Nimepewa invoice ya kumnunulia matairi ya Prado, Jamani wadada!!!

Nimepewa invoice ya kumnunulia matairi ya Prado, Jamani wadada!!!

Ina maana sisi wanaume wenye kipato cha chini ndio wa kunyanyasika siyo. Nimemtokea mdada mrembo mwenye maisha yake ya uhakika. Nimemkomalia sound za kufa mtu.
Leo nimeonana naye alichofanya ni kunipatia invoice ya kumnunulia matairi manne ya gari yake.
Aliniambia unanipenda, nimnunulie matairi alafu tutazungumza
Nauliiiizaaaa hhhiiiii nii haki milioni moja kasoro mimi nitaipata wapi?

Nimtukane ama!!!!!!
umtukane ili iweje?
 
Alipohitaji matairi alikuwa na maana ya mipira ya mapenzi au dawa ya penzi. Jipinde kwa mangi fasta chukua zako nne, inaonekana huyo demu ana usongo na wewe ile mbaya mpaka anahitaji vi-nne kazi unayo, kula vizuri kwanza.
 
ha haaaa, sasa watoto wa mujini wanaweza tumia tairi za kichina?
au ndo yale tairi moja wananunua watu8?
maana mjini hapa unaweza dhani unamjengea mtu nyumba kumbe hiyo nyumba mnaijenga watu 5, chezeya watoto wa mujini wewe

unachukua gari.....unaenda nayo kariakoo ukimrudishia ina tairi nne mpya....kashata kuuuubwa utafikiri BG/PIRELLI kumbe mchina moja 200,000/- tu......
 
Inawezekana kabisa anakupima kujua unaweza kumnunulia hayo matairi anayotaka,kuna maswali najiuliza,wakati unamtongoza inaonekana kabisa ulijiweka juu sana kiasi kwamba huyo mwanamke anakuona bab kubwa ndio maana kaona hata kukupa hiyo invoice ni jambo dogo kwako,kama kweli unampenda ikwa dhati ya moyo wako ilifaa umwambie hali halisi ya maisha yako kwani inatambulika kabisa kuwa mapenzi si pesa wala kipato.
Bado una nafasi ya kumwambia ukweli na akakupenda kulingana na hali ya maisha yako ilivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom