Nimesikitishwa na aina hii ya usajili unaofanywa na Mwenyekiti wangu Freeman Mbowe

Ila inabidi tufikirie jamn hawa mama zenu mbna kama wanakauli ambazo hazipendezi hata kwenye jamii
 
Tunachofanya sasa ni kama wanaume wanaovizia wanawake wanaoachwa na waume zao then sisi tunaingia kwa mbwembwe kwa lengo la kutaka kufunganao ndoa. Tunajua wameachwa kwa sababu gani? Tena muogope mwanamke anayeachika kwa mumewe then haraka haraka anakusanya virago vyake na kuhamia kwako. Je wakipatana na mumewe utakuwa katika hali gani? Siri zako zote zitakuwa hadharani.

Nikiri kwa dhati ya moyo kwamba, sijafurahishwa na aina ya usajili unaofanywa na Mwenyekiti wangu Freeman Aikael Mbowe. Dhamira ni njema ila aina ya watu tunaochukua kwa kweli tuna kila sababu ya kujiona hatujitendei haki.

CHADEMA si chama cha kuokoteza wanachama. CHADEMA si chama cha kutegemea mtu anayechukia CCM kwa sababu tu maslahi yake yamepokonywa. CHADEMA si chama zoa zoa. Kilijengwa kwa misingi imara ambayo iliasisiwa na wazee wetu Edwin Mtei na Bob Makani. Ninasikitika kusema kuwa tunawakwaza sana wazee hawa ambao walitumia nguvu kubwa kuweka misingi imara ya chama chetu.

Tulivyomchukua Edward Lowasa tulipewa propaganda kuwa anakuja na wabunge 50 pamoja na wenyeviti wa Mikoa 18 na Wenyeviti wa wilaya wa CCM zaidi ya 100. Hata hivyo, tulichoshuhudia ni kinyume chake. Leo hii tukifanya tathmini ya wanachama tuliowachukua utakuta zaidi ya nusu wamesharejea CCM kiakili na wengine wametangaza hadharani kukihama chama chetu.

Huku mitaani tunachekwa sana kwa sasa. Mwanzo walikuwa wanatuita kichaka cha mafisadi na sasa tumeongezewa ugonjwa mwingine wa kuwa kichaka cha wauza unga na mateja.

Niwasihi sana viongozi wetu. Tanzania hii ina watu wengi ambao wanaweza kuwa potential katika chama chetu. Hapa ndipo CCM wanapotushika. Sisi tunahangaika na Wema Sepetu mmoja ama Edward Lowasa ama Frederick Sumaye ama Laurence Masha ama Milton Makongoro Mahanga ama Kingunge Ngombale Mwiru, wenzetu CCM wanafanya usajili wa maana kwa kutekeleza ilani ya chama chao na kujali maslahi ya wananchi. Wapo busy kutekeleza miradi ya vijijini ambako kuna wapiga kura wengi. Sisi tunang'ang'ana na watu wanaotafuta unafuu wa maisha! Twafwaaaaaaa!
Nenda ukawe kada wa Mashoga....stupid
 
Madudu yanayotokea sasa kwa serikali hii yalitakiwa kuifanya chadema iwe imara zaidi bahati mbaya imekua mbovu zaidi
 
Tupe mfano wa usajili uliofanywa na ccm,ambao unatisha hao uliowaona hamna kitu
 
Dhambi ya kumtukana na kumuita Slaa kuwa ni Dr Mihogo itawaandama milele chadema.
Wachawi, mafisadi, wauza madawa ya kulevya, wahujumu uchumi wote watajiunga Chadema.
Unajua unafiki nao sio mzuri mtoa mada sija muelewa unajifanya m/kiti wako halafu unawananga watu wengine kama m/kiti wako kwa nn usimfuate umpe huo ushauri au umetumwa
 
Chadema ni genge la wahuni na wapigaji, tunakoelekea na akina Chid mapenzi , Chid Benzi & co wote watakua lulu ya chadema.
 
Pale FC buku 7 anapojifanya ni mwana CHADEMA na kushusha porojo jamvini,
Umefeli mleta mada
 
Chadema sijawahi kusikia kuwa Viongozi wa Kitaifa wamekwenda kumuona Slaa na kumtembelea nyumbani kwake, subili aumwe au apate shida yeyote utawaona mbio mbio watajisomba bila aibu huku wakitoa maneno ya kinafiki. Sasa Wema Sepetu amepatwa na kesi , basi wako mbio mbio, wanajifanya wanahuruma sana nakwamba wanajali haki nakwamba ni watetezi na wapigania haki. Kumbe kwa Wema wanalenga kitu, wakishakipata tayari na kukitumia, watampotezea kama Dr. ASlaa ambaye alikitumikia chama kwa uaminifu mkubwa na kwa uvumilivu na kwa shida na raha. Leo hii hata salamu imekuwa shida, utawaona haooo na Mrembo Wema Sepetu. Oh...Mungu Chadema Tuokoe.
 
Tunachofanya sasa ni kama wanaume wanaovizia wanawake wanaoachwa na waume zao then sisi tunaingia kwa mbwembwe kwa lengo la kutaka kufunganao ndoa. Tunajua wameachwa kwa sababu gani? Tena muogope mwanamke anayeachika kwa mumewe then haraka haraka anakusanya virago vyake na kuhamia kwako. Je wakipatana na mumewe utakuwa katika hali gani? Siri zako zote zitakuwa hadharani.

Nikiri kwa dhati ya moyo kwamba, sijafurahishwa na aina ya usajili unaofanywa na Mwenyekiti wangu Freeman Aikael Mbowe. Dhamira ni njema ila aina ya watu tunaochukua kwa kweli tuna kila sababu ya kujiona hatujitendei haki.

CHADEMA si chama cha kuokoteza wanachama. CHADEMA si chama cha kutegemea mtu anayechukia CCM kwa sababu tu maslahi yake yamepokonywa. CHADEMA si chama zoa zoa. Kilijengwa kwa misingi imara ambayo iliasisiwa na wazee wetu Edwin Mtei na Bob Makani. Ninasikitika kusema kuwa tunawakwaza sana wazee hawa ambao walitumia nguvu kubwa kuweka misingi imara ya chama chetu.

Tulivyomchukua Edward Lowasa tulipewa propaganda kuwa anakuja na wabunge 50 pamoja na wenyeviti wa Mikoa 18 na Wenyeviti wa wilaya wa CCM zaidi ya 100. Hata hivyo, tulichoshuhudia ni kinyume chake. Leo hii tukifanya tathmini ya wanachama tuliowachukua utakuta zaidi ya nusu wamesharejea CCM kiakili na wengine wametangaza hadharani kukihama chama chetu.

Huku mitaani tunachekwa sana kwa sasa. Mwanzo walikuwa wanatuita kichaka cha mafisadi na sasa tumeongezewa ugonjwa mwingine wa kuwa kichaka cha wauza unga na mateja.

Niwasihi sana viongozi wetu. Tanzania hii ina watu wengi ambao wanaweza kuwa potential katika chama chetu. Hapa ndipo CCM wanapotushika. Sisi tunahangaika na Wema Sepetu mmoja ama Edward Lowasa ama Frederick Sumaye ama Laurence Masha ama Milton Makongoro Mahanga ama Kingunge Ngombale Mwiru, wenzetu CCM wanafanya usajili wa maana kwa kutekeleza ilani ya chama chao na kujali maslahi ya wananchi. Wapo busy kutekeleza miradi ya vijijini ambako kuna wapiga kura wengi. Sisi tunang'ang'ana na watu wanaotafuta unafuu wa maisha! Twafwaaaaaaa!

SITAKI HATA KUSOMA THREAD YAKO BORA UCHAGUE JIWE KULIKO CCM. KUCHAGUA CCM NI SAWA NA KUITA MAUTI NJOO UNICHUKUE
 
We sio kada wa chadema.

Nimepitia post zako zoteeee kwenye profile yako. Wewe ni kuponda tu Chadema mwanzo mwisho. Hamna hata a single post you are neutral.

Ni kijana wa lumumba anayetumia jina la Kada Wa Chadema kama a tool of propaganda lakin umeferiii sanaa. Profile yako imekuumbua.
Kwahiyo angekuwa kada wa chadema ingekuwa sawa?
 
Hawa wachawi, mafisadi, wauza madawa ya kulevya na wahujumu uchumi wanaokimbilia Chadema wametokea mbinguni???Si mlikuwa nao hapo Lumumba, je walikuwa wasafi walipokuwa Lumumba na wamekuja kuchafukia Chadema? Hakuna mzigo mkubwa zaidi ya kuwa mwanaccm aisee!
Sasa kuna tofauti gani kati ya ccm na chadema kwa ufisadi? Wanahama huku wanaenda kule and viceversa.
 
Back
Top Bottom