Nimepigwa na Askari na kuumizwa, nipo Hospitali

Supa_baba

Member
Apr 19, 2019
5
18
E0A41CE4-EC82-440A-896D-12FA8ED7610E.jpeg

Mimi ni mwananchi, mfanyabiashara naishi Mbagala jijini DSM katika Wilaya ya Temeke.

Leo tarehe 19/04/2019 majira ya saa nne asubuhi ndani ya kituo cha Polisi cha Maturubai, Mbagala nimeshambuliwa bila hatia yoyote na askari Polisi anayefahamika kwa jina la Friday Mgina akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi na amenishambulia mbele ya askari wenzake na amepora gari langu aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T615 DBX na kuondoka nalo na mpaka sasa sijui hilo gari lipo wapi.

Kwa sasa nipo hospitali ya serikali Mbagala Zakhiem kwa ajili ya matibabu ila hali yangu ni mbaya kwani nikikohoa natoa damu na nikipiga chafya natoa damu.

Nawaomba viongozi wangu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wapate taarifa ili hata nikifa ifahamike chanzo cha kufa kwangu ni kipigo nilichopewa na askari huyu.

Pia naomba sana taarifa hizi zimfikie Rais wangu mpendwa aone jinsi mwananchi wake nisiye na hatia nilivyoteswa na kuumizwa na Askari Polisi.
 
Pole sana. Askari wameagizwa kutuua siku hizi. Una bahati unapumua. Angekuua sasa hivi Mambosasa angekuwa anasema wewe ni jambazi na ulirushiana risasi askari wake. Kwa sababu ya mafunzo mazuri, askari wakakuwahi.
View attachment 1076020

Mimi ni mwananchi, mfanyabiashara naishi Mbagala jijini DSM katika Wilaya ya Temeke.

Leo tarehe 19/04/2019 majira ya saa nne asubuhi ndani ya kituo cha Polisi cha Maturubai, Mbagala nimeshambuliwa bila hatia yoyote na askari Polisi anayefahamika kwa jina la Friday Mgina akiwa amevaa sare za Natafakari kuachana na Mitandao ya simu ya Tanzania baada ya TCRA kukosa weledi na kusababisha usumbufu wa kijinga sanaJeshi la Polisi na amenishambulia mbele ya askari wenzake na amepora gari langu aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T615 DBX na kuondoka nalo na mpaka sasa sijui hilo gari lipo wapi.

Kwa sasa nipo hospitali ya serikali Mbagala Zakhiem kwa ajili ya matibabu ila hali yangu ni mbaya kwani nikikohoa natoa damu na nikipiga chafya natoa damu.

Nawaomba viongozi wangu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wapate taarifa ili hata nikifa ifahamike chanzo cha kufa kwangu ni kipigo nilichopewa na askari huyu.

Pia naomba sana taarifa hizi zimfikie Rais wangu mpendwa aone jinsi mwananchi wake nisiye na hatia nilivyoteswa na kuumizwa na Askari Polisi.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom