Nimeshindwa namna ya kumshauri...

mwambie mkeo aongee na mdogo wake,kipi wifi yake anakikosa kwake?? wanawake sisi ni baadhi yetu tu ndio huwa tunachiti wengi ni wavumilivu ndoani,LOL...we always want to feel SEXY,LOVED AND WANTED...hii ni CONSTANTLY ..sasa kuna kitu kinamiss hapo...mwambie mkeo aongee na mdogo wake..LOL
You are right, wanawake mpaka ukute anacheat basi huyo sijui ni amezibuka au ni kitu gani, tuna kamshipa flani hivi ka aibu au nafsi inakushtaki

Cha msingi, azungumze na wifi yake kwa lugha ambayo ni positive, halafu majibu ya wifi yatampa maamuzi ya either kumshirikisha mdogo wake au la
 
Yaani mtu achepuke halafu uende kuuliza upamde wa pili kuwa umepungukiwa na nini? Kweli kabisa? Aisee hapana. Issue adeal na mchepukaji tu. Hii ni kuhamisha tatizo kwa asiyehusika!

Mkuu hapo nime assume,kila siku wanaotoka nje wanasukumwa na kukosa kwa vitu fulani ndani ya ndoa,sasa kutumia approach nyingine hakutaleta matokeo chanya....
 
Mkuu hapo nime assume,kila siku wanaotoka nje wanasukumwa na kukosa kwa vitu fulani ndani ya ndoa,sasa kutumia approach nyingine hakutaleta matokeo chanya....
Hahahaa kwanini isiwe wamevutiwa na kitu gani huko nje uassume wamesukumwa na kutoka nje? Namaanisha pull and push factors hapa!
 
Kuna msg imeingia kwenye simu ya mke wangu ikitoka kwa wifi yake (mke wa mdogo wake) . Clearly ni ya mapenzi akisema wataonana na bla bla zingine; na leo kweli ameamka anasafiri kwenda mjini??.. Msg ilikuja kwa bahati mbaya maana alikuwa anaongea na mke wangu muda huo huo, hivyo alituma kwa namba ya mke wangu instead ya mwanaume.

Tatizo: Mke wangu anataka kuiforward kwa mdogo wake. Nimekataa maana itavunja ndoa. Mke wangu anasema atakuja kuwaulia ndugu yao kwa ukimwi maana it seems siyo mwaminifu! Nimemwambia anipe muda nitafakari how to handle this situation. Concern ya mke wangu ni ndugu yao kupata magonjwa hasa Ukimwi....

Nimpe ushauri gani?
umekumbuka kufuta hiyo sms
 
Inaelekea mke wako na wifi yake wanaelewa vizuri. Ikiwezekana akae chini na wifi yake amueleze tatizo linalomfanya akose uaminifu katika ndoa. Si ajabu huyu wifi ana mzigo mkubwa moyoni hana pa kuutua. Haridhishwi kitandani, matatizo ya pesa na kadhalika.
 
mwambie mkeo aongee na mdogo wake,kipi wifi yake anakikosa kwake?? wanawake sisi ni baadhi yetu tu ndio huwa tunachiti wengi ni wavumilivu ndoani,LOL...we always want to feel SEXY,LOVED AND WANTED...hii ni CONSTANTLY ..sasa kuna kitu kinamiss hapo...mwambie mkeo aongee na mdogo wake..LOL
Bahati mbaya huwezi kuwa na kila kitu maishani. Ni wachache waliobahatika kuwa na hivyo vyote, ni kuvumilia tu otherwise ni njia ya kujustify uzinzi. Na wanaume tutasema mke wangu wakati ninamuoa alikuwa hivi alikuwa vile sasa siyo tena tuna cheat.
 
Kuna msg imeingia kwenye simu ya mke wangu ikitoka kwa wifi yake (mke wa mdogo wake) . Clearly ni ya mapenzi akisema wataonana na bla bla zingine; na leo kweli ameamka anasafiri kwenda mjini??.. Msg ilikuja kwa bahati mbaya maana alikuwa anaongea na mke wangu muda huo huo, hivyo alituma kwa namba ya mke wangu instead ya mwanaume.

Tatizo: Mke wangu anataka kuiforward kwa mdogo wake. Nimekataa maana itavunja ndoa. Mke wangu anasema atakuja kuwaulia ndugu yao kwa ukimwi maana it seems siyo mwaminifu! Nimemwambia anipe muda nitafakari how to handle this situation. Concern ya mke wangu ni ndugu yao kupata magonjwa hasa Ukimwi....

Nimpe ushauri gani?
Bora ndoa ivunjike kuliko mwanaume mwenzako unamuona anameza ARV's kwa kitu ambacho ungeweza kukizuia.

Au utafurahi kweli kumuona jamaa analea mtoto asiye wake .

Ni kwamba tabia ya umalaya haikanywi kwa maneno pekee , ukilijua hilo utakuwa unafanya maamuzi yenye busara .

Leo unamkanya kwa upole ukidhani akiitiwa dinner nzuri na akaahidiwa hela kidogo , ili aende kwa jamaa atakataa? Kikubwa tu atafanya kwa siri sanaaa.
 
Kwa mtazamo wangu, Ikiwezekana mkeo ampigie simu wifi yake kwa upole kabisa na busara kwamba kwa bahati mbaya ile sms aliyokua anatuma sehemu nyingine imekuja kwake na amuombe tu anachofanya sio kizuri Kama mwanamke mwenzake, angeweza kumwambia mumewe lakini hajapenda kufanya hivyo akiamini kwamba ilo litaharibu ndoa yao hivyo ameamua kumwambia mwenyewe ili abadilike na haache hayo mambo Kama ataamua kuendelea na kuto badilika basi itabidi aseme.
Nadhani ilo litamtesa kwa kumpa hukumu ndani ya nafsi yake kwa mstaarabu ataomba msamaha ila kwa aliye vurugwa ataonekana tu kwa mwitikio wake na apo Sasa anaweza enda kumwambia ndugu yake.

Kama ulikuwa kwenye akili yangu....fact fata ushauri huu
 
Asante. Mke wangu ali propose hiyo njia nikasema inaweza ikaleta confrontation kati yao maana alikasirika sana ! Fine ngoja apoe kwanza aweze kumwambia kwa upole as you proposed. Ngoja tulitafakari

Fanya hivyo kaka ushauri mzuri huu hata ivyo usikose kutupa mrejesho kaka
 
Bora ndoa ivunjike kuliko mwanaume mwenzako unamuona anameza ARV's kwa kitu ambacho ungeweza kukizuia.

Au utafurahi kweli kumuona jamaa analea mtoto asiye wake .

Ni kwamba tabia ya umalaya haikanywi kwa maneno pekee , ukilijua hilo utakuwa unafanya maamuzi yenye busara .

Leo unamkanya kwa upole ukidhani akiitiwa dinner nzuri na akaahidiwa hela kidogo , ili aende kwa jamaa atakataa? Kikubwa tu atafanya kwa siri sanaaa.
Well said! Kwetu kuna methali isemayo "anayetembea na mke wako/mume huwezi kujua kama kaacha mpaka umfukie kaburini". Meaning kuwa mtu akishapenda hawezi kuacha katu, labda afe!
 
Je una uhakika kaka yake hajawahi kukamatwa na msg yoyote na mkewe?
Hiyo ni issue nyingine sasa mkuu, ila wao wanawajibika kufanya hivyo. Haya mambo tunayalea lea kijinga sana. Bora nusu shari kuliko shari kamili. Wakiweza kumkabili binti na kukawa na response ya mabadiliko sawa, vinginevyo wamweke mume wazi tu
 
Mambo mengine hupaswi kuyafuata hivyo,uongo unaruhusiwa katika mazingira kama haya,waongee na binti response yake ndiyo iwe hukumu yake,messeji isifutwe kama ushaidi na awekwe wazi kuwa haifutwi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom