Nimerudi Salama

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,510
19,347
Nilikuwa safarini Tabora kwa ajili ya kupiga kura. Ni uchaguzi pekee nilioshiriki tangu mwaka 1995 ambapo kura yangu nilimpigia Mrema pale Ubungo; mwaka huu nimempigia Slaa. Kama ambavyo mwaka 1995 niliamini kuwa Mrema aliibiwa kura, ndivyo vivyo hivyo ninavyoamani leo kuwa mwaka 2010 Slaa kaibiwa kura tena. Kwa maana halisi ni kuwa kura yangu haithaminiwi. Kura ya mwaka huu ilikuwa ni ghali sana kwangu kwa vile nilitumia gharama nyingi kwenda na kurudi Tanzania kuhakikisha kuwa nimeandikishwa kwenye daftari, jambo lilinihitaji kuwepo physically, na baadye kwenda kupiga kura yangu. Ingawa kulikuwa na gharama za safari, nadhani gharama kubwa zilikuwa ni zile za kukosekana kazini kwangu, ambapo ndipo mninapopatia ugali wangu wa kila siku.

Kitendo cha watanzania kuibiwa uchaguzi na kunyamaza ni sawa kabisa na kurudi kwenye utawala wa mkoloni..................................... Nitatumia muda zaidi siku za mbeleni kuongelea hili.

Kwa leo, nawaarifu rafiki zangu hapa JF kuwa nimerudi salama. Ingawa nilikuwa nasoma post zote za JF, nilikuwa nashindwa sana kuweka post zangu kupita mobile phone yangu. Nilifurahi sana kwa vile mitando yote ya Tanzania ilikuwa inanipa connection bila matatizo yoyote ingawa simu yangu ni ya AT&T
 
Back
Top Bottom