Nimeponyeka kutapeliwa na rafiki wa facebook

seifutz

Member
Jul 18, 2021
34
113
"Mwanamke mmoja wa kizungu aliniomba urafiki huko Facebook, nikakubali na akaruka inbox siku hiyo hiyo.

Alijitambulisha kwa jina la Dkt.Christina kutoka London, Uingereza. Akasema yeye ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto katika hospital kubwa huko London. Pia anapenda kumtumikia Mungu katika kufariji na kutoa misaada kwa wenye hali ya chini.

Pia akasema akipata likizo basi atakuja Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii, hivyo nitakuwa mwenyeji wake na angependa kufikia nyumbani kwangu (hakujua Kama mimi ni baharia naishi chumba kimoja na mtungi wa gesi ndani).

Nikajibu karibu sana. Akaomba kunifahamu kiufupi, nikamueleza na kuanzia hapo tukawa marafiki.

Basi akaniachia email yake hapo messenger kwa maana alisema kuwa sio mtumiaji sana wa Facebook hivyo nitumie email kuwasiliana nae.

Tukawa tunawasiliana kwa njia ya email. Badae akafuta picha na akaunti ya Facebook. Siku moja akaniambia kuwa walikuwa na kikao Cha wafanyakazi hapo hospital na baadhi ya wafanyakazi waliofanya vizuri walipewa zawadi. yeye alikuwa ni mmoja wao. Alipewa zawadi za laptop Hp 2, smartphone (iPhone) 1, na TV LG 1. Kwa maana yeye hakuwa na uhitaji wa vitu, basi akapata wazo la kunitumia mimi Kama zawadi ya kudumisha urafiki wetu.

Nilifurahi sana nikajua ghetto langu linakuja kunoga.

Siku moja akasema amepata dharura na anaenda Hawaii hivyo hatokuja Africa. Lakini zawadi zangu amempa rafiki yake anayeenda Senegal, ambaye ni mtumishi aliyemtaja kwa jina la Sister Janneth. Akanipa na email ya huyo Janneth ili niwasiliane nae jinsi ya kupata zawadi zangu. Janneth alikuwa akija Senegal na jopo lake kwa ajili ya kuhubiri injili na kutoa misaada.

Niliwasiliana na Janneth na akaniambia nimtumie post address yangu ili atume mzigo. Utata ulikuja pale aliponiambia kuwa nimtumie $150 kupitia benki ya Western Union ili aweze kuusafirisha huo mzigo.

Daah nilijiuliza maswali mengi sana, sasa Kama hawa wanagawa misaada wameshidwaje kunilipia gharama za kuusafirisha huo mzigo? nikapata jibu kuwa hawa Ni matapeli wa kizungu. Nikamjibu kuwa hiyo hela sina, kama vipi uza laptop moja halafu hela ya mauzo itumie kutuma huo mzigo utakaobaki.

Kuanzia siku hiyo hakunitafuta tena

Chanzo: Watu Na Story
 
Mimi hivo hivo tukawa tunachat kwa kiingereza , akawa anaomba hela weee baadae kabisa ananieleza kwa kiswahili ina maana hata hamsini elfu haipo nikastuka nikajua sio mzungu wala nini kanyaboya tu
Duhh
 
Back
Top Bottom