Nimesahau mzigo ndani ya basi

Mkuu ili linawezekana kweli? Msaada tafadhali
 
mmmh
 
Bag ya laptop haifai hata kuweka kwenye carrier maana mtu anaweza kupita nayo hata ukisinzia.

unaweza kukuta hata mtu anaefanya usafi amepita nalo.
 
Muhusika ni mpuuzi inamaana ulimpompigia kuwa umesahau begi lako alikuwa hajui gari imeondoka na dereva gani na konda gani .ili waangalie mzigo wako wauhifadhi.??? Kampuni nzima unapaswa kuishitaki kwa kuweka namba ambazo hazipatikan. Hii inakumbusha nilishawai achwa na gari na kupoteza mizigo yangu yote na konda alikuwa anajua kabisa gari limeniacha na mzigo wangu wanaujua ila sikuwa na la kufanya mana ilikuwa kibaharia zaidi ni nchi nyingine.

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Yaani wao wanakomalia kuwa mzigo wa ndani hawana dhamana nao. Pia ile route ya Dar Moro haikuwa rasmi, gari ni kama ilikuwa inatoka Dar kwenye matengenezo ndiyo wakapitia abiria pale nje ya stendi zinanako paki zile gari za IT ile mida ya usiku
 
Bag ya laptop haifai hata kuweka kwenye carrier maana mtu anaweza kupita nayo hata ukisinzia.

unaweza kukuta hata mtu anaefanya usafi amepita nalo.
Ni kweli, ila Dereva alilala humo humo ndani ya gari na mwanamke. Kondakta ndiye alilala nje hotelini/lodge
 
Kipengele cha abiria chunga mzigo wako kimewapa wafanyakazi wa basi hilo haki ya kutotiwa haitiani.
Linahesabiwa kama ni kosa la uzembe
 

Sidhani kama hao wafanyakazi wa mabus au wakata tiketi wanayo mikataba ya kudumu,wengi wao ni SAwa na barmaedi uhama kufuata maslai bora, sema labda waliprint vitabu vingi kwa namba za staff kabla awajahama. Ilitakiwa waupdate.
 
Unatakiwa umtafute kwa akili sana. Hao wafanyakazi wasijue issue yoyote. Na zaidi itakuwa vizuri uulizie kwa ma-alwatan wa stendi kwani wana info zote. Ukienda ofisi ya kukatia tiketi hawatakuambia ni nani mmiliki.
 
Kwanini uliposhuka tu chalinze na kugundua umesahau begi hukufanya taratibu ya kuwasiliana na wakala wa frester hapo chalinze akupe mawasiliano ya hilo basi lao lililoelekea Morogoro wakuangalizie begi lako? Pole huna wa kumlaumu ila ww mwenyewe
Mara nyingi hawa makondacta wanafichaga vitu ukishamuuliza tu.
 
Unatakiwa umtafute kwa akili sana. Hao wafanyakazi wasijue issue yoyote. Na zaidi itakuwa vizuri uulizie kwa ma-alwatan wa stendi kwani wana info zote. Ukienda ofisi ya kukatia tiketi hawatakuambia ni nani mmiliki.
Sawa mkuu, asante sana
 
Pole sana, bahati mbaya sana kibongo bongo ukipoteza kitu/vitu kwa namna uliyopoteza ni nadra kupata kitu/vitu hivyo...
 
Nakushauri tu next time
Uwe na laptop kama hivyo lakini pia pale nyumbani uwe na Desktop PC kwa ajili ya kufanya user data backup yaani ni muhimu sana hii. Wala usiseme utaweka kwenye External HDD. laa

Mimi natumia njia hiyo na Alhamdulillah sijawahi kupoteza PC

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Usikae mbali na vitu kama pc hata kama unaweka kwenye sehemu za kuwekea mizigo ila pendelea kubaki na begi la pc yako kamwe.


"kusahau begi langu lenye computer na vitu vingine"



Narudi nyuma kidogo, ni kuwa baada ya kujua nimesahau begi nilipiga zile namba za simu za kwenye tiketi kama nne ndipo nilipompata muhusika kwani wengi walisema wameshaacha kazi kampuni ile.

"Muhusika alipokuja mida kama ya saa kumi tukaenda kwenye bus na kukuta dereva kalala kwenye bus na akajibu kupitia dirishani kuwa hajaona hilo begi"



Huenda huyu mhusika alifanya mchongo coz pc kama hizo si chini ya 300 000

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Sure,pia siku hizi kuna cloud service nyingi tena nyingine ni free kwa kiasi flani cha data,na unaweza kuziaccess data zako ukiwa papote,hizi ni njia salama za kuhifadhi data zako hasa ambazo ni za muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…