Nimepewe urithi wangu mapema, nimechanganyikiwa

Nimepewe urithi wangu mapema, nimechanganyikiwa

Tafuta mademu wakali uwagonge sana ili upate akili ya kutafuta pesa zako mwenyewe.
Mshauri vizuri, USIMUONEE WIVU, mungu ndiye hupanga mja wake apate kwa namna gani, ukiumbiwa ugumu stahimili magumu.
 
Tuagize kwa uzi wako ndio utawajua watanzania jinsi gani walivyo na wivu, Nunua banda lako, lengo point nzuri Anza biashara zako kwa mtaji wa million moja tu, zingine hifadhi bank.
 
Nimepata nyumba chamazi kwa ml 15 sasa nawaza hiyo inayobaki
Achana na haya mawazo ya kizee mkurugenzi. Hiyo hela utenda tu kuizika, na biashara ya milioni 3 haiwezi kukutoa hapo ulipo na kukupeleka mbali zaidi.

Tuliza kichwa hata kwa miezi miwili mitatu hivi, angalia unamudu shughuli/biashara gani ya kukuingizia kipato; halafu tumia hiyo hela kuanzisha hiyo shughuli/biashara.

Mambo yakienda vizuri, utakuwa na jeuri ya kununua nyumba hata Masaki! Na siyo Chamazi tena.
 
Mwaka 2016 namimi nilipata hela ya urithi milioni 18.9 kipindi hicho nilikua chuo. Kwa namna fulani najilaumu nilivyoitumia kwa sababu kama ningea zisha biashara ingenisaidia sana mpaka saivi lakini ya Mungu mengi ila haya ni machache niliyofanya.

Niliweka fixed account ya mwaka mzima milion 8 nikapewa asilimia 6 hii risiti ninayo mpaka saivi.

Nilimkopesha bro wangu milioni 5 ili amalizie ujenzi. Baada ya muda fulani alianza kunilipa laki 5 kila mwezi mpaka akakamilisha deni lote hii kwa namna fulani ilifanya nikawa na matumizi mabaya ya hela.

Nilipata shamba Rukwa vijijini uko eka 3 kwa milioni 1. Wakati huo huo Vodacom wakatangaza wanauza share nikaenda kuweka laki saba kununua hisa zao ambazo nimepokea dividends mara mbili tu

Nilinunua kiwanja kwa milion moja, hiki mpaka sasa kipo ila sijakiendeleza bado. Pia baada ya ile hela kumature nilinunua shamba la mpunga eka 4 kwa milion 4. Pia kipindi hicho nikaanza biashara ya kununua mpunga na kuja kuuza baadae ilinifaidisha kiasi ila sikuwa consistency hivyo mtaji ulikufa.

Toka nilipopokea hiyo hela nilianza kujilipia ada chuo. Mpaka kufika 2019 mwishoni ndio pesa ilikua inaishia na mimi ndio chuo namaliza na hapo ndio rangi zikaanza kuonekana asee nilikula msoto wa maana hasa 2020 wakati ndio napata mtoto wa kwanza hakuna ndugu anayekusikiliza akusaidie ila nashukuru kaka na dada angu walinisaidia kidogo.

Kuna kitu kinaniambia mimi sina nidhamu ya pesa kwa sababu kuna jamaa yangu alipewa mtaji wa laki 5 akaanza biashara ya m-pesa sasa hivi amejenga kwa biashara hiyo pia ana vibanda vingine vinne anafanya biashara ya uwakala mkuu kwenye hivyo vibanda vinne mtaji milioni 14 hii ya uwakala mkuu sijui ana mtaji kiasi gani.

Mkuu nakushauri fanya maamuzi ya maana kabla hujaja kujilaumu baadae.
 
Hilo wazo lako ni zuri.
Njoo Chanika ununue nyumba ya milioni 12, milioni 1 nunua furniture na hiyo nyingine fanya biashara unayoipenda.
Usifanye jambo lolote tofauti na hilo wazo lako.
Humu wapumbavu ni wengi sana.
Acha kumpoteza kijana ....hiyo hela aingize kwenye biashara
 
Fungua accountya tigo pesa..
Jiunge na tigo kibubu ziweke hizo pesa ...gawio elf 50 had 70 kila mwez
Wakat unatafakari cha kufanya
 
Bora ununue shamba maeneo ya nyanda za juu kusini chapili nenda veta fungua mashine za mbao na mashine za tofali na kuchomelea weka Bank million nane
 
Acha Uboya Tafuta Kiwanja Goba (Tegeta A) Nunua Cha Not Less Than 800 sqm for about 12 - 15 M hyo nyingine nunua bajaj used register uber / bolt ingia mtaani komaa starehe weka pembeni.

Biashara hutaweza simply huna experience ya biashara, biashara zinazodumu ni zile unazo anza nazo from scratch with little capital. Usipende kuanza biashara yeyote na hela nyingi, it will not work.

Like i said anza na bajaj used. Hutajuta

Utakuja Siku Moja Utaniambia, Blaza Kweli Ulinishauri. Naku hakikishia Hutajuta.
 
Kila la kheri, usijali bado kuna za mirathi baada ya kifo...
 
Wakubwa Kwema?

Kama kichwa cha Habari kinavyoeleza hapo juu
Mimi ni kijana wa miaka 24, nimepewa Urithi wangu mapema kiasi cha milion 18 net.

Nimeambia hizo pesa nikizifanyia ujinga ndiyo basi tena nitakuwa sina kitu kwa mzee sasa nimewaza kununua hata kijumba cha milioni 14 nje ya Dar es salaam hata cha vyumba viwili.

Halafu 4 inayobaki nijaribu kuitia kwenye biashara yoyote itakayoweza kuizalisha sasa wakuu napagawa kwa sababu sikujipanga nisaidie kwa lolote hiyo kwangu ndo karata ya mwisho
Kama uko serious na hii issue, mfate mzee wako akueleze cha kufanya kwa uangalizi wake maana wewe bado mdogo
 
18M ni ndogo sana kwa biashara ila ni nyingi mno ukiisikia. Tulia nayo. Unaenda kununua nyumba kwani hapo umefukuzwa? Investment ya nyumba ni ujinga sana maana return yake ni ndogo sana. Jitulize la sivyo mzee atakupa laana ya maisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom