Nimeshandaa vipindi cha radio kadhaa ila sina fedha za kulipia kurusha kipindi hicho!

Oct 29, 2015
59
31
Kuna kipindi cha TV nahitaji kuanzisha, nimeshaandaa video kadhaa, lakini shida inayonikabili ni uhaba wa fedha ili kurusha vipindi hivyo.

Kwa kuzingatia kauli hii MTU NI WATU, NA WATU NI MTU, Ninakuja katika jukwaa hili, kwa kuwa hapa kuna mkusanyiko wa watu wenye kariba tofauti tofauti, naamini mahali hapa ninaweza kupata japo msaada wa kimawazo, ambayo yatakuwa msaada mkubwa katika kufanikisha azima yangu hii.

Kutokana na jukwaa hili kuwa na nafasi finyu kwa video ya kuambatanisha, ninaambatanisha link ya youtube kwa video moja, ambalo ni kama tangazo, ili kutoa japo mwanga kwa jambo hili ninalolita mbele yenu.


Natanguliza shukrani zangu, na mawazo ya kila namna yanapokelewa.
 
Back
Top Bottom