Nimepigwa na Askari na kuumizwa, nipo Hospitali

Pole sana asee! ila nahic kuna ki2 hujakisema na hujakisema makusudi
View attachment 1076020

Mimi ni mwananchi, mfanyabiashara naishi Mbagala jijini DSM katika Wilaya ya Temeke.

Leo tarehe 19/04/2019 majira ya saa nne asubuhi ndani ya kituo cha Polisi cha Maturubai, Mbagala nimeshambuliwa bila hatia yoyote na askari Polisi anayefahamika kwa jina la Friday Mgina akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi na amenishambulia mbele ya askari wenzake na amepora gari langu aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T615 DBX na kuondoka nalo na mpaka sasa sijui hilo gari lipo wapi.

Kwa sasa nipo hospitali ya serikali Mbagala Zakhiem kwa ajili ya matibabu ila hali yangu ni mbaya kwani nikikohoa natoa damu na nikipiga chafya natoa damu.

Nawaomba viongozi wangu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wapate taarifa ili hata nikifa ifahamike chanzo cha kufa kwangu ni kipigo nilichopewa na askari huyu.

Pia naomba sana taarifa hizi zimfikie Rais wangu mpendwa aone jinsi mwananchi wake nisiye na hatia nilivyoteswa na kuumizwa na Askari Polisi.
 
Nchi za wenzetu, askari ni rafiki wa raia ila huku kwetu mambo ni tofouti kidogo..

Hii chuki inayopandikizwa haitowaacha salama siku za usoni..

kuna rafiki yangu kapoteza kitambulisho cha NIDA hata kwenda polisi kushtaki anaogopa. Yaani polisi hawako friendly kabisa na raia wanawaza negativity tu. something is wrong kwenye mafunzo yao.
 
Nilikuwepo pale saa 5 asubuhi. Ulikua ushaondoka?
Mimi ndio maana nawachukia askari siwapendi hata iweje.
Kwani wao wanakupenda? Ata mimi pindi nipo shule ya msingi niliwachukia sana walimu kumbe nilikuwa nakosea,ile ndio professional yao, ata ungekuwa ndio unaifanya wewe lazima ungekaa kwenye ethics izo izo, respect to each other !!!!!!!!
 
Askari kazi yake ni kukamata kama umetenda kosa na sio kupiga watu
Hao askari labda Wa INDIA ndio watakukamata kama mwali af wakuseme mpaka ulie, uku Africa lazima ulegezwe kwa mambata,faulo,mabanzi, iv unajua kazi ya askari ni risk?
 
Back
Top Bottom