Hongera sana mkuu, ukikaa ukitafakari kwa makini, yale yote ambayo ulitamani wewe ufanyiwe wewe, sasa ndio wakati wake wa kuyalipa kwa mwanao. yale yote pia ambayo wazazi walikuzuia kuyafaanya utotoni mwako jaribu pia kuyafikiria, yale unayoona yalifaa uyafanye lakini ukanyimwa hio fursa, ni wakati pia wa kumaptia mwanao hayo.
Upendo wa kweli kwa mtoto ni pamoja na kumuonya na ikibidi kiboko kwa wakati wake azawadiwe, asikudanganye mtu kiboko kimetusaidia sana wengi wetu kuwa watu wema.
Pia Mkuu, akikua usimzoeshe kufanyiwa kazi na house girl, mfunze kutandika kitanda chake mwenyewe, chombo chake cha kulia ajue kukiosha, usafi na nguo zake afue mara moja moja mkuu pia kazi nyingine za nyumbani afanye. itamsaidia sana na atakuwa mkubwa akiwa responsible.
Maneno machache ya hekima yasema hivi
Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Mithali 13:24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
Mithali 22:15Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Waefeso 6:4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.