Nimeshangazwa na kukuta mabati yamepanda bei

Ukweli ni kwamba kuna mfumuko wa bei mkubwa kuanzia 10% kwenda juu ndani ya miezi minane.

Chakula, mbolea, ujenzi vitu vyote.

Bei ya mazao mishahara haijaongezeka sambamba hivi vitu.

Hayo ni matokea ya kutunga sera zisizo na uhalisia. Utaua biashara nyingi sana kwa style hii.

Pia ongezeko la mshahara halina maana, wanakupa 3% wanachukua 30%.

Ni bora uthibiti inflation (upandaji wa bei wa vitu vyote).

Kiwe kipaumbele Serikai BOT, Wizara ya fedha.

Hizo kodi, tozo mwisho wa siku hazitaweza kulipwa. Bia utaua wengi kwa sera kama hizi indirectly.
Hi ni wake up call ndhani tunaelekea kubaya zaidi tusiposhtuka mapema, nondo ya mm 12 ilikua 20k lakni leo ni 25-27k ndani ya muda mfupi sana
 
Nimesoma report kutoka mwananchi, kumbe shida inaanzia china, nao wana miradi mikubwa kiasi kwamba export ya materia ya chuma imepunguzwa, kwa hiyo tujipange siku ngumu zinakuja mbeleni dont expect hizi price zishuke paap!
 
Vipi kuhusu mafuta, mbolea, vifurushi, chakula. Wachina nao wanahusika?
 
Inaweza kuwa sababu pia!
 
Nimesoma report kutoka mwananchi, kumbe shida inaanzia china, nao wana miradi mikubwa kiasi kwamba export ya materia ya chuma imepunguzwa, kwa hiyo tujipange siku ngumu zinakuja mbeleni dont expect hizi price zishuke paap!

Hiyo inaweza kuwa factor moja, sio kigezo kikubwa kivile Vifaa vya ujenzi viko vingi, cement, tiles, vigae, gypsum, mabati, mabomba, vifaa vya umeme nk.

Vyote vimeongezeka bei hadi kokoto,mchanga, Fikiria.
 
Vipi kuhusu mafuta, mbolea, vifurushi, chakula. Wachina nao wanahusika?
Yote ni mfumuko wa bei, huwezi ku control mfumuko wa bei kiurahisi kwa sababu mnyororo unaosababisha kutokea mfumuko wa bei ni mkubwa sana unahusisha sector nyingi sana ndani na nje ya nchi

Nikupe mfano, nchi nyingi zilikuwa zimejuifungia hamna uzalishaji wa kutosha kuanzia kwenye, mazao, uchimbaji madini kama chuma na aluminium, mafuta, viwanda n.k now wanajifungulia unadhani hali itakuwaje?
 
Hiyo inaweza kuwa factor moja, sio kigezo kikubwa kivile Vifaa vya ujenzi viko vingi, cement, tiles, vigae, gypsum, mabati, mabomba, vifaa vya umeme nk.

Vyote vimeongezeka bei hadi kokoto,mchanga, Fikiria.
Kumbuka vitu vyote kwa asilimia zaidi ya 80 tunaagiza kwenye nchi zilizokuwa zimejifungia tangu kuanza kwa covid 19...chekecha ubongo
 
Yote ni mfumuko wa bei, huwezi ku control mfumuko wa bei kiurahisi kwa sababu mnyororo unaosababisha kutokea mfumuko wa bei ni mkubwa sana unahusisha sector nyingi sana ndani na nje ya nchi

Nikupe mfano, nchi nyingi zilikuwa zimejuifungia hamna uzalishaji wa kutosha kuanzia kwenye, mazao, uchimbaji madini kama chuma na aluminium, mafuta, viwanda n.k now wanajifungulia unadhani hali itakuwaje?

Unaweza na kwa kiasi kikubwa na siku zote ujaribu kufanya hivyo, you need elastic system. Vitu vikipanda unaweka subsidies or kupunguza kodi kwa muda fulani, vikipungua unaongeza kodi.

Vitu kama mazao tunayoyazalisha wenyewe kuna sababu za msingi kupanda bei zaidi ya bei za mbolea na vifaa vingine vya uzalishalii kuongezwa
 
Kumbuka vitu vyote kwa asilimia zaidi ya 80 tunaagiza kwenye nchi zilizokuwa zimejifungia tangu kuanza kwa covid 19...chekecha ubongo

Sio vyote. Vyakula tunazalisha, cement kwa kiasi kikubwa tunazalisha hata mabati tunayo ya kwetu, mchanga, kokoto tunachimba.

Justification gani zipo za kuongeza bei maradufu kwa kila kitu?

Sera rafiki kwa wakati mgumu zingesaidia.
 
Inaweza kushuka mkuu ila sidhani kama ni hivi karibuni! Ngoja tusubirie tu
muda unasubiri bei ishuke mara mtoto anaumwa mara michango ya harusi basi niweke benki au ktk simu mara tozo mara makato ya mwezi tunapigwa kotekote mkuu.
 
Yote ni mfumuko wa bei, huwezi ku control mfumuko wa bei kiurahisi kwa sababu mnyororo unaosababisha kutokea mfumuko wa bei ni mkubwa sana unahusisha sector nyingi sana ndani na nje ya nchi

Nikupe mfano, nchi nyingi zilikuwa zimejuifungia hamna uzalishaji wa kutosha kuanzia kwenye, mazao, uchimbaji madini kama chuma na aluminium, mafuta, viwanda n.k now wanajifungulia unadhani hali itakuwaje?

Nchi zote zinazojitambua duniani huwalinda wananchi wao, hadi kuwalipa mishahara yao kukaa nyumbani.

Walichukua mikopo, asilimilia kubwa ilielekezwa kupunguza makali.

Sisi tumefanya kinyume chake.
 
muda unasubiri bei ishuke mara mtoto anaumwa mara michango ya harusi basi niweke benki au ktk simu mara tozo mara makato ya mwezi tunapigwa kotekote mkuu.

Ni hivi hii serikali haina au haijali kuwa na sera rafiki kwa Mtanzania wa kawaida.

Unaongeza bei za mbolea, pembejeo muhimu, bei za chakula zitapanda bei. Unaongeza kodi kwenye mafuta kila kitu kitapanda, tozo za vifurushi unaua sekta ýa mitandao, mawasiiano inayowaajiri vijana wengi.

Kivipi unashangaa kuna mfumuko wa bei?
 
Nchi zote zinazojitambua duniani huwalinda wananchi wao, hadi kuwalipa mishahara yao kukaa nyumbani.

Walichukua mikopo, asilimilia kubwa ilielekezwa kupunguza makali.

Sisi tumefanya kinyume chake.
Ha ha kwa hiyo ukichanbua Tanzania kwa uwezo wake ukikuwa unategemea upokee kila mwezi laki 6 ya kijikimu?unaongelea nchi ambazo zina mfumo wa miaka 400 au 200 kabla hamjaanza kuunda nchi yenu, acha kulia lia, njoo kwenye reality
 
Ulikuwa mfano kukuelewesha. Nafikiri umeelewa
 
Back
Top Bottom