda tu Chadema mwanzo mwisho. Hamna hata a single post you are neutral.

Ni kijana wa lumumba anayetumia jina la Kada Wa Chadema kama a tool of propaganda lakin umeferiii sanaa. Profile yako imekuumbua.
 
Dhambi ya kumtukana na kumuita Slaa kuwa ni Dr Mihogo itawaandama milele chadema.
Wachawi, mafisadi, wauza madawa ya kulevya, wahujumu uchumi wote watajiunga Chadema.
Hawa wachawi, mafisadi, wauza madawa ya kulevya na wahujumu uchumi wanaokimbilia Chadema wametokea mbinguni???Si mlikuwa nao hapo Lumumba, je walikuwa wasafi walipokuwa Lumumba na wamekuja kuchafukia Chadema? Hakuna mzigo mkubwa zaidi ya kuwa mwanaccm aisee!
 
Siasa ni mbinu na mkakati... wewe mtoa mada unawafuasi wangapi instagram, facebook ukijilinganisha na Wema Sepetu ...
Ina maana Atanzania tumekuwa wapumbavu hivyo kiasi cha kumfuata Wema Sepetu kwenye itikadi zake za kisiasa? Hili siamini hata kidogo. Wema ana mashabiki wengi na wapo cut across. Wapo CCM, wapo UKAWA na wapo hata TLP. Wanachompendea wema si itikadi zake za kisiasa.
 
Ina maana Atanzania tumekuwa wapumbavu hivyo kiasi cha kumfuata Wema Sepetu kwenye itikadi zake za kisiasa? Hili siamini hata kidogo. Wema ana mashabiki wengi na wapo cut across. Wapo CCM, wapo UKAWA na wapo hata TLP. Wanachompendea wema si itikadi zake za kisiasa.
Wasanii wanamchango mkubwa sana kwa siasa za kiafrika... Jiulize CCM walitumia kiasi gani kuwalipa wasanii kipindi cha kampeni? Kwanini?
 
Back
Top Bottom