Nimeponyeka kutapeliwa na rafiki wa facebook

Dalmine

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
5,803
2,000
"Mwanamke mmoja wa kizungu aliniomba urafiki huko Facebook, nikakubali na akaruka inbox siku hiyo hiyo.

Alijitambulisha kwa jina la Dkt.Christina kutoka London, Uingereza. Akasema yeye ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto katika hospital kubwa huko London. Pia anapenda kumtumikia Mungu katika kufariji na kutoa misaada kwa wenye hali ya chini.

Pia akasema akipata likizo basi atakuja Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii, hivyo nitakuwa mwenyeji wake na angependa kufikia nyumbani kwangu (hakujua Kama mimi ni baharia naishi chumba kimoja na mtungi wa gesi ndani).

Nikajibu karibu sana. Akaomba kunifahamu kiufupi, nikamueleza na kuanzia hapo tukawa marafiki.

Basi akaniachia email yake hapo messenger kwa maana alisema kuwa sio mtumiaji sana wa Facebook hivyo nitumie email kuwasiliana nae.

Tukawa tunawasiliana kwa njia ya email. Badae akafuta picha na akaunti ya Facebook. Siku moja akaniambia kuwa walikuwa na kikao Cha wafanyakazi hapo hospital na baadhi ya wafanyakazi waliofanya vizuri walipewa zawadi. yeye alikuwa ni mmoja wao. Alipewa zawadi za laptop Hp 2, smartphone (iPhone) 1, na TV LG 1. Kwa maana yeye hakuwa na uhitaji wa vitu, basi akapata wazo la kunitumia mimi Kama zawadi ya kudumisha urafiki wetu.

Nilifurahi sana nikajua ghetto langu linakuja kunoga.

Siku moja akasema amepata dharura na anaenda Hawaii hivyo hatokuja Africa. Lakini zawadi zangu amempa rafiki yake anayeenda Senegal, ambaye ni mtumishi aliyemtaja kwa jina la Sister Janneth. Akanipa na email ya huyo Janneth ili niwasiliane nae jinsi ya kupata zawadi zangu. Janneth alikuwa akija Senegal na jopo lake kwa ajili ya kuhubiri injili na kutoa misaada.

Niliwasiliana na Janneth na akaniambia nimtumie post address yangu ili atume mzigo. Utata ulikuja pale aliponiambia kuwa nimtumie $150 kupitia benki ya Western Union ili aweze kuusafirisha huo mzigo.

Daah nilijiuliza maswali mengi sana, sasa Kama hawa wanagawa misaada wameshidwaje kunilipia gharama za kuusafirisha huo mzigo? nikapata jibu kuwa hawa Ni matapeli wa kizungu. Nikamjibu kuwa hiyo hela sina, kama vipi uza laptop moja halafu hela ya mauzo itumie kutuma huo mzigo utakaobaki.

Kuanzia siku hiyo hakunitafuta tena

Chanzo: Watu Na Story

Aisee wewe ni mjanja sana,, na inavyoonekana hauishi dar. Kama co wa mwanza bac dodoma or morogoro. Mwanaume wa dar lingemkuta hili dahh 🤣
 
Tuchki

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
1,675
2,000
Kuna mmoja Nilichat nae LinkedIn akasema yeye ni engineer yupo Egypt anataka kuja kikaz dar es salaam kuanzia July mpka leo kila siku anasema atakuja nikaja kustukia anataka nimtumie ela sijui akifika anirudishie nikamblock
 
Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
1,307
2,000
"Mwanamke mmoja wa kizungu aliniomba urafiki huko Facebook, nikakubali na akaruka inbox siku hiyo hiyo.

Alijitambulisha kwa jina la Dkt.Christina kutoka London, Uingereza. Akasema yeye ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto katika hospital kubwa huko London. Pia anapenda kumtumikia Mungu katika kufariji na kutoa misaada kwa wenye hali ya chini.

Pia akasema akipata likizo basi atakuja Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii, hivyo nitakuwa mwenyeji wake na angependa kufikia nyumbani kwangu (hakujua Kama mimi ni baharia naishi chumba kimoja na mtungi wa gesi ndani).

Nikajibu karibu sana. Akaomba kunifahamu kiufupi, nikamueleza na kuanzia hapo tukawa marafiki.

Basi akaniachia email yake hapo messenger kwa maana alisema kuwa sio mtumiaji sana wa Facebook hivyo nitumie email kuwasiliana nae.

Tukawa tunawasiliana kwa njia ya email. Badae akafuta picha na akaunti ya Facebook. Siku moja akaniambia kuwa walikuwa na kikao Cha wafanyakazi hapo hospital na baadhi ya wafanyakazi waliofanya vizuri walipewa zawadi. yeye alikuwa ni mmoja wao. Alipewa zawadi za laptop Hp 2, smartphone (iPhone) 1, na TV LG 1. Kwa maana yeye hakuwa na uhitaji wa vitu, basi akapata wazo la kunitumia mimi Kama zawadi ya kudumisha urafiki wetu.

Nilifurahi sana nikajua ghetto langu linakuja kunoga.

Siku moja akasema amepata dharura na anaenda Hawaii hivyo hatokuja Africa. Lakini zawadi zangu amempa rafiki yake anayeenda Senegal, ambaye ni mtumishi aliyemtaja kwa jina la Sister Janneth. Akanipa na email ya huyo Janneth ili niwasiliane nae jinsi ya kupata zawadi zangu. Janneth alikuwa akija Senegal na jopo lake kwa ajili ya kuhubiri injili na kutoa misaada.

Niliwasiliana na Janneth na akaniambia nimtumie post address yangu ili atume mzigo. Utata ulikuja pale aliponiambia kuwa nimtumie $150 kupitia benki ya Western Union ili aweze kuusafirisha huo mzigo.

Daah nilijiuliza maswali mengi sana, sasa Kama hawa wanagawa misaada wameshidwaje kunilipia gharama za kuusafirisha huo mzigo? nikapata jibu kuwa hawa Ni matapeli wa kizungu. Nikamjibu kuwa hiyo hela sina, kama vipi uza laptop moja halafu hela ya mauzo itumie kutuma huo mzigo utakaobaki.

Kuanzia siku hiyo hakunitafuta tena

Chanzo: Watu Na Story
hapo hakuna mzungu wala nani
Ni matapeli wa west Africa tu hapo wanataka kukuibia, na hapo ujue unachati na mtu mmoja kwenye kila account
 
Mr Devil

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
4,708
2,000
Kuna nungunungu mmoja ye alisema ni mwanajeshi wa kimarekani akanitajia na operation iliyompeleka Afghanistan,Sasa Kuna dili alikula na mabosi zake wakauza mafuta wakagawana mtonyo so wakwake akataka ausafirishe niupokee ili baadae aje anipe changu,maana kule kwao angehojiwa pesa ndefu Kama hizo katolea wapi!. Issue ilienda akanitumia hadi vitambulisho vyake vya jeshi,picha n.k! Mlolongo ulikuja kufikia mpk tukaanza kuombana hela nikaona hii ni nungunungu! Nikatupa kule.

Utapeli wa hivi mbona wa kitambo Sana na ushakuwa wakishamba sasa!. Hiyo yako pia ilishamtokea mtu wangu wa karibu na mimi ndo nilikuwa namjibu huyo daktari feki!..
Scams zipo nyingi za kutosha halafu nyengine za kijinga sana!.. Tena huku ni chamtoto dark web ndo kiboko!. Kule wanakupiga na hauna sehemu ya kushitaki dark web is dark!!. Niliwahi jaribu kutaka kuvuna Bitcoin kule kumbe ni utapeli tu mwisho wasiku wanakuomba ulipie Bitcoin na wakati wanagawa Bitcoin..

Dark web Kuna watu wana njaa tu kule! Jitu moja lilishawahi niambia "we want your money".. ila nafikiri kule zipo site ambazo zinafanya kazi real ila kuzijua sasa ndo shughuli pevu!. Nachokipendea kule hamjuani ila unaweza kupewa vyanzo vya unachokitaka in deeply ila ujue kuchuja!. Kwenye huu ulimwengu unatakiwa utumie akili yako vizuri.
hii ata mimi tayari alikua mwanajeshi wa kike kaji tambulisha kwa picha na dollars zipo kwenye beg anajiita sargent Eve..ni mda kidogo
 
Dead Man

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
695
1,000
Punguza tamaa uchwara ndugu,
Huyo sio mzungu huyo ni Mnigeria hizo ndio ishu zao, Hujifanya either demu wa kizungu au Man wa kizungu kutapeli wetu.
Hii haijampata yeye.
Uzi huu una maudhui haya HAPA

WatuNiStory
kutoka ukurasa wa W A T U
 
Dead Man

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
695
1,000
Aisee wewe ni mjanja sana,, na inavyoonekana hauishi dar. Kama co wa mwanza bac dodoma or morogoro. Mwanaume wa dar lingemkuta hili dahh 🤣

Aliye simulia hii anatokea Dar.

Uzi huu una maudhui haya HAPA

WatuNiStory
kutoka ukurasa wa W A T U
 
sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
4,570
2,000
Wanigeria ni wahuni sana aisee , sema wapo maboya ambao wanatuma hiyo pesa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom