Nimeshindwa: Kwenu wataalam, hii inaitwaje?

Nimeshindwa: Kwenu wataalam, hii inaitwaje?

Mara nyingi hutokea unaweza kuyapanga majengo katika mtazamo fulani na siku ukifika unakuta yapo hivyo asilimia fulani
 
Ishawai kunitokea ndotoni napita maeneo flani naendesha chombo spidi mara ghafla wanakatiza wamama wawili basi yule wa mwisho nikamgonga. Asubuhi yake wakati nakatiza maeneo yale ikanilazimu kuendesha polepole basi ikitokea kama vile nilivyoota lakini kwa kuwa nilikuwa na tahadhari wale wamama waliweza kuvuka salama na mimi nikiendelea na safari salama. Ila niliwaza Sana siku hiyo
 
Sakayo
Wakati nipo nyumbani kusubiri matokeo ya Kidato cha Nne, niliwahi kuota ndoto kuwa nimefaulu kwa point 1 zaidi ya ufaulu aliopata rafiki yangu niliyekuwa naishi naye lakini alinitangulia mwaka mmoja.
Baada ya matokeo ni kweli ilikuwa hivyo(Huwezi kuamini).

Kabla ya machaguo ya kujiunga na kidato cha 5, niliota nasafiri kwenda masomoni ukanda fulani ambao kabla sijawahi kufika. Nilipuuza ndoto ile kwani nilichaguliwa kwenda kusoma ukanda tofauti kabisa. Miezi 9 baadaye, lilitokea tukio ambalo lilifanya nihame shule na nilikohamia ni kule nilikoota ndoto kuwa naenda kusoma. Nilikuja kukumbuka baada ya kuwa tayari akili imetulia na naendelea na masomo.

Yapo mengi, tena mengi tu. Hayo ndiyo nimeona niwashirikishe leo
Naona kama tunafanana kabisaa!
Kuna maisha nayaishi nilishayaota kabisaa, leo Nimeongea na mtu ambaye nilishaongea naye siku nyingi saaana ndotoni na tukaongea kitu kile kile sema nimekuja kukumbuka baada ya kumaliza mazungumzo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nguzo za Dunia hii zina siri nyingi sana kwenye ulimwengu wa roho!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maombi ni muhimu kabla ya kulala ili kuzuia zisiwe zinaenda kuzurula,maana zisiporudi kwakweli itakuwa ni hatari sana.Nadhani hii ndio sababu mnaamka asubuhi unakuta mtu amekufa bila hata ya kuumwa,kumbe roho yake ilienda kuzurula ikapotea njia au ikapata ajali au ikapata mchepuko ikamuacha jamaa hana kitu.......
hakika mkuu
mpaka tuje kufahamu usiri wa dunia hii tuna safari ndefu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa inanitokea, naota nimekaa sahemu Fulani na watu Fulani, tunspiga story, na mpangilio wa watu.

Alafu baada ya muda Fulani inatokea precisely the same.

Mara nyingine hata nikifikiria Jambo huwa linatokea vile vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
si mchezo
nyie ndio wale ambao mna kipaji cha kuhisi jambo litatokea na likatokea pia mabingwa wa meditiation
vipi umezaliwa mwez April?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishawai kunitokea ndotoni napita maeneo flani naendesha chombo spidi mara ghafla wanakatiza wamama wawili basi yule wa mwisho nikamgonga. Asubuhi yake wakati nakatiza maeneo yale ikanilazimu kuendesha polepole basi ikitokea kama vile nilivyoota lakini kwa kuwa nilikuwa na tahadhari wale wamama waliweza kuvuka salama na mimi nikiendelea na safari salama. Ila niliwaza Sana siku hiyo
teh
tupo kwenye usiri wa mambo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom