Mkuu, sidhani kama miezi miwili tu inaweza kuwa kipimo sahihi, jitahidi sana kumjifunza mwenzako vizuri.
Pili, kukimbilia kukutana naye kimwili sio jambo jema sana kwa afya yako na utu wako pia, nikimaanisha kadiri unavyojirahisisha kwa tamaa zamwili wako, ndivyo pia unajiexpose kwenye matatizo mengi sana. Yafaa kwanza ujue afya yako vizuri then ujue na yake pia, ambayo si chini ya miezi mitatu kupata majibu sahihi. Kukimbilia hio mambo inakupunguzia asilimia kubwa sana ya trust kwa mwenzio kwa kujua au pasipo kujua, wengi wanajiuliza; yaani miezi miwili tu ananisumbua kiasi hiki? Ikitokea nimeumwa? au kipindi cha ujauzito, au baada ya kujifungua, mwenzangu atanivumilia kweli kwa uaminifu? Je akisafiri/nikisafiri kwa muda kuna subira kweli apo? N.k, n.k.
Kaka jipe muda, pia kutokusoma sana kusikunyime kusimama kama mwanaume, Ndugu yetu mmoja alioa Mke form four yeye la saba (yeye ni fundi ujenzi), akamwendeleza mkewe akawa mwl wa primary, akasoma 5&6 akaenda mlimani kwa degree ya kwanza na ya pili, Japo mwanamke alianza dharau za apa na pale lakini Jamaa alisimama ngangari kwenye nafasi yake kama mwanaume na kusimamia majukumu yake kama mwanaume, hadi leo wanaishi kwa amani na upendo. kikubwa zingatia amani ya moyo wako.
''heri kula mboga za mwituni ukiwa na amani kuliko kula pamoja na wafalme bila ya amani Kila la kheri kaka