Mungu amenisaidia nimekuwa mtu wa kwanza kituoni kwangu kupiga kura. Nilifika saa 11 na dakika 33 (05h33) na kituo kilifunguliwa saa 12 na robo (06h15) na nilipiga kura yangu saa moja na dakika nne asubuhi hii (07h04).
Pia nemefurahi kutimiza /kufikisha messages 1000 leo hii.
Utaratibu ni mzuri lakini inaelekea hata wasimamizi wa vituo mambo mengine hawayaelewi. Kwa kuwa nilikuwa wa kwanza kufika ilibidi niwasaidie watu wengine kutambua sehemu yao ya kupiga kura.
FFU wamejaa kwenye vituo na magari ya jeshi (JWTZ) ndio yanayosaidia usafari wa viti (nimeona kwa macho yangu) na vitu vingine.
Tatizo ni kwamba kura yangu sio siri (kunja kiganja na nyoosha vidole viwili huku vingine ukibaki umevikunja)
naam hapa kilima hewa tayari tushapiga kura kwa amani na sasa nnaelekea amani kwa wazee pale barazani kupata kahawa na kutafuna kashata nikisubiri habari moja mbili hadi jioni nianze kujipanga kupokea matokeo
mji unazizima kwa ukimya watu wote kama wamepigwa na butwaa
Mimi nipo ktk kituo cha Mbagala kizuiani hapa. Foleni ni ndefu na wadau wanaenda kupiga kura huku tukiwa na kumbu kumbu ya swala letu la kulipukiwa mabomu kugeuzwa la kisiasa.
Nipo kwenye foleni bado natamani nipewe karatasi hata mia niwekeke tick kwa shujaa, Dr wa ukweli.
Hivi siruhusiwi kuweka X kwenye picha ya JK?
Nimekwisha piga kura yangu nakwenye kituo changu ulinzi umekamilika kwani mmoja wa maagent nimemuona mwanafunzi wa chuo kikuu ambae hawawezi kumdanganya!!
Wasiwasi wangu uko kwenye vituo ambako chadema hawajasimamisha wagombea Ubunge , huko kama hawakuwekwa wasimamizi imara ni sehemu ambayo hawa mafedhuli wanaweza kujazi kura za wizi za urais!! Hopefully hili limethibitiwa.