Nimepewe urithi wangu mapema, nimechanganyikiwa

Nimepewe urithi wangu mapema, nimechanganyikiwa

Njoo nikuuzie 40*40 kwa 7m nje kidogo ya mji mpaka ukijenga hivyo vyumba viwili utatumia 1.5 unabakiwa na hela unaweza kufuga na kutafuta biashara ya kufanya mjini

Sehemu gan mkuu
 
Hilo wazo lako ni zuri.
Njoo Chanika ununue nyumba ya milioni 12, milioni 1 nunua furniture na hiyo nyingine fanya biashara unayoipenda.
Usifanye jambo lolote tofauti na hilo wazo lako.
Humu wapumbavu ni wengi sana.

Chanika sehemu gan mkuu
 
Wakubwa Kwema?

Kama kichwa cha Habari kinavyoeleza hapo juu
Mimi ni kijana wa miaka 24, nimepewa Urithi wangu mapema kiasi cha milion 18 net.

Nimeambia hizo pesa nikizifanyia ujinga ndiyo basi tena nitakuwa sina kitu kwa mzee sasa nimewaza kununua hata kijumba cha milioni 14 nje ya Dar es salaam hata cha vyumba viwili.

Halafu 4 inayobaki nijaribu kuitia kwenye biashara yoyote itakayoweza kuizalisha sasa wakuu napagawa kwa sababu sikujipanga nisaidie kwa lolote hiyo kwangu ndo karata ya mwisho
Una shughuli gani kwa Sasa? Nakushauri iweke benki, na isahau mpaka utakapokuwa umetulia na kuangalia mazingira yatakayokuwezesha kuizungusha na kuzalisha zaidi.
 
Nimepata nyumba chamazi kwa ml 15 sasa nawaza hiyo inayobaki
Nyumbani itakuingizia kipato? Pesa tayari unayo, usikurupuke kuifanyia lolote, ihifadhi sio kwa mtu bali benki utafakari kwa utulivu nini cha kufanya.
 
Nyumbani itakuingizia kipato? Pesa tayari unayo, usikurupuke kuifanyia lolote, ihifadhi sio kwa mtu bali benki utafakari kwa utulivu nini cha kufanya.
Nyumba ni zaidi ya bank,atakula vichwa,benk haizai
 
Wakubwa Kwema?

Kama kichwa cha Habari kinavyoeleza hapo juu
Mimi ni kijana wa miaka 24, nimepewa Urithi wangu mapema kiasi cha milion 18 net.

Nimeambia hizo pesa nikizifanyia ujinga ndiyo basi tena nitakuwa sina kitu kwa mzee sasa nimewaza kununua hata kijumba cha milioni 14 nje ya Dar es salaam hata cha vyumba viwili.

Halafu 4 inayobaki nijaribu kuitia kwenye biashara yoyote itakayoweza kuizalisha sasa wakuu napagawa kwa sababu sikujipanga nisaidie kwa lolote hiyo kwangu ndo karata ya mwisho
Nyumba haitakuongezea kipato cha kudumu
 
Kama zinakuchanganya bado kazinunulie nyumba zote achana na biashara inalipa kwenye makaratasi
Kama mtu ana miaka 24 na ana changanyikiwa na milioni 18 mwache

Hakusoma mchezo wa maisha
 
Mnaomba ushauri bila kutaja conditions mnatutia uvivu, ngoja nikupe in general. Chukua milioni 10 weka fixed account miezi sita. Unabaki na 8M

Milioni 3 agiza incubator ya mayai si zaidi ya 2000 hivi hela hiyo inatosha kununua, kusafirisha hadi Dar endapo uko jiji hili. Hapo inabaki 5M

After a month hapo ushafanya research na unasubiri incubator ifike kwani itachukua kama 50 days from ordering day mpaka kushushwa bandarini mpaka godown, panga chumba maeneo ya Kimara au eneo lolote lenye wafugaji wengi wa kuku, itategemea na research yako. Lipa kama 100k per month, ukilipa kodi ya 6months ni 600k plus hela ya kununua vitu 1.4M jumla ni 2M, hakikisha hapo kuna eneo la kutosha na sio mjini sana. Unabaki na 3M.

Wakati huo toa 1M ya kutumia kwenye vitu vya kijinga, hela inawasha siku zote. Unabaki na 2M hiyo ishi nayo tu kazi yako kutotoreshea watu vifaranga. Utaongeza mambo mengine kwenye huo ujasiriamali.

After 6 months ushaijua biashara toa 10M ikuze. Hiyo ni idea moja tu, zipo nyingi
Unaongea kama kitu rahisi vile
 
Kwakua tayari kuna mtu anajiita mzee wa upako, we unatakiwa ujiite mzee wa kuwapaka alafu utenge 1M kila wikendi uwe unatafuta viwete wa mchongo wawili unawapa posho ya elf 10 unawaombea hadi wapone, hadi 1M iishe unakua umewaombea viwete wa mchongo 100 tayari Ni mtaji huo, unasubiri faida sasa huku ukijiita mzee wa kuwapaka

Kama zumaridi ana wenge kiasi kile lakin watu wamemuamini maana yake mchongo uko kule
Hahahaaa.

Tangu nianze kuona watu wanaombewa na hawa wanaojiita manabii/mitume na wanapona, sikuwahi kuwaamini hata siku moja.

Mjini shule, akili ina run mambo
 
1. Ziweke fixed kwanza huku ukipunguza wenge na kufikiria kwa umakini.

Ziweke fixed hata miezi 3 huku uki brainstorm.

2. Kila biashara inalipa ukihadithiwa.

Nachokushauri kwenye biashara "FOLLOW UR PASSION""

Au kama vipi Tuagize biaaa

#YNWA
Hujasikia msururu wa mabenk yakifilisika???

Kuweka pesa benk kipind hiki ni bonge la kamar husuusan pesa ya ngama km hiyo

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
UKinunua nyumba umepotea tayar..... tqfuta fani yeyote ya kusomea veta... halafu hiyo milioni 14 weka fixed deposit kwanza kichwa kitulie
Nilikuwa nasubiri hii comment... Veta mpango mzima... Au kama vipi akajifunze ukinyozi, akafungue goli lake sehemu
 
Achana na mambo ya kujenga, itaisha hela ndogo sana hiyo...tafuta fani yoyote uanze kuingiza hela ya mboga wakati unawaza biashara kubwa ya kufanya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom