Nimepata Mpenzi ila mh..! Ushauri wenu wakuu

Nimepata Mpenzi ila mh..! Ushauri wenu wakuu

Kimbia na usiangalie nyuma. Mpgaji huyo c unajua kwa sasa hawana namna wanakuja kwa style tofaut. Pole sn muombe Mungu atakupa a right person.
nshakimbia mpendwa! ahsante
 
Baada ya kupona maumivu ya kuachana na mpenzi ambaye nilitegemea atakua mume wangu, Mungu si athumani nikakutana na kaka mmoja ambae tulijikuta tunaanzisha mahusiano. Kaka huyu anafanya kazi Mkoa mwingine, ila huku nilipo mimi ndio kwao. kipindi nilipokutana nae alikua kaja likizo hivyo baada ya likizo yake kuisha tuliagana vizuri na mawasiliano yaliendelea vizuri tu, akiniahidi mwezi wa tisa ataleta barua ya uchumba nyumbani, na Mungu akipenda basi mwakani tutafunga ndoa.

Wiki mbili baada ya kuondoka, kuna siku alinitumia sms kwamba kuna kiwanja kinauzwa huko anapoishi, nimkopeshe kiasi fulani cha pesa ili akinunue, nilishtuka maana hatuna zaidi ya miezi mitatu toka tumeanza mahusiano. Sikumjibu vibaya nilimwambia kwa sasa sina pesa akakubali kwa shingo upande. Mawasiliano yakaendelea japo sio kivilee kama mwanzoni,

Leo tena nimepokea sms akidai ana shida na laki mbili, hata kama sina basi nijitahidi hata nimkopee kwa mtu atarudisha mwisho wa mwezi huu. Ni kweli nilishaanza kumpenda, ukizingatia nimekua mpweke kwa muda mrefu. Ushauri wenu wakuu huyu kweli ana mapenzi na mimi au anataka kunitapeli then asepe????
Huyo yupo kwenye majina ya vyeti feki....so account haitasoma this month.....Fanya umpe asije akaadhirika afu ndo mmeshakubaliana....Ila angalia icje hadi mahali ukatoa ww
 
Kuna rafiki angu kipenzi sn nmstaarabu wa hali ya juu anatafta mchumba kama upo serious kweli nikuunganushe nae sahv. Sawa Yingamale?
 
sijampa bado, alisema hana haraka ya dyudyu mpaka atakapoleta mahari

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "Pigo la Uaminifu?" Hilo ndilo jamaa alilotaka kukupiga. Alijifanya hana haraka ya papuchka hadi akulipie mahari ili uone huyu ndio mwenyewe ili iwe rahisi kukuingiza kingi.

Asee tumechoka kusikia kesi za wadada kuzulumiwa na waliowahi kuwa mabwana zao. Huyo jamaa hana lengo zuri na wewe. Ila ukiamua kumpa mpe ujue kuwa umecheza kamari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom